\v 65 Wewe umemtendea mema mtumishi wako, Yahwe, sawasawa na neno lako. \v 66 Unifundishe utambuzi sahihi na uelewa, kwa kuwa nimeamini katika amri zako.