\v 9 Mwabuduni Bwana katika uzuri wa utakatifu wake, tetemekeni mbele zake, nchi yote. \v 10 Semeni kati ya mataifa, kwamba Yahwe anatawala; ulimwengu pia umeimarishwa na hauwezi kutikiswa; yeye huwahukumu watu kwa haki.