\v 4 Wale wakutafutao wafurahi na kushangilia katika wewe; wale waupendao wokovu wako siku zote waseme, "Mungu asifiwe." \v 5 Lakini mimi ni maskini na muhitaji; harakisha kwangu, Mungu; wewe ni msaada wangu nawe huniokoa mimi. Yahwe, usichelewe.