\c 141 \v 1 Ee Yahwe, ninakulilia wewe; uje upesi kwangu. Unisikilize nikuitapo. \v 2 Maombi yangu na yawe kama uvumba mbele zako; mikono yangu iliyoinuliwa na iwe kama dhabihu ya jioni.