\v 4 Mtafuteni Yahwe na nguvu zake; utafuteni uwepo wake siku zote. \v 5 Kumbukeni mambo ya ajabu aliyoyatenda, \v 6 miujiza yake na amri zitokazo kinywani mwake, enyi kizazi cha Ibrahimu mtumishi wake, enyi watu wa Yakobo, wachaguliwa wake.