\c 89 \v 1 Nitaimba sifa za matendo ya uaminifu wa agano milele; nitatangaza kweli yako kwa vizazi vijavyo. \v 2 Maana nimesema, "Uaminifu wa agano umeimarishwa milele; na kweli yako umeiimarisha mbinguni."