\c 136 \v 1 Mshukuruni Yahwe; kwa kuwa ni mwema, kwa maana fadhili zake za dumu milele. \v 2 Mshukuruni Mungu wa miungu, kwa maana fadhili zake za dumu milele. \v 3 Mshukuruni Bwana wa mabwana, kwa maana fadhili zake za dumu milele.