\v 6 Musa na Haruni walikuwa miongoni mwa makuhani wake, na Samweli alikuwa miongoni mwa wale walio muomba Yeye; walimuomba Yahwe, naye akawajibu. \v 7 Alizungumza nao toka nguzo ya wingu; walizishika amri zake takatifu, na sheria ambazo aliwapatia.