# Taarifa ya Jumla: Musa anaendelea kuzungumza na watu wa Israeli kana kwamba walikuwa mtu mmoja, kwa hiyo maneno ya "wako" na "yako" hapa ni katika umoja. # unaweza kula mizabibu idadi yoyote unayotaka "kisha unaweza kufurahia kula mizabibu mpaka utosheke" # lakini usiweke yoyote katika kikapu chako Maana kamili ya kauli hii inaweza kuwekwa wazi. "lakini haupaswi kuweka mizabibu yoyote katika kikapu chako kubeba pamoja nayo" # Utakapokwenda katika shamba la zao lililoiva la jirani yako "Utakapokwenda katika shamba la jirani yako ambapo kuna zao linaota" # unaweza kuvuna kichwa cha mavuno kwa mkono wako "kisha unaweza kula viini vya mbegu kwa mikono yako" # lakini haupaswi kutumia mundu kuvuna zao lililoiva la jirani yako "lakini usikate chini mazao yalioiva ya jirani yako na kuchukua" # mundu kifaa chenye ncha kali ambacho wakulima hutumia kuvuna ngano