# Sentensi unganishi Baada ya Kuhani Mkuu kumpatia Sauli barua, Sauli alisafiri kuelekea Dameski. # Hata alipokuwa akisafiri Sauli aliondoka Yerusalemu na kuelekea Dameski. # Ilitokea kwamba Haya ni maelezo yanayobadisha simulizi kuonyesha kwamba jambo la tofauti litatokea. # ikaangaza kotekote nuru kutoka mbinguni "nuru kutoka mbinguni ikawangaza kotekote" # Kutoka mbinguni Inaweza kuwa na maana kuwa; 1) Mbinguni, mahali Mungu anaishi au 2) Anga. # Akaanguka chini Inawezekana kwamba 1)"Sauli alianguka pekee yake chini"au 2)"Mwanga ulisababisha yeye kuanguka chini"au 3)Sauli alianguka chini kama yeyote ambaye huanguka,"Sauli hakuanguka kwa bahati mbaya. # Kwa nini unaniudhi ? Bwana alimkemea Sauli katika hali ya swali. "Unaniudhi mimi!"