# Niongoze katika njia ya amri zako "Niongoze kulingana na amri zako" au "Nifundishe kutii amri zako." Amri za Mungu zinalinganishwa na njia ambayo mtu anatembea akimtii Mungu. # Ongoza moyo wangu kuelekea Hii ni lahaja. "Moyo" hapaunamaanisha nia, hamu, na maamuzi yanayoongoza maisha ya mtu. "Unifanye nitake" # amri zako za agano "kutii amri zako za agano." Hii inamaanisha kutii amri za Musa. # kuongezeka pasipo haki "hamu ya utajiri." Hii inamaanisha utajiri unaopatikana kwa njia zisizo sawa au kuwatendea ubaya wengine.