# Sentensi unganishi Yakobo anabadilisha mada toka kwenye kuwakemea matajiri na kuwapa mawaidha waamini. # Maelezo ya jumla Kwa kufunga Yakobo anawakumbusha waamini kuhusu ujio wa Bwana na kuwapa mafundisho mafupi namna ya kuishi kwa ajili ya Mungu. # Kwa hiyo vumilieni "Kwa ajili ya hili kuweni na subira na uvumilivu" # mpaka ujio wa Bwana Sentensi hii inaelezea ujio wa Yesu, atakapoanzisha ufalme wake duniani na kuhukumu watu wote. "Mpaka Kristo atakapokuja" # Mkulima Katika mazungumzo haya Yakobo anatumia mkulima na mwamini kuelezea namna ya kuwa mvumilivu. # Kazeni mioyo yenu Yakobo anawataka waamini wawe na mioyo thabiti na kuwa na msimamo. "Kuweni na msimamo" au "Ifanyeni imara mioyo yenu" # kuja kwake Bwana ni karibu. "Bwana atarudi mapema"