# Taarifa ya jumla. Neno "ninyi" linamaanisha waamini waliotawanyika ambao Yakobo anawaandikia. # Sogeeni karibu na Mungu, na yeye atakaribia karibu nanyi Hapa anamaanisha kuwa wakweli na wazi kwa Mungu. # Safisheni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na takaseni mioyo yenu, enyi wenye nia mbili. Hizi ni sentensi mbili zinazoendana. # Safisheni mikono yenu Hii ni amri kwa watu kufanya mambo ya haki na sio maovu. "Ishini namna ambavyo inampendeza Mungu" # Takaseni mioyo yenu "mioyo" inamaanisha mawazo ya mtu na hisia zake" Mheshimu Mungu kwa mawazo yako" # nia mbili "Nia mbili" linamaanisha mtu ambaye hawezi kufanya maamuzi juu ya jambo fulani. "Mtu ambaye hawezi kuamua amtii Mungu au la" # Huzunika, omboleza, na Lia Maneno haya matatu yana maana moja. Yakobo anayatumia kwa pamoja kuonesha kuwa watu watahuzunika sana kwa kutokumtii Mungu" Yakobo anasema haya kama amri. # Geuzeni kicheko chenu kuwa huzuni na furaha yenu kuwa maombolezo Hapa kicheko kimezungumzwa kuwa kitageizwa kuwa huzuni na furaha kuwa maombolezo. "Acheni kucheka na mtubu kwa Mungu" # Nyeyekeeni wenyewe mbele za Bwana "Jinyenyekezeni mbele za Mungu" # Atawainua juu Yakobo anazungumza namna ambavyo Mungu anamuheshimu mtu mnyenyekevu na kumnyanyua toka chini. "atakuheshimu wewe"