# Bahari iliwatoa wafu ... Kifo na kuzimu viliwatoa wafu Hapa Yohana anazungumzia bahari, kifo na kuzimu kana kwamba ni watu hai. # wafu walihukumiwa Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Mungu aliwahukumu wafu" # Kifo na kuzimu zilitupwa Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Mungu alizitupa kifo na kuzimu" au "Malaika wa Mungu walizitupa kifo na kuzimu" # kuzimu Hapa "kuzimu" ni njia nyingine ya kusema mahali ambapo wasioamini wanapokwenda pale wanapokufa ili kusubiri hukumu ya Mungu. # mauti ya pili "kufa mara ya pili." Hii inaelezwa kama adhabu ya milele katika ziwa la moto katika 20:13 na 21:7. "kifo cha mwisho ni ziwa la moto" # Kama jina la yeyote halikupatikana limeandikwa Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Kama malaika wa Mungu hawakupata jina la mtu" # litupwa ndani ya ziwa la moto Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "malaika alimtupa katika ziwa la moto" au "malaika alimtupa mahali ambapo moto unawaka milele"