# Taarifa ya Jumla: Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania. # Taarifa ya Jumla: Zaburi hii ni wimbo kuhusu uaminifu wa Mungu. # Kwa mwanamuziki mkuu "Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu" # Yeduthuni Mmoja wa wanamuzi wakuu wa Daudi alikuwa na jina hili. Hii inaweza kumaanisha ni yeye. # Zaburi ya Daudi Maana zinazowezekana ni 1) Daudi aliiandika zaburi au 2) zaburi inamhusu Daudi au 3) zaburi iko katika mtindo wa zaburi za Daudi. # wokovu wangu unatoka kwake "yeye ndiye anayeniokoa" # Yeye pekee ni mwamba wangu na wokovu wangu Mwandishi anazungumzia uwezo wa mungu kumlinda kana kwamba Mungu ni mwamba. "Yeye pekee ndiye anayeweza kunilinda na kuniokoa" # yeye ni mnara wangu wa juu Mwandishi uwezo wa Mungu kumlinda kana kwamba Mungu ni mnara wa juu. "ananiepusha na kushikwa na adui" # sitasogezwa sana "hakuna kitu kinachoweza kunisogeza kamwe"