# sentensi unganishi Yuda anatumia mifano mingi kumfafanua mtu asiye na utaua. Anawambia waamini jinsi wanvyo paswa kumtambua mtu huyu miongoni mwao. # Hawa ni wale "Hawa" ina rejea kwa watu waovu. # miti iliyopukutika isiyo na matunda Kama baadhi ya miti isiyozalisha matunda katika mwisho wa majira ya joto, hivyo watu hawa waovu hawana imani na kazi za haki. # bila matunda, kufa mara mbili Kama miti ambayo imeuawa mara mbili kama vile kwa baridi usingeweza kutoa matunda, kwa hiyo watu waovu hawana thamani na hawana maisha ndani yao. # iliyong'olewa na mizizi Kama miti ambayo imeng'olewa kwenye udongo na mizizi yake, watu waovu wametenganishwa kutoka kwa Mungu ambaye ni chanzo cha maisha. # pori la mawimbi ya bahari Kama mawimbi ya bahari yanayosukumwa na upepo mkali, hivyo watu waovu hawakuwa na msingi wa imani na walihamishwa kwa urahisi katika mwelekeo mwingi. # yakitoa aibu yao wenyewe Kama upepo usababishao pori la wimbi kukoroga povu chafu, hivyo watu hawa kwa kupitia mafundisho ya uongo na matendo huwa aibisha wenyewe. AT: "kama vile wimbi huleta povu na uchafu, watu hawa wanachafua wengine kwa aibu yao." # Nyota zinazo randaranda, ambao weusi wa giza umetunzwa kwa ajili yao milele Kama vile nyota zitembeavyo angani na kufanya ugumu kuzifuata, hivyo na wewe usiwafuate watu hao.