# mabwana zake wale wanao mmiliki yule msichana mtumwa # tumaini la faida Hii inamaanisha ule uwezo wa kubashiri aliokuwa nao yule msichana na watu kumlipa kwa kuwabashiria. # kuwaburuza wao Mabwana waliwaburuza "Paulo na Sila" lakini siyo kundi lote akiwemo Luka na Timotheo. # mbele ya wenye mamlaka 'Katika uwepo wa mamlaka' au 'kuhukumiwa na mamlaka # Walipowafikisha kwa mahakimu, walisema, "Baada ya mabwana kuwaleta Paulo na Sila mbele ya mahakimu, mabwana wale wakasema" # Wanafundisha "Paulo na Sila wanafundisha" # siyo ya kisheria mabwana wanajumuisha mambo ya kitawala katika madai yao kwani wao pia walikuwa raia wa Kirumi