# Taarifa ya Jumla: Asafu anazungumza kwa niaba ya Israeli. Anaanza katika mstari wa 8 kuzungumzia jinsi Mungu alivyowaweka Israeli katika nchi yao kana kwamba Mungu alikuwa ni mtu anayesafisha ardhi ili kupanda mzabibu. # kuta zake kuta za mawe, sio za mbao # nguruwe wa msituni nguruwe pori wanaharibu bustani na mashamba na kuvamia watu. # msitu ardhi ambapo kuna miti mingi # wanyama hawa ni wanyama pori wa aina yoyote # shambani ardhi ambapo kuna mimea mingi lakini hakuna miti