# Kauli Unganishi: Mwandishi anaendelea kuzungumza na mfalme. # Katika sehemu ya baba zako watakuwa watoto wako Hii inamaanisha wana wa mfalme watachukua nafasi yake kama mfalme, kama yeye alivyochukua nafasi ya mababu zake. # utafanya wakuu duniani kote Msemo "duniani kote" ni kukuza kwa neno kusisitiza kwamba atatawala juu ya mataifa mengi. "utafanya watawala juu ya mataifa mengi" # Nitalifanya jina lako likumbukwe katika vizazi vyote Hapa "atakayefanya" ni mwandishi. Neno "jina" linamaanisha tabia ya mfalme na sifa yake. "Nitawasababisha watu katika kila kizazi kujua kuhusu ukuu wako"