# Taarifa ya Jumla: Hapa mwandishi anaanza kueleza kile kinachoonekana kuwa sherehe ya arusi ya mfalme na bibi arusi wake. # manemane, mshubiri ,na mdalasini Hii ni mimea yenye harufu nzuri ambayo watu hutumia kutengeneza manukato. # majumba ya mapembe Mapembe ni meno meupe magumu ya nje ya mnyama. Msemo huu unaelezea jumba lenye kuta na samani ambazo watu wamepamba kwa mapembe. # vyombo vya nyuzi vimekupa furaha Maneno "vyombo vya nyuzi" yanamaanisha muziki ambao watu hutengeneza kwa kucheza vyombo vya nyuzi. "muziki wa vyombo vya nyuzi umekufanya kuwa na furaha" # wanawake wenye heshima Hawa wanawake ni wake wa mfalme waliopokea kibali hiki. # malkia Hii inamaanisha mwanamke atakaye kuwa malkia. "bibi arusi wako, malkia" au "bibi arusi wako, atakaye kuwa malkia" # Ofiri Hili ni jina la sehemu iliyokuwa ikijulikana kwa dhahabu yake safi. " Mahali hapajulikani.