# Kwa kuwa tumeyeyuka kwenye mavumbi; miili yetu inang'ang'ania nchini Misemo hii ya usambamba ina maana za kufanana. Mwandishi anaelezea watu wake kama wamelala ardhini katika mkao wa kushindwa na kudhalilishwa. # Kwa kuwa tumeyeyuka kwenye mavumbi Mwandishi anazungumzia kudhalilishwa kwao kana kwamba miili yao ni vitu, kama barafu, inayoyeyuka na kulowa kwenye mchanga. # miili yetu inang'ang'ania nchini Mwandishi anazungumzia kudhalilishwa kwao kana kwamba miili yao ilikuwa imekwama kwenye ardhi na hawakuweza kujinyanyua juu. # inuka Hii ni amri ya kusimama. Msemo huu unamaanisha kuanza kutenda kitu. "Tenda jambo"