# Taarifa ya Jumla: Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kihebrania. # Kwa mwanamuziki mkuu "Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu" # Zaburi ya wana wa Kora "Hii ni zaburi ambayo wana wa Kora waliandika." # Maschili Hii inaweza kuwa mtindo wa muziki. # Tumeskia kwa maskio yetu, Mungu Neno "maskio" linaongeza mkazo kwa kauli waliosikia na kuelewa vitu ambavyo mwandishi anataka kueleza. Mwandishi anaeleza kauli hii kwa Mungu. "Mungu, tumesikia vizuri" # katika siku zao, katika siku za kale Misemo yote hii miwili inatumia neno "siku" kumaanisha wakati ambao mababu wa watu wa Israeli walipokuwa hai. # Uliondoa mataifa "Ulilazimisha watu wa mataifa mengine kuondoka" # kwa mkono wako Hapa neno "mkono" linamaanisha nguvu ya Mungu. "kwa nguvu yako" # uliwapanda watu wetu Mwandishi anamzungumzia Mungu kusababisha Waisraeli kuishi katika nchi kana kwamba aliyokuwa akiwapanda katika udongo kama ambavyo angepanda mti. "uliwasababisha watu kuishi huko"