# mbingu zako, ambazo vidole vyako Vidole vya Mungu vinaashiria ni yeye. "mbingu ulizoumba" # binadamu ana umuhimu gani hadi umtambue, au mtu hadi umwangalie? Misemo hii inaelezwa kwa njia ya swali kuongeza msisitizo. "Ni ajabu kuwa unawawaza watu na kuwajali!" # binadamu ... mtu Misemo hii yote inamaanisha watu kwa ujumla. # umewavika taji la utukufu na heshima Utukufu na heshima zinazungumziwa kana kwamba ni mataji. Maneno "utukufu" na "heshima" yanakaribiana kwa maana. "umewapa utukufu na heshima" au "umewasababisha kuwa kama wafalme"