# Sentensi unganishi Kama Yesu alivyokuwa ametabiri, Petro anamkana Yesu mara tatu kabla ya jogoo hajawika. # chini ya uani "nje ya uani" # mmoja wa wasichana wa kuhani mkuu Mtumishi wa kike alimtumikia kuhani mkuu. "moja wa watumishi wa kike waliomtumikia kuhani mkuu" # alimkana Hii inamaanisha kudai kwamba kitu fulani si sahihi. Katika hali hii, Petor alikuwa akisema kwamba alichosema mtumishi wa kike kuhusu yeye hakikuwa sahihi. # Sijui wala sielewi kuhusu kile unachosema Ote,"kujua" na "kuelewa" zina maana ile ile hapa. Maana imerudiwa kuongeza msisitizo kwa kile alichokuwa akisema Petor. "Hakika sikuelewi unachoongelea"