# Acha fadhila ionyeshwe kwa mtu muovu, lakini hatajifunza haki Hii inaweza kuelezwa kwa hali ya kutenda. "Hata kama Yahwe ni mwema kwa watu waovu, bado hawajifunzi kufanya kile kilicho sahihi" # mtu muovu Hii ina maana watu waovu kwa ujumla. # katika nchi ya wenye haki Hapa "nchi" inawakilisha watu ambao wanaishi kule. "Katika nchi ambapo watu hufanya kile kilicho sahihi" # haoni ukuu wa enzi wa Yahwe Hapa "kuona" inawakilisha kutambua kitu. "hatambui ya kwamba Yahwe ni mkuu"