# Sentensi uanganishi: Paulo tena anazungumzia jinsi wazee (maaskofu) wanapaswa kutunzwa na kisha kumpa Timotheo maelezo binafsi. # watambue wazee wanaoongoza vyema "Ninyi waumini wote mnapaswa kufikiri kama mnastahili" # Heshima mara mbili Maana inawezekana ni 1) "ya heshima na malipo" au 2) "heshima zaidi kuliko wengine wapokeavyo" # wale wanaofanya kazi na neno na katika kufundisha "wale wanaohubiri na kufundisha neno la Mungu" # kufunga kifaa kianachowekwa kwenye pua na mdomo wa mnyama ili kumzuia kula wakati anafanya kazi. # kupura nafaka Hii ni njia ya kutenganisha nafaka na makapi kwa kutumia mkokoteni unaovutwa na ng'ombe # anastahili "inastahili"