# kwanza mitume Hii inaweza kumaanisha 1) " ninataja karama ya kwanza kuwa ni ya mitume" au 2) "karama ya muhimu zaidi ni ya mitume" # wale wasaidiao " wale wanaotoa msaada kwa waumini wenzao" # wale wafanyao kazi ya kuongoza " wale wanaosimamia kanisa" # wote walio na aina mbalimbali za lugha Watu wanaozungumza lugha za kigeni moja au zaidi bila kujifunza. # Je sisi wote ni mitume? wote ni manabii? wote ni waalimu? wote wanafanya matendo ya miujiza? Paulo anawakumbusha wasomaji wake jambo wanalolijua. kwa maneno mengine anasema " baadhi yao tu ni mitume. Baadhi yao tu ni manabii. Baadhi yao tu hufanya matendo ya miujiza"