# Maelezo ya Jumla Mungu anaendelea kuzungumza ujumbe Nathani anao paswa kumpa Daudi. # nitawapanda hapo Mungu ana taja kuwaweka Waisraeli kwenye nchi ya ahadi kama mmea aliyo uotesha kwenye ardhi. "Nitawapandikisha hapo" # siku zile nilipo waamuru Kipindi cha vizazi vingi kina tajwa kama siku. "nilipo amuru" au kutoka vizazi nilivyo amuru" # kuwa juu ya watu wangu Waisraeli Kuwa katika mamlaka yaelezwa kama kua juu ya mtu. "kuwaamuru watu wangu Israeli" # maadui zako wote ... nina kwambia Maneno "zako" na "nina kwambia" ya muhusu Daudi. # nitawatiisha kumfanya mtu au mnyama asiweze kutembea. # nitakujengea nyumba Yahweh anaeleza kumpa Daudi wazao wengi kutawala juu ya Israeli kama kumjenga nyumba.