forked from WA-Catalog/sw_tn
33 lines
1.0 KiB
Markdown
33 lines
1.0 KiB
Markdown
|
# wanaliandaa wavu wao kwa ajili yangu
|
||
|
|
||
|
Njama za waovu zinazungumziwa kana kwamba ni wavu walioweka kumnasa mwandishi.
|
||
|
|
||
|
# walichimba shimo kwa ajili ya maisha yangu
|
||
|
|
||
|
Njama za waovu zinazungumziwa kana kwamba ni shimo walilochimba kumkamata mwandishi. "walitaka kunishika katika shimo kama mnyama mkubwa"
|
||
|
|
||
|
# maisha yangu
|
||
|
|
||
|
Hii inamaanisha mwandishi. "mimi"
|
||
|
|
||
|
# Acha maangamizi yawapite kwa kushtukiza
|
||
|
|
||
|
Maangamizi yanazungumziwa kana kwamba ni mnyama hatari ambaye atawavamia ghafla. "Acha waangamizwe ghafla" au "Acha washtukizwe kwa sababu umewaangamiza ghafla"
|
||
|
|
||
|
# wavu waliouandaa
|
||
|
|
||
|
Njama za waovu zinazungumziwa kana kwamba zilikuwa ni wavu walioweka kumnasa mwandishi. "wavu walioweka ili kuninasa kama mnyama na kunidhuru"
|
||
|
|
||
|
# Acha waanguke humo
|
||
|
|
||
|
Hii ni sitiari kama mstari wa 7. Wavu umekusudiwa kumnasa mwandishi. "Acha waanguke katika shimo walilo nichimbia"
|
||
|
|
||
|
# waanguke humo
|
||
|
|
||
|
Maana zinazowezekana ni 1) kuanguka katika shimo la mstari wa 7 au 2) kuanguka katika uharibifu.
|
||
|
|
||
|
# maangamizi yao
|
||
|
|
||
|
"ili waangamizwe" au "hivyo ndivyo unavyopaswa kuwaangamiza"
|
||
|
|