forked from WA-Catalog/sw_tn
29 lines
798 B
Markdown
29 lines
798 B
Markdown
|
# Taarifa ya Jumla:
|
||
|
|
||
|
Asafu anazungumza kwa niaba ya Israeli. Anaanza katika mstari wa 8 kuzungumzia jinsi Mungu alivyowaweka Israeli katika nchi yao kana kwamba Mungu alikuwa ni mtu anayesafisha ardhi ili kupanda mzabibu.
|
||
|
|
||
|
# Geuka
|
||
|
|
||
|
"Geuka kwetu" au "Njoo utusaidie tena"
|
||
|
|
||
|
# na ugundue
|
||
|
|
||
|
"na uangalie"
|
||
|
|
||
|
# mzabibu huu
|
||
|
|
||
|
Mwandishi anaendelea kufananisha taifa la Israeli na mzabibu.
|
||
|
|
||
|
# Huu ni mzizi ambao mono wako wa kuume ulipanda
|
||
|
|
||
|
Mkono wa kuume unawakilisha uwezo na nguvu ya Yahwe. "Huu ndio mzizi ambao wewe, Yahwe, ulipanda"
|
||
|
|
||
|
# kichipukizi
|
||
|
|
||
|
sehemu za mimea ambazo zinaanza kutokeza kutoka ardhini
|
||
|
|
||
|
# chini; wanaangamia kwa sababu ya lawama yako
|
||
|
|
||
|
Maana zinazowezekana ni 1) chini; watu wako wanaangamia kwa sababu ya lawama yako." au 2) "chini. Na adui zako waangamie kwa sababu ya lawama yako!"
|
||
|
|