sw_tn_fork/mat/11/01.md

45 lines
1.5 KiB
Markdown
Raw Normal View History

2018-04-12 01:01:04 +00:00
# Maelezo kwa ujumla
Huu ni mwanzo wa sehemu mpya wa simulizi amabapo mwandishi anaonesha jinsi ambavyo Yesu aliwaijibu wanafunzi wa Yohana Mbatizaji.
# Ikawa baada ya
Hiki kirai kinaibadilisha kutoka habari ya mafundisho ya Yesu kwenda kile kilichotokea baadaye. "Kisha" au "baadaye"
# Kuwaelekeza
"kufundisha" au "kuamurisha".
# wanafunzi wake kumi na mbili.
Hii inawahusu wale mitume kumi na wawili waliochaguliwa na Yesu.
# katika miji yao
Kimilikishi "yao" kinamaanisha Wayahudi wote kwa ujumla
# Sasa
Neno hili limetumika hapa kuonesha mwanzo katika habari kuu. Mathayo anaanza kusimulia habari mpaya
# Na Yohana akiwa gerezani aliposikia juu ya
"Wakati Yohana, akiwa gerezani aliposikia juu ya" au "Yohana alipoambiwa na mtu, wakati akiwa gerezani kuhusu, "Ingawa Mathayo hajawaambia wasomaji kwamba mfalme Herode alikuwa amemfunga gerezani Yohana mbatizaji, wasomaji wa kwanza wangekuwa wanaielewa habari na maana yake. Mathayo atatoa habari za Yohana mbatizaji baadaye, kwa hiyo yawezekana si vizuri kufafanua zaidi hapa.
# alituma ujumbe kupitia wanafunzi wake.
Yohana Mbatizaji aliwatuma wanafunzi wake ujumbe kumpelekea Yesu.
# na wakamuuliza
kiwakilishi "mu'' kinamrejea Yesu.
# Wewe ni yule ajaye
"Wewe ndiye yule amabye tunamtarajia kuja." Hii ni namna nyingine ya kumaanisha Masihi au Kristo.
# au kuna mwiingine tunayepaswa kumtazamia
''Tunapaswa kumtazamia mwingine." kiwakilishi "tu" kinarejerea ,wayahudi wote, siyo wanafunzi wa Yohana pekee.