Paulo amepanga sehemu ya sura hii kama sala ya sifa kwa Mungu. Lakini Paulo hazungumzi na Mungu pekee. Anafundisha kanisa huko Efeso. Pia anawaambia Waefeso jinsi anavyowaombea.
Wasomi wengi wanaamini kwamba sura hii inafundisha juu ya somo inayojulikana kama "kujaaliwa." Hii inahusiana na dhana ya Biblia ya "kujaaliwa." Wasomi wengine huchukua hii kuonyesha kwamba Mungu amechagua, tangu kabla ya msingi wa dunia, baadhi ya watu ili kuwaokoa milele. Wakristo wana maoni tofauti juu ya kile Biblia inafundisha juu ya suala hili. Kwa hivyo watafsiri wanahitaji kuwa makini zaidi wakati wa kutafsiri sura hii, hasa kuhusiana na mambo ya usababisho. (See: rc://en/tw/dict/bible/kt/predestine)