sw_tn_fork/act/13/06.md

53 lines
1.4 KiB
Markdown
Raw Normal View History

2018-04-12 01:01:04 +00:00
# Maelezo ya jumla
Mistari hii imetaja viwakilishi vingi vya majina kuelezea watu mbalimbali walio tajwa na mwandishi Luka.
# katika kisiwa chote
Walitembelea kisiwa chote kutoka upande mmoja hadi upande mwingine wakiunena ujumbe wa Injili katika kila mji walimopita.
# Pafo
Ni mji Mkuu wa kisiwa cha Kapro mahali Liwali alikuwa akiishi.
# Walimkuta
Neno "Kumkuta" linamaanisha kuwa walimfikia bila ya kumtafuta.
# Mtu fulani mchawi
"Mtu aliyekuwa akifanya kazu ya uchawi" au "Mtu aliyekuwa akifanya mambo yasiyo ya kawaida katika fani ya kimazingaombwe"
# ambaye jina lake lilikuwa Bar Yesu
"Bar - Yesu" maana yake "Mwana wa Yesu". Hakukuwa na mahusiano yoyote ya karibu na Yesu Kristo". Jina Yesu lilikuwa ni jina la kawaida katkia wakati ule.
# Mchawi huyu alishirikiana
"Alikuwa mara kwa mara pamoja na" au "Alikuwa mara kwa mara akiambatana na"
# Liwali
Huyu alikuwa Kiongozi mtendaji Katika utawala mkoa wa dola ya Rumi.
# aliyekuwa mtu mwenye akili
Hii ni historia ya maisha ya Liwali Sergio Paulus.
# Lakini Elima "yule mchawi"
Huyu alikuwa Bar- Yesu, ambaly aliyekuwa akiitwa mchawi.
# hivyo ndivyo jina lake lilivyo tafsiriwa
"Hivyo ndivyo jina lake katika lugha ya kigriki"
# aliwapinga; alijaribu kumgeuza
"Aliwazuia akijaribu kumgeuza"
# alijaribu kumgeuza yule liwali atoke kwenye imani
"Alijaribu kumshawishi Liwali kuiacha imani ya ujumbe wa Injli"