# Sitaki ninyi msijue "Natamani sana mtambue" # Mimi Neno "mimi" linamaanisha paulo. # wewe...wewe... ninyi Maneno haya "wewe" na "ninyi" yanamaanisha Mataifa walioamini. # ili kwamba msiwe na hekima katika kufikiri kwenu wenyewe. Waamini wa mataifa wanaweza kuamini kwamba wana hekima zaidi kuliko Wayahudi wasioamini. "Ili msifikiri kwamba mna hekima zaidi ya mlivyo" # ubaguzi mgumu umetokea katika Israeli Baadhi ya Wayahudi walikataa kukubali wokovu kupitia kwa Yesu. # hadi kukamilika kwa mataifa kutakapokuja Neno "mpaka" linaelezea kuwa Wayahudi wengi wataamini baada ya Mungu kumaliza kuwaleta Mataifa kanisani.