# sisi ni zaidi ya washindi "tunao ushindi kamili" # katika yeye aliyetupenda Aina ya upendo ambao Yesu alituonesha unaweza kuwekwa wazi. "kwasababu ya Yesu, aliyetupenda sana alikuwa tayari kufa kwa ajili yetu." # Mimi nimekwisha shawishika "Nimeshawishiwa" au "Nina ujasiri" # mamlaka Maana inaweza kuwa 1) mapepo (UDB) au 2) wafalme na watawala wa kibinadamu. # wala nguvu Maana inaweza kuwa 1) viumbe vya kiroho vyenye nguvu au 2) wanadamu wenye nguvu.