# kila mzaliwa wa kwanza afunguaye tumbo, mzaliwa wa kwanza. Virai hivi viwili vinamaanisha jamabo lilelile ili kutoa msisitizo wa mzaliwa wa kwanza. # mtoto wa kiume afunguaye tumbo "mtoto wa kiume ambaye ni mzaliwa wa kwanza kwa mama" # nilipowachukua Hii ni tafsida inayotumika kuonyesha kitendo cha mtu anapomwua mtu. "Nilipomwua" # Niliwatenga Kiwakilishi "wa" kinawawakilisha wazaliwa wa kwanza wa Israeli."