sw_ulb/36-ZEP.usfm

144 lines
8.7 KiB
Plaintext
Raw Blame History

This file contains ambiguous Unicode characters

This file contains Unicode characters that might be confused with other characters. If you think that this is intentional, you can safely ignore this warning. Use the Escape button to reveal them.

\id ZEP
\ide UTF-8
\h Sefania
\toc1 Sefania
\toc2 Sefania
\toc3 zep
\mt Sefania
\s5
\c 1
\cl Sura 1
\p
\v 1 Hili ni neno la Yahwe ambalo lilikuja kwa Sefania mwana wa Kushi mwana wa Gedalia mwana wa Amaria mwana wa Hezekia, katika siku za Yosia mwana wa Amoni, mfalme wa Yuda.”
\q1
\v 2 Nitaangamiza kabisa kila kitu kutoka usoni mwa dunia - hili ni tamko la Bwana mwenyewe.
\q1
\v 3 Nitamwangamiza mtu na mnyama; Nitawaangamiza ndege wa mbinguni na samaki wa baharini, uharibifu pamoja na waovu. Hivyo nitamfutilia mbali mtu kutoka uso wa dunia - hili ni tamko la Bwana mwenyewe.
\s5
\q1
\v 4 Nitafika kwa mkono wangu juu ya Yuda na wote wenyeji wa Yerusalemu. Nitafutilia mbali kila mabaki ya Baali kutoka sehemu hii na majina ya watu waabuduo sanamu miongoni mwa makuhani,
\q1
\v 5 watu ambao juu ya nyumba huabudu miili ya mbinguni, na watu ambao huabudu na kuapa kwa Yahwe bali ambao pia huapa kwa mfalme wao.
\q1
\v 6 Nitawafutilia mbali pia wale ambao wamegeuka nyuma kutoka kumfuata Yahwe, wale ambao pia humtafuta Yahwe pasipo kuuliza ulinzi wake.
\s5
\q1
\v 7 Uwe kimya mbele ya Bwana Yahwe! Kwa kuwa siku ya Yahwe ni karibu, Yahwe ameandaa dhabihu na amewatenga wageni wake.
\q1
\v 8 “Itakuja katika siku ya dhabihu ya Bwana, hivyo nitawapiga wakuu na wana wa mfalme, na kila mmoja aliyevikwa mavazi ya kigeni.
\q1
\v 9 Katika siku hiyo nitawapiga wote wale ambao huruka juu ya kizingiti, wale ambao hujaza nyumba ya bwana wao kwa vurugu na udanganyifu.
\s5
\q1
\v 10 Itakuwa katika siku ile - hili ni tangazo la Yahwe - kwamba kilio cha huzuni kitakuja kutoka kwenye mlango wa samaki, ikipiga yowe kutoka Wilaya ya Pili, na sauti ya kishindo kikuu kutoka vilimani.
\q1
\v 11 Pigeni yowe, wenyeji wa Soko la Wilaya, kwa wote wafanyabiashara watakuwa wameharibiwa, wote wale ambao hupima fedha watakuwa wamefutiliwa mbali.
\s5
\q1
\v 12 Itakuwa katika siku ile nitaitafuta Yerusalemu kwa taa na kuwapiga wanaume ambao watakuwa wamekaa kwenye mvinyo wao na kusema mioyoni mwao, Yahwe hatafanya chochote, ama kizuri au kiovu.
\q1
\v 13 Mali zao zitakuja kuporwa, na nyumba zao zitakuwa zimetelekezwa kwa maangamizi! Watajenga nyumba lakini hawataishi humo, na kupanda mizabibu lakini hawatakunywa mvinyo wake.
\s5
\q1
\v 14 Siku kubwa ya Yahwe i karibu, karibu na inaharakisha upesi! Sauti ya siku ya Yahwe itakuwa ya kilio cha uchungu wa kishujaa!
\q1
\v 15 Siku hiyo itakuwa siku ya ghadhabu, siku ya huzuni na uchungu, siku ya dhoruba na maangamizi, siku ya giza na utusitusi, siku ya mawingu na giza nene.
\q1
\v 16 Itakuwa siku ya parapanda na kengele dhidi ya ngome mijini.
\s5
\q1
\v 17 Hivyo nitaleta dhiki juu ya wanadamu, kwa hiyo watatembea karibu kama wanaume vipofu tangu walipofanya dhambi dhidi ya Yahwe. Damu yao itamwagwa kama vumbi, na sehemu zao za ndani kama kinyesi.
\q1
\v 18 Wala fedha zao wala dhahabu zao hazitaweza kuwaokoa juu ya ghadhabu ya Yahwe. Ndani ya moto wa wivu wake dunia yote itateketezwa, hivyo ataleta ukamilifu, mwisho wa kutisha kwa wote wakaao duniani.”
\s5
\c 2
\cl Sura 2
\p
\v 1 Kusanyikeni pamoja ninyi wenyewe mkutano wa hadhara na kusanyikeni, taifa lisilokuwa na aibu -
\q1
\v 2 kabla amri kuchukua madhara na siku hiyo kupita kama makapi, kabla hasira kali ya ghadhabu ya Yahwe kuja juu yenu, kabla siku ya ghadhabu ya Bwana kuja juu yenu.
\q1
\v 3 Mtafuteni Yahwe, ninyi watu wote wanyenyekevu duniani mnaozitii amri zake! Tafuteni haki yake. Tafuteni unyenyekevu, na labda mtalindwa katika siku ya ghadhabu ya Yahwe.
\s5
\q1
\v 4 Hivyo Gaza utatelekezwa, na Ashkeloni utageuka kuwa uharibifu. Watauondoshea mbali Ashdodi wakati wa mchana, na wataung'oa Ekroni!
\q1
\v 5 Ole kwa wanaokaa kando ya bahari, taifa la Wakerethi! Yahwe amesema dhidi yenu, Kanaani, nchi ya Wafilisiti. Nitawaangamiza hakuna mkazi atakayebakia.
\s5
\q1
\v 6 Hiyo nchi ya kando ya bahari itakuwa malisho kwa wachungaji na kwa mazizi ya kondoo.
\q1
\v 7 Nchi ya kando ya bahari itakuwa mali ya mabaki ya watu wa nyumba ya Yuda, watakaochungia makundi yao huko. Watu wao watalala jioni katika nyumba ya Ashikeloni, kwa kuwa Yahwe Mungu wao atawatunza na kurejesha wafungwa wao.
\s5
\p
\v 8 Nilizisikia dhihaka za Moabu na wakiwatukana watu wa Amoni wakati walipowadhihaki watu wangu na kujitukuza mipakani mwao.
\q1
\v 9 Kwa hiyo, kama ninavyoishi - hili ni tamko la Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israeli, -Moabu itakuja kuwa kama Sodoma, na watu wa Amoni kama Gomora; mahali pachafu na shimo la chumvi, jangwa la daima. Lakini watu wangu waliosalia watawateka mateka, na watu wa taifa langu waliobaki watachukua umiliki wao.
\s5
\q1
\v 10 Hili litatokea kwa Moabu na Amoni kwa sababu ya kiburi chao, tangu walipowadhihaki na kuwatukana watu wa Yahwe wa majeshi.
\q1
\v 11 Ndipo watamwogopa Yahwe, kwa kuwa ataidhihaki miungu yote ya dunia. Kila mmoja atamwabudu yeye, kila mmoja kutoka mahali pake, kutoka kila upande wa pwani.
\s5
\q1
\v 12 Ninyi Wakushi pia mtakufa kwa upanga wangu,
\q1
\v 13 na mkono wa Mungu utaishambulia kaskazini na kuiangamiza Ashuru, Kwa hiyo Ninawi utatelekezwa kwa kuteketezwa, kuwa pakavu kama jangwa.
\q1
\v 14 Ndipo makundi ya wanyama yatalala pale, kila mnyama wa mataifa, wote kirukanjia na nungunungu watapumzika juu ya safu zao. Sauti itasikika kutoka madirishani; kifusi kitakuwa milangoni; nakshi za mwerezi wao mihimili itakuwa imeifunua.
\s5
\q1
\v 15 Huu ni mji wa kushangiliwa ambao umekaa pasipo hofu, ambaye husema moyoni mwake, “Mimi niko, na hakuna mwingine wa kufanana na Mimi.” Kwa namna ulivyokuwa wa kutisha, mahali pa kulala wanyama ndani yake. Kila mmoja ambaye hupitia kwake huuhisia na kutingisha mikono yake.
\s5
\c 3
\cl Sura 3
\p
\v 1 Ole kwa mji ulioasi! Mji wenye vurugu umenajisiwa.
\q1
\v 2 Haukuisikiliza sauti ya Mungu, wala haukupokea masahihisho kutoka kwa Yahwe. Hakumtumaini Yahwe na hatamkaribia Mungu wake.
\s5
\q1
\v 3 Wafalme wao ni simba wanaounguruma miongoni mwao. Waamuzi wao ni mbwa mwitu wa jioni wasiobakiza kitu ambacho kitakuwa kimemung'unywa asubuhi yake.
\q1
\v 4 Manabii wake wanakiburi na wanaume wasaliti. Makuhani wake wamepanajisi mahali patakatifu na wameifanyia vurugu sheria.
\s5
\q1
\v 5 Yahwe ni mwenye haki miongoni mwao. Hawezi kufanya makosa. Kila asubuhi husimamia haki yake! Haitafichika nuruni, hata hivyo watu wasio wenye haki hawajui kuona aibu.
\s5
\p
\v 6 Nimeyaharibu mataifa; ngome zao zimeharibiwa. Nimeifanya mitaa yao magofu, hivyo hakuna hata mmoja anayepitia kwake. Miji yao imeharibiwa kwa hiyo hakuna mtu anayeikaa.
\q1
\v 7 Nikasema, Hakika mtaniogopa mimi. Pokeeni masahihisho na msikatiliwe mbali kutoka kwenye miji yenu kwa yote yale niliyokuwa nimeyapanga kuyafanya kwenu. Lakini walikuwa na shauku kuanza kila siku kwa kuharibu matendo yao yote.
\s5
\q1
\v 8 Kwa hiyo ningojeni - hili ni tamko la Yahwe - mpaka siku ambayo nitainuka kwa ajili ya waathirika. Uaamuzi wangu nikuwakusanya mataifa, kuzikusanya falme, na kumwaga juu yao hasira yangu, uchungu wangu wote mkali, hivyo nchi yote itamezwa kwa moto wa hasira yangu.
\s5
\q1
\v 9 Ndipo nitawapa midomo safi watu, kuwaita wote kwa jina la Bwana kunitumikia wakisimama bega kwa bega.
\q1
\v 10 Kutoka ng'ambo ya mto Ethiopia waniabuduo - watu wangu waliotawanyika - wataleta dhabihu kwa sababu yangu.
\q1
\v 11 Katika siku hiyo hamtawekwa kwenye woga kwa matendo yenu yote ambayo mmeyafanya dhidi yangu, tangu wakati ule nitaondoa kutoka kwenu wale waliosherehekea fahari yenu, na kwa sababu hamtakuwa na muda mrefu kufanya majivuno juu ya mlima wangu mtakatifu.
\s5
\q1
\v 12 Lakini nitawaacha kama wa chini zaidi na watu masikini, na mtapata kimbilio katika jina la Yahwe.
\q1
\v 13 Mkazi wa Israeli si muda mrefu hatafanya udhalimu au kusema uongo, na hakuna ulimi wa udanganyifu utakaoonekana mdomoni mwao; hivyo watalisha na kulala chini, na hakuna hata mmoja atakayewafanya kuogopa.”
\s5
\q1
\v 14 Imba, binti Sayuni! Piga kelele, Israeli. Ufurahi na kushangilia kwa moyo wako wote, binti wa Yerusalemu.
\q1
\v 15 Yahwe ameiondoa hukumu yako; amewafukuzia mbali adui zako! Yahwe ni mfalme wa Israeli miongoni mwenu. Kamwe hamtamwogopa tena mwovu!
\q1
\v 16 Katika siku hizo watasema kwa Yerusalemu, “Usiogope, Sayuni. Usiiache mikono yako ilegee.
\s5
\q1
\v 17 Yahwe Mungu wako yuko katikati yenu, mwenye nguvu wa kuwaokoa. Atasherehekea juu yenu na kwa furaha atakuwa kimya juu yenu kwa upendo wake. Atakuwa na furaha juu yenu na atashangilia kwa furaha,
\q1
\v 18 katika siku maalumu ya sherehe. Nitaondoa maafa kutoka kwenu; si muda mrefu hamtabeba aibu kwa ajili yake.
\s5
\q1
\v 19 Tazama, niko tayari kuwashughulikia watesi wenu wote. Katika wakati ule, nitawaokoa waliolemaa na kuwakusanya waliotupiliwa mbali. Nitawafanya kuwa sifa, na nitaibadilisha aibu yao iwe sifa katika dunia yote.
\q1
\v 20 Katika wakati ule nitawaongoza; katika wakati ule nitawakusanya pamoja. Nitawafanya mataifa yote ya dunia kuwaheshimu na kuwasifu, wakati mtakapoona hivyo, nitakuwa nimewarudisha,” asema Yahwe.