sw_ulb/12-2KI.usfm

1421 lines
126 KiB
Plaintext
Raw Blame History

This file contains ambiguous Unicode characters

This file contains Unicode characters that might be confused with other characters. If you think that this is intentional, you can safely ignore this warning. Use the Escape button to reveal them.

\id 2KI
\ide UTF-8
\h 2 Wafalme
\toc1 2 Wafalme
\toc2 2 Wafalme
\toc3 2ki
\mt 2 Wafalme
\s5
\c 1
\cl Sura 1
\p
\v 1 Moabu aliasi dhidi ya Israeli baada ya kifo cha Ahabu.
\v 2 Baada hapo Ahazia akaanguka chini ya dirisha zinazokinzana kwenye chumba chake juu katika Samaria, na alikuwa amejeruhiwa. Kwa hiyo alituma wajumbe na kuwaambia, “Nendeni, muulizeni Baal Zebubu, mungu wa Ekroni, kama nitapona hili jeraha.”
\s5
\p
\v 3 Lakini malaika wa Yahwe wakamwambia Eliya Mtishbi, “Inuka, nenda ukaonane na wajumbe wa mfalme wa Samaria, na uwaulize, Je ni kwa sababu hakuna Mungu katika Israel hata mnakwenda kuuliza kwa Baal-Zebebu, mungu wa Ekroni?
\v 4 Kwa hiyo Yahwe anasema, Hutaweza kushuka chini kutoka kwenye kitanda ambacho ulichokipanda; badala yake, utakufa hakika.’” Baada ya hapo Eliya akaondoka.
\s5
\p
\v 5 Wakati wale wajumbe waliporudi kwa Ahazia, akawaambia, “Kwa nini mmerudi?”
\p
\v 6 Wakamwambia, “Mtu amekuja kuonana na sisi ambaye ametuambia, Rudini kwa mfalme ambaye aliyewatuma, na mkamwambie, Yahwe amesema hivi: Je ni kwa sababu hakuna Mungu katika Israeli mpaka mmewatuma watu kwenda kumuuliza kwa Baal Zabubu, mungu wa Ekron? Kwa hiyo hutashuka kutoka kitanda ulichokipanda; badala yake, utakufa hakika.’”
\s5
\p
\v 7 Ahazia akawaambia wajumbe wake, “Alikuwa mtu wa aina gani, yule ambaye alikuja kuonana nanyi na akasema haya maneno kwenu?”
\p
\v 8 Wakamjibu, “Alikuwa amevaa kanzu yenye manyoya na alikuwa na mkanda wa ngozi kiunoni kwake.” Hivyo mfalme akajibu, “Yule alikuwa Eliya Mtishbi.”
\s5
\p
\v 9 Ndipo mfalme akatuma mkuu wa askari hamsini kwa Eliya. Akaenda mpaka kwa Eliya ambapo alipokuwa amekaa juu ya mlima. Mkuu wa askari akamwambia Eliya, “Wewe, mtu wa Mungu, mfalme amesema, Shuka chini.’”
\p
\v 10 Eliya akajibu na kusema; “Kama mimi ni mtu wa Mungu, moto na ushuke chini kutoka mbinguni na ukuteketeze wewe na watu wako hamsini.” Kisha moto ukashuka chini kutoka mbinguni na kumla yeye na watu wake hamsini.
\s5
\p
\v 11 Tena Mfalme Ahazia akamtuma mkuu mwingine pamoja na maaskari wengine hamsini. Huyu mkuu pia akasema kwa Eliya, “Wewe, mtu wa Mungu, mfalme anasema, Teremka chini haraka.’”
\p
\v 12 Eliya akajibu na kuwaambia, “Kama mimi ni mtu wa Mungu, ngoja moto ushuke kutoka mbinguni na ukuteketeze wewe na watu wako hamsini.” Moto wa Mungu ukashuka chini tena kutoka mbinguni na kumla yeye na watu wake hamsini.
\s5
\p
\v 13 Bado tena mfalme alituma kundi la tatu la wapiganaji hamsini. Huyu mkuu akaenda, akaanguka mbele ya miguu ya Eliya, na kumsihi na kumwambia, “Wewe, mtu wa Mungu, nakuomba, acha uzima wangu na uzima wa hawa watumishi wako hamsini uwe na thamani machoni kwako.
\v 14 Ndipo, moto ukashuka chini kutoka mbinguni na kuwala wale wakuu wawili wa kwanza pamoja na watu wao, bali sasa acha uzima wangu uwe na thamani machoni kwako.”
\s5
\p
\v 15 Malaika wa Yahwe akamwambia Eliya, “Nenda chini pamoja naye. Usimwogope.” Hivyo Eliya akainuka na kwenda chini pamoja naye kwenda kwa mfalme.
\p
\v 16 Baadaye Eliya akamwambia Ahazia, “Hivi ndivyo Yahwe asemavyo, Umewatuma wajumbe kuzungumza pamoja na Baal-Zebubu, mungu wa Ekron. Je ni kwa sababu hakuna Mungu katika Israeli ambaye unayeweza kumuuliza habari? Kwa hiyo sasa, hutaweza kushuka chini kutoka kwenye kitanda ulichokipanda; utakufa hakika.’”
\s5
\v 17 Hivyo Mfalme Ahazia alikufa kulingana na neno la Yahwe ambalo Eliya alilisema. Yoramu alianza kutawala katika eneo lake, katika mwaka wa pili Yoramu mwana wa Yohoshafati mfalme wa Yuda, kwa sababu Ahazia hakuwa na mtoto.
\p
\v 18 Na mambo mengine yanayomhusu Ahazia, je hayakuandikwa katika kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli?
\s5
\c 2
\cl Sura 2
\p
\v 1 Ulipofika, wakati BWANA alipopenda kumpandisha Eliya kwenda mbinguni kwa upepo wa kisulisuli, Eliya aliondoka pamoja na Elisha kutoka Gilgali.
\v 2 Eliya akamwambia Elisha, “Kaa hapa, tafadhali, kwa sababu BWANA amenituma niende mpaka Betheli.” Elisha akajibu, “Kama BWANA aishivyo, na kama uishivyo, sitakuacha.” Hivyo wakashuka chini kuelekea Betheli.
\s5
\v 3 Wana wa manabii ambao walikuwa Betheli walikuja kwa Elisha na kumwambia, “Je unajua kwamba BWANA atamwondoa bwana wako kuanzia leo?” Elisha akajibu, “Ndiyo, nalijua hilo, ila msizungumze kuhusu hilo.”
\v 4 Eliya akamwambia, “Elisha, subiri hapa, tafadhali, kwa kuwa BWANA amenituma niende Yeriko.” Kisha Elisha akajibu, “Kama BWANA aishivyo, na kama uishivyo, sitakuacha.” Hivyo wakaenda Yeriko.
\s5
\p
\v 5 Kisha wana wa manabii ambao walikuwa Yeriko wakaja kwa Elisha na kumwambia, “Je unajua kwamba BWANA atamwondoa bwana wako kutoka kwako leo?” Elisha akajibu, “Ndiyo, nalijua hilo, lakini msilizungumzie hilo.”
\p
\v 6 Kisha Eliya akamwambia, “Kaa hapa, tafadhali, kwa kuwa BWANA amenituma kwenda Yeriko.” Elisha akajibu, “Kama BWANA aishivyo, na kama uishivyo, sitakuacha.” Hivyo wawili wakaenda mbele.
\s5
\v 7 Baadaye watu hamsini wa watoto wa wale manabii wakasimama kuwakabili kwa mbali kidogo wale wawili wakasimama karibu na Yordani.
\v 8 Eliya akachukua vazi lake, akaliviringisha, na kuyapiga maji kwa kutumia lile vazi. Ule mto ukagawanyika katika sehemu mbili hivyo basi wawili hao wakatembea hadi nchi kavu.
\s5
\p
\v 9 Ilitokea, walipokwisha kuvuka, kwamba Eliya akamwambia Elisha, “Niambie unachotaka nifanye kwako kabla sijaondolewa kutoka kwako.” Elisha akajibu, “Naomba sehemu kubwa ya roho yako ije kwangu.”
\p
\v 10 Eliya akajibu, “Umeomba jambo gumu. Hata hivyo, kama ukiniona wakati nitakapoondolewa kutoka kwako, hii itatokea kwako, lakini kama sivyo, haitatokea.”
\s5
\p
\v 11 Ikawa walipokuwa bado wakienda mbele na kuzungumza, gari la kukokotwa na farasi lenye moto na farasi wa moto ikatokea, ambapo iliwatenga kutoka kila mmoja, na Eliya akaenda juu kwa upepo wa kisulisuli kwenda mbinguni.
\v 12 Elisha akaiona akalia kwa sauti, “Baba yangu, baba yangu, gari la kukokotwa na farasi la Israeli na waendesha farasi!” Hakumwona Eliya tena, na akashikilia nguo zake mwenyewe na kugawanya kwenye vipande viwili.
\s5
\v 13 Akachukua vazi la Eliya lililokuwa limemwangukia, na kurudi kusimama kwenye ukingo wa Yordani.
\v 14 Akayapiga maji pamoja na lile vazi la Eliya alilokuwa ameliangusha na kusema, “BWANA uko wapi, Mungu wa Eliya?” Wakati alipoyapiga yale maji, yaligawanyika katika pande mbili na Elisha akavuka.
\s5
\p
\v 15 Wakati hao wana wa manabii ambao walitoka Yeriko walipomuona akikatiza kwao, wakasema, “Roho ya Eliya imepumzika kwa Elisha!” Hivyo wakaja kuonana naye, na wakasujudu ardhini mbele yake.
\v 16 Wakamwambia, “Ona sasa, miongoni mwa watumishi wako kuna watu hamsini hodari. Tunakuomba waache waende, na kumtafuta bwana wako, endapo huyo Roho wa BWANA alipomchukua juu na kumtupa juu ya mlima mmoja au kwenye bonde moja.” Elisha akajibu, “Hapana, msiwatume.”
\s5
\p
\v 17 Lakini walimsihi Elisha hadi akaona aibu, akasema, “Watume.” Ndipo wakawatuma watu hamsini, na wakatafuta kwa muda wa siku tatu, lakini hawakumpata.
\v 18 Wakarudi kwa Elisha, wakati alipokuwa bado yuko Yeriko, na akasema, “Je sikusema, msiende?’”
\s5
\p
\v 19 Watu wa mjini wakamwambia Elisha, “Ona, tunakuomba, hali ya mjini hapa ni pazuri, kama bwana wangu awezavyo kuona, lakini maji ni mabaya na hiyo nchi huzaa mapooza.”
\p
\v 20 Elisha akajibu, “Nileteeni chombo kipya na muweke chumvi ndani ya hicho chombo,” hivyo wakamletea.
\s5
\p
\v 21 Elisha akaenda hadi kwenye chemichemi za maji na kutupia chumvi ndani; halafu akasema, “BWANA asema hivi, Nimeyaponya haya maji. Kuanzia muda huu, hakutakuwa na kifo au nchi isiyozaa matunda.’”
\v 22 Hivyo hayo maji yakapona hata leo, kwa lile neno ambalo Elisha aliongea.
\s5
\p
\v 23 Ndipo Elisha akapanda kutoka pale mpaka Betheli. Naye lipokuwa akienda hadi kwenye barabara, wakatokea vijana nje ya mji na kumtania, wakamwambia, “Paa juu, wewe mwenye kipara! Paa juu, wewe mwenye kipara!”
\v 24 Elisha alipotazama nyuma yake na kuwaona; akawalaani kwa jina la BWANA, na dubu wa kike wawili wakatokea kichakani na kuwararua vijana arobaini na mbili.
\v 25 Ndipo Elisha alipoondoka pale na kuelekea Mlima Karmeli, na kutoka huko alirudi samaria.
\s5
\c 3
\cl Sura 3
\p
\v 1 Basi katika mwaka wa kumi na nane wa Yehoshefati mfalme wa Yuda, Yoramu mwana wa Ahabu alianza kutawala juu yata Israeli katika Samaria; alitawala miaka kumi na miwili.
\v 2 Alifanya yaliyo maovo machoni pa BWANA, lakini si kama baba yake na mama yake; kwa kuwa aliiondoa ile nguzo ya mungu wa Baali ambayo baba yake aliitengeneza.
\v 3 Hata hivyo alishikilia dhambi za Yeroboamu mwana wa Nebati, ambaye alisababisha Israeli kufanya dhambi; wala hakuziacha mbali nao.
\s5
\p
\v 4 Basi Mesha mfalme wa Moabu alifuga kondoo. Alikuwa akimpatia mfalme wa Israeli kondoo 100,000 na manyoya ya kondoo dume 100,000.
\v 5 Ila baada ya Ahabu kufa, yule mfalme wa Moabu aliasi dhidi ya mfalme wa Israeli.
\v 6 Hivyo Mfalme Yoramu akaondoka Samaria katika muda huo kuwahamasisha Waisraeli wote kwa ajili ya vita.
\s5
\v 7 Akatuma mjumbe kwa Yehoshafati mfalme wa Yuda, akisema, “Mfalme wa Moabu ameasi dhidi yangu. Je mtakwenda pamoja nami kupigana dhidi ya Moabu?” Yehoshafati akajibu, “Nitaenda. Mimi ni kama wewe, watu wangu ni kama watu wako, farasi wangu ni kama farasi wako.”
\p
\v 8 Ndipo akasema, “Tutawashambulia kwa njia gani?” Yehoshafati akajibu, “Kwa njia ya jangwa la Edemu.”
\s5
\p
\v 9 Hivyo huyo mfalme wa Israeli, Yuda, na Edomu wakazunguka kwa muda wa siku saba. Hapakuwa na maji kwa ajili ya jeshi lao, wala kwa farasi au wanyama.
\p
\v 10 Basi mfalme wa Israeli akasema, “Hii ni nini? Yahwe amewaita wafalme watatu ili kutekwa mikononi mwa Moabu?”
\s5
\p
\v 11 Lakini Yehoshafati akasema, “Je hakuna nabii wa BWANA, ambaye tunaweza kufanya shauri kuhusu BWANA kupitia yeye?” Mtumishi mmoja wa wafalme wa Israeli akajibu na kusema, “Elisha mwana wa Shafati yuko hapa, ambaye alikuwa akimimina maji kwenye mikono ya Eliya.”
\p
\v 12 Yehoshafati akasema, “Neno la Yahwe liko pamoja naye.” Hivyo mfalme wa Israeli, Yehoshafati, na mfalme wa Edomu wakashuka chini kwenda kwake.
\s5
\v 13 Elisha akamwambia mfalme wa Israeli, “Nifanye nini kwa ajili yako? Nenda kwa manabii wa baba na mama yako.” Ndipo mfalme wa Israeli akamwambia, “Hapana, kwa sababu BWANA amewaita hawa wafalme watatu pamoja ili kuruhusu jeshi la Moabu liwateke.”
\p
\v 14 Elisha akajibu, “Kama BWANA wa majeshi aishivyo, ambaye nimesimama mbele zake, hakika kama nisingemheshimu uwepo wa Yehoshafati mfalme wa Yuda, nisingevuta usikivu kwako, au hata kukutazama.
\s5
\v 15 Lakini sasa niletee mpiga kinanda.” Ndipo alipokuja mpiga kinanda alipocheza, mkono wa BWANA ukaja juu ya Elisha.
\v 16 Akasema, “BWANA asema hivi, Fanya hili bonde la mto mkavu lijae mahandaki.
\v 17 Kwa kuwa BWANA asema hivi, Hutaona upepo, wala hamtaona mvua, bali hili bonde la mto litajaa maji, na mtakunywa, ninyi na mifugo yenu na wanyama wenu wote.
\s5
\v 18 Jambo hili ni jepesi machoni pa BWANA. Pia atawapa ushindi juu ya hao Wamoabu.
\v 19 Mtaiteka kila ngome ya mji na kila mji mzuri, kukata kila mti mzuri, kusimamisha chemichemi zote za maji, na kuharibu kila sehemu nzuri ya nchi na miamba.”
\s5
\p
\v 20 Hivyo asubuhi karibia na muda wa kutoa sadaka ya kuteketeza, yakaja maji kutoka uelekeo wa Edomu; nchi ikajaa maji.
\s5
\p
\v 21 Ndipo wakati Wamoabu wote waliposikia kwamba wafalme wamekuja kupigana dhidi yao, walikusanyika pamoja, wote waliotakiwa kubeba silaha, na wakasimama mpakani.
\v 22 Walitembea asubuhi na mapema na jua likang'aa kwenye maji. Wakati Wamoabu walipoyaona yale maji yaliyowaelekea, yanaonekana mekundu kama damu.
\v 23 Wakatamka kwa hasira, “Hii ni damu! Yamkini hao wafalme wameharibiwa, na wameuana wao kwa wao! Sasa basi, Moabu, ngoja tuende tukawateke nyara!”
\s5
\p
\v 24 Wakati walipokuja kwenye kambi ya Israeli, Waisraeli wakawashtukiza na kuwashambulia Wamoabi, ambao walikimbia mbele yao. Hilo jeshi la Israeli waliwakimbiza hao Wamoabu hadi kwao wakiwaua.
\v 25 Waliiharibu miji, na kila aina ya amani ya nchi kila mtu alirusha jiwe mpaka ulipojaa. Walizuia kila chemichemi ya maji na kukata chini miti mizuri yote. Kir-haresethi tu ndiyo ilichwa na mawe yake. Lakini hao maaskari wakawashambulia na makombeo wakiwazunguka na kuishambulia.
\s5
\v 26 Ndipo Mfalme Mesha wa Moabu alipoona kwamba ameshindwa, alichukua watu hodari wa upanga 700 pamoja naye kwenda kwa mfalme wa Edomu, lakini walishindwa.
\v 27 Ndipo akamchukua mtoto wake wa kwanza, ambaye angetawala baada ya yeye, na akamuudhi kwa kumtoa kama sadaka ya kuteketezwa juu ya ukuta. Hivyo, kulikuwa na hasira kubwa dhidi ya Israeli, na hao Waisraeli, na Jeshi la Israeli likamuacha mfalme Mesha na kurudi kwenye nchi yao.
\s5
\c 4
\cl Sura 4
\p
\v 1 Ndipo mke wa mmoja wa watoto wa manabii alipokuja kwa Elisha akilia, akisema, “Mtumishi wako mume wangu amekufa, na unajua kwamba mtumishi wako alikuwa anamcha BWANA. Basi aliyemdai amekuja kuwachukua watoto wangu wawili kwenda kuwa watumwa.”
\p
\v 2 Hivyo Elisha akamwambia, “Nikusaidie nini? Niambie una nini kwenye nyumba yako?” Akamwambia “Mtumishi wako hana kitu kwenye nyumba, isipokuwa chupa ya mafuta.”
\s5
\p
\v 3 Kisha Elisha akasema, “Nenda kaazime vyombo kwa majirani zako, vyombo vitupu. Azima vyombo vingi uwezavyo.
\v 4 Kisha lazima uende ndani na kujifungia mlango wewe na watoto wako, na kumiminia mafuta vyombo vyote; vile vilivyojaa ukavitenge.”
\s5
\p
\v 5 Basi akamuacha Elisha na kujifungia mlango yeye na watoto wake. Wakavileta vile vyombo kwake, na akivijaza kwa mafuta.
\v 6 Ikawa vyombo vilipojaa, akamwambia mtoto wake, “Niletee chombo kingine.” Ila akamwambia, “Hakuna vyombo vingine.” Kisha mafuta yakakoma kutoka.
\s5
\p
\v 7 Ndipo akaja na kumwambia mtu wa Mungu. Akasema, “Nenda kauze mafuta; lipa deni lako, na yatakayobaki waachie watoto wako.”
\s5
\p
\v 8 Siku moja Elisha alitembea Shunemu ambapo mwanamke Mwenye cheo aliishi; alimsihi ale chakula pamoja naye. Ikawa alipopita mara nyingi, angeweza kusimama pale na kula.
\v 9 Huyo mwanamke akamwambia mme wake, “Ona, sasa nadhani kwamba huyu ni mtu mtakatifu wa Mungu ambaye hupita siku zote.
\s5
\v 10 Ngoja tutengeneze chumba kidogo kwenye paa kwa ajili ya Elisha, na tuweke kitanda juu ya hicho chumba, meza, na taa. Kisha atakapokuwa anakuja kwetu, atakuwa anakaa hapo.”
\p
\v 11 Ikawa siku moja akaja tena kwamba Elisha akasimama pale, akakaa kwenye hicho chumba na kupumzika hapo.
\s5
\v 12 Elisha akamwambia Gehazi mtumishi wake, “Mwite huyu Mshunami.” Wakati alipomuita, alisimama mbele yake.
\v 13 Elisha akamwambia, “Mwambie, Umetusumbukia kwa kutujali. Nini kifanyike kwa ajili yako? Tunaweza kukuombea kwa mfalme au kamanda wa jeshi?’” Akajibu, “Ninaishi miongoni mwa watu wangu.”
\s5
\p
\v 14 Kisha Elisha akajibu, “Tumfanyie nini kwa ajili yake, sasa?” Gehazi akajibu, “Kweli hana mtoto, na mume wake ni mzee.”
\p
\v 15 Hivyo Elisha akajibu, “Mwite.” Wakati alipomuita, akasimama kwenye mlango.
\v 16 Elisha akasema, “Katika kipindi kama hiki mwakani, katika kipindi cha mwaka mmoja, utakuwa ukimkumbatia mtoto.” Akasema “Hapana, bwana wangu na mtu wa Mungu, usidanganye kwa mtumishi wako.”
\s5
\p
\v 17 Lakini yule mwanamke akabeba mimba na kujifungua mtoto wa kiume kipindi hicho hicho katika mwaka uliofuata, kama Elisha alivyokuwa amemwambia.
\p
\v 18 Wakati mtoto alipokuwa mkubwa, akaenda kwa baba yake siku moja, ambaye alikuwa na watu wanaovuna.
\v 19 Akamwambia baba yake, “Kichwa changu, kichwa changu.” Baba yake akamwambia mtumishi wake, “Mbebe mpeleke kwa mama yake.”
\v 20 Wakati mtumishi alipombeba kumrudisha kwa mama yake, yule mtoto alikaa kwenye magoti yake hadi mchana na baada ya hapo mtoto alikufa.
\s5
\v 21 Hivyo yule mwanamke akambeba na kumlaza kwenye kile kitanda cha mtu wa Mungu, akafunga mlango, na kutoka nje.
\p
\v 22 Akamwita mume wake, na kusema, “Tafadhali nitumie mmoja wa watumishi wako na moja ya punda wako ili niweze kuwahi kwa mtu wa Mungu ili niweze kurudi.”
\s5
\p
\v 23 Mume wake akasema, “Kwa nini unataka kwenda kwake leo? Sio mwezi mpya wala Sabato.” Alijibu, “Itakuwa sawa.”
\p
\v 24 Ndipo akatandika kwenye punda na kumwambia mtumishi wake, “Mwendeshe haraka; usinipunguzie mwendo hadi nitakapokwambia ufanye hivyo.”
\s5
\v 25 Hivyo alienda na kuja na mtu wa Mungu katika mlima Karmeli. Basi wakati mtu wa Mungu alipomuona kwa mbali, akamwambia Gehazi mtumishi wake, “Tazama, mwanamke Mshunami anakuja.
\v 26 Tafadhali mkimbilie na umwambie, Hamjambo kwako pamoja na mume wako na mtoto wako?’” Akajibu, “Hawajambo.”
\s5
\p
\v 27 Baada ya kufika kwa huyo mtu wa Mungu katika mlima, alimkumbatia miguu yake. Gehazi akaja karibu ili kumuondoa lakini mtu wa Mungu akasema, “Muache, kwa kuwa amefadhaika sana. Na BWANA amenificha tatizo lake kwangu, na hajaniambia kitu.”
\s5
\p
\v 28 Ndipo akasema, “Nilikuuliza mtoto wako, bwana wangu? Sikusema, Usinifiche?’”
\p
\v 29 Ndipo Elisha akamwambia Gehazi, “Vaa kwa ajili ya safari na uchukue fimbo yangu mkononi mwako. Nenda kwake. Kama ukimkuta mtu yeyote, usimsalimie, na kama mtu yeyote akikusalimia, usimjibu. Laza fimbo yangu kwenye uso wa mtoto.
\s5
\p
\v 30 Lakini mama yake na huyo mtoto akasema, “Kama BWANA aishivyo, na kama uishivyo, sitakuacha.” Hivyo Elisha akainuka na kumfuata.
\p
\v 31 Gehazi akawatangulia na kulaza ile fimbo kwenye uso wa yule mtoto, lakini yule mtoto hakuongea wala kusikia. Hivyo baada ya hapo Gehazi akarudi kuonana na Elisha na kumwambia akisema, “Mtoto hakuamka.”
\s5
\v 32 Ndipo Elisha alipofika kwenye ile nyumba, yule mtoto alikuwa amekufa na alikuwa bado yupo kwenye kitanda.
\v 33 Hivyo Elisha aliingia ndani na kufunga mlango yeye mwenyewe na yule mtoto na kuomba kwa BWANA.
\v 34 Alipanda juu na kulala juu ya yule mtoto; aliweka mdomo wake kwenye mdomo wake, macho yake kwenye macho yake, na mikono yake kwenye mikono yake. Akajinyoosha yeye mwenyewe kwa yule kijana, na mwili wa yule mtoto ukaanza kupata joto.
\s5
\v 35 Baada ya hapo Elisha aliinuka na kuanza kutembea kuzunguka kile chumba na kurudi tena juu na kujinyoosha mwenyewe kwa yule kijana. Yule kijana alipiga chafya mara saba na kisha akafungua macho yake!
\p
\v 36 Hivyo Elisha akamwita Gehazi na kumwambia, “Mwite yule Mshunami!” Hivyo akamwita, na wakati alipofika kwenye kile chumba, Elisha akasema, “Mchukue mtoto wako.”
\v 37 Kisha akainamisha uso wake chini kwenye miguu yake na kusujudu, na kisha kumchukua mtoto wake na kuondoka.
\s5
\p
\v 38 Kisha Elisha akarudi tena Gilgali. Kulikuwa na njaa katika nchi, na wana wa manabii walikuwa wamekaa mbele yake. Akamwambia mtumishi wake, “Weka sufuria kubwa kwenye moto na pika kwa ajili ya watoto wa manabii.”
\p
\v 39 Mmoja wao akaenda kwenye shamba kukusanya mboga mboga. Alikuta matango ya porini na kukusanya ya kutosha hadi alipojaza kwenye nguo yake. Walizikata na kuziweka kwenye sufuria, lakini hakujua zilikuwa za aina gani.
\s5
\v 40 Basi, wakawapakulia na kusambaziwa kwa watu kwa ajili ya kula. Baadaye, kadiri walivyokuwa wakiendelea kula, walipiga kelele na kusema, “Mtu wa Mungu, kuna kifo kwenye sufuria!” Hivyo wasingeweza kula tena.
\v 41 Lakini Elisha akasema, “Lete unga.” Alitupia kwenye sufuria na kusema, “Pakua kwa watu kwa ajili ya kula, kwa hiyo wanaweza kula.” Kisha hapakuwa kitu chochote kibaya kwenye ile sufuria.
\s5
\p
\v 42 Akaja mtu kutoka Baal Shalisha kwa mtu wa Mungu na kumletea chakula cha kwanza cha mavuno yake mikate Ishirini ya shayiri, na masuke mabichi kwenye gunia. Akasema, “Wape haya watu ili waweze kula.”
\v 43 Mtumishi wake akasema, “Je, niandae hii mbele ya watu mia moja?” Lakini Elisha akasema, “Wapeni hawa watu, ili waweze kula, kwa sababu BWANA anasema, Watakula na kingine kitabaki.”’
\v 44 Basi mtumishi wake akawaandalia mbele yao; wakala, na kuacha kingine kimebaki, kama neno la BWANA lilivyokuwa limesema.
\s5
\c 5
\cl Sura 5
\p
\v 1 Basi Naamani, kamanda wa jeshi la mfalme wa Shamu, alikuwa mtu mkubwa na mtu mwenye kuheshimiwa mbele ya bwana wake, kwa ajili yake BWANA aliwapa ushindi Washami. Pia alikuwa hodari, mtu shujaa, lakini alikuwa ana ukoma.
\p
\v 2 Washami walikuwa wametoka kuongoza kikosi na kumchukua kijana mdogo wa kike kutoka nchi ya Israeli. Akamuhudumia mke wa Naamani.
\s5
\v 3 Yule binti akamwambia bibi yake, “Natamani kwamba bwana wangu angelikuwa pamoja na nabii ambaye yupo Samaria! Halafu angelimponya bwana wangu ukoma wake.
\p
\v 4 Hivyo Naamani akaingia na kumwambia mfalme kile ambacho yule binti kutoka nchi ya Israeli alichokuwa amekisema.
\s5
\v 5 Kisha mfalme wa Shamu akasema, “Nenda sasa, na nitatuma barua kwa mfalme wa Israeli.” Naamani akaondoka na kuchukua talanta zake kumi za fedha, vipande elfu sita vya dhahabu, na nguo kumi za kubadilisha.
\v 6 Pia alichukua barua ya kumpelekea mfalme wa Israeli inayosema, “Sasa wakati hii barua itakapoletwa kwako, utaona kwamba nimemtuma mtumishi wangu Naamani kwako, hivyo basi utamponya ukoma wake.”
\s5
\p
\v 7 Wakati mfalme wa Israeli alipoisoma ile barua, alichana mavazi yake na kusema, “Je mimi ni Mungu, niue na nirudishe uhai, kwamba huyu mtu anataka nimponye mtu ukoma wake? Inaonekana anatafuta vita na mimi.”
\s5
\p
\v 8 Ikawa wakati Elisha mtu wa Mungu aliposikia kwamba mfalme wa Israeli alichana nguo zake, akatuma neno kwa mfalme akisema, “Kwa nini umechana nguo zako? Muache aje kwangu sasa, na atajua kwamba kuna nabii katika Israeli.”
\v 9 Basi Naamani akaja na farasi wake na magari yake ya kukokotwa na farasi na kusimama kwenye mlango wa nyumba ya Elisha.
\v 10 Elisha akamtumia mjumbe, akisema, “Nenda na ukazame mwenyewe katika Yordani mara saba, na ngozi ya mwili wako itajirudi; utakuwa msafi.”
\s5
\p
\v 11 Lakini Naamani alikasirika na kuondoka na kusema, “Tazama, nilidhani bila shaka angekuja kwangu na kusimama na kuliita jina la BWANA Mungu wake, na kupitisha mkono wake kwenye sehemu ya ugonjwa na kuponya ukoma wangu.
\v 12 Je sio Abana na Faepari, mito ya Damaskasi, bora kuliko maji yote ya Israeli? Je siwezi kuoga ndani yao na kuwa safi?” Hivyo akageuka na kwenda kwa hasira.
\s5
\p
\v 13 Ndipo watumishi wa Naamani wakaja karibu na kumwambia, “Baba yangu, kama yule nabii angekuambia kufanya kitu kigumu, usingelifanya? Je si zaidi basi, atakapokwambia rahisi, Zama mwenyewe na uwe safi?’”
\v 14 Ndipo akashuka chini na kuzama mwenyewe mara saba kwenye mto Yordani, akitii maelekezo ya mtu wa Mungu. Nyama ya mwili wake ikarudi tena kama nyama ya mwili wa mtoto mdogo, na alikuwa amepona.
\s5
\p
\v 15 Naamani akarudi kwa yule mtu wa Mungu, yeye na watu wake wengine, na kuja na kusimama mbele yake. Akasema, “Tazama, sasa najua kwamba hakuna Mungu katika Dunia nzima isipokuwa katika Israeli. Kwa hiyo basi, chukua zawadi kutoka kwa mtumishi wako tafadhali.”
\p
\v 16 Lakini Elisha akajibu, “Kama BWANA aishivyo, ambaye nimesimama mbele yake, sitapokea chochote.” Naamani akamsihi Elisha apokee zawadi, lakini alikataa.
\s5
\p
\v 17 Hivyo Naamani akasema, “Kama sivyo, nakuomba acha apewe mtumishi wako pale mzigo wa baghala mbili za udongo, kwa kuwa kuanzia sasa, mtumishi wako hatatoa tena sadaka ya kuteketezwa wala dhabihu kwa mungu yeyote isipokuwa BWANA.
\v 18 Katika jambo hili moja BWANA anaweza kumsamehe mtumishi wako, hii ni, wakati mfalme wangu atakapoenda kwenye nyumba ya Rimoni kuabudu pale, na kujifunza kwenye mikono yangu na kumuinamia mwenyewe kwenye nyumba ya Rimoni, BWANA aweze kumsamehe mtumishi wako katika hili jambo.”
\p
\v 19 Elisha akamwambia, “Nenda kwa amani.” Hivyo Naamani akaondoka.
\s5
\p
\v 20 Alikuwa amesafiri lakini umbali mfupi, wakati Gehazi mtumishi wa Elisha mtumishi wa Mungu alisema mwenyewe, “Tazama, bwana wangu amemuachilia huyu Naamani Mshami kwa kuacha kupokea zawadi kutoka kwenye mikono yake ambazo alizileta. Kama BWANA aishivyo, nitakimbia nikimfuata na kupokea kitu kutoka kwake.”
\p
\v 21 Hivyo Gehazi akamfuata Naamani. Wakati Naamani alipomuona mtu mmoja anakimbia akimfuata, aliruka chini kutoka kwenye gari lake kuonana naye na kusema, “Je kila kitu kiko sawa?”
\p
\v 22 Gehazi akasema, “kila kitu kiko sawa. Bwana wangu amenituma, akisema, Tazama, sasa wamekuja kwangu kutoka nchi ya mlima ya Efraimu vijana wawili wa watoto wa manabii. Tafadhali, wapatie talanta ya fedha na nguo mbili za kubadilisha.’”
\s5
\p
\v 23 Naamani akajibu, “Ninafuraha kubwa kukupatia talanta mbili.” Naamani akamsihi Gehazi na kumpa talanta mbili za fedha kwenye mifuko miwili ya kubebea, pamoja na nguo mbili za kubadilisha, na kutandaza kwa wafanyakazi wake wawili, ambao walikuwa wamebebea ile mifuko miwili ya fedha mbele ya Gehazi.
\v 24 Wakati Gehazi alipokuja kwenye ule mlima, alichukua ile mifuko ya fedha kutoka kwenye mikono yao na kuificha kwenye nyumba; akawatuma wale watu, na wakaondoka.
\v 25 Wakati Gehazi alipoingia na kusimama mbele ya bwana wake, Elisha akamwambia, “Umetokea wapi, Gehazi?” Akajibu, “Mtumishi wako hakwenda mahali.”
\s5
\p
\v 26 Elisha akamwambia Gehazi, “Je roho yangu haikuwa na wewe wakati yule mtu alipoyarudisha magari yake ya farasi ili kukutana na wewe? Je huu ni muda wa kupokea pesa na nguo, mashamba ya mzaituni na mizabibu, na kondoo na Ng'ombe, na watumishi wakiume na watumishi wakike?
\v 27 Basi ukoma wa Naamani utakuwa kwenye uzao wako daima.” Basi Gehazi akatoka kwenye uwepo wake, mwenye ukoma kama theluji.
\s5
\c 6
\cl Sura 6
\p
\v 1 Wana wa manabii wakamwambia Elisha, “Sehemu ambayo tunayoishi na wewe ni ndogo sana kwa ajili ya wote.
\v 2 Tafadhali, tuache tuende Yordani, na umwache kila mtu akate mti hapo ambako tunaweza kuishi.” Elisha akajibu, “Unaweza kwenda mbele.”
\p
\v 3 Mmoja wao akasema, “Nenda na watumishi wako tafadhali.” Elisha akajibu, “Nitaenda.”
\s5
\p
\v 4 Kwa hiyo akaenda pamoja nao, na wakati walipokuja Yordani, wakaanza kukata miti.
\p
\v 5 Lakini mmoja wao alipokuwa akikata, kichwa cha shoka kikaangukia kwenye maji; akalia kwa sauti na kusema, “La hasha, bwana wangu, kilikuwa kimeazimwa!”
\s5
\p
\v 6 Basi mtu wa Mungu akasema, “kiliangukia wapi?” Yule mtu akamwonyesha Elisha ile sehemu. Akakata kijiti, akarusha kwenye maji, na kufanya chuma kuelea.
\v 7 Elisha akasema, “Kichukue.” Basi yule mtu akafikisha mkono wake na kukinyakua.
\s5
\p
\v 8 Basi mfalme wa Shamu alikuwa akipigana vita dhidi ya Israel. Akafanya shauri na watumishi wake, akisema, “kambi yangu itakuwa sehemu fulani na fulani.”
\p
\v 9 Basi huyo mtu wa Mungu akapeleka habari kwa mfalme wa Israeli, akisema, “Kuwa makini usipite ile sehemu, kwa kuwa ndipo Washamu wanakoshukia hapo.”
\s5
\v 10 Mfalme wa Israeli akatuma mjumbe kwenda pale sehemu ambayo mtu wa Mungu alipaongelea na kumtahadharisha. Zaidi ya mara moja au mbili, wakati mfalme alipoenda pale, alikuwa kwenye ulinzi wake.
\p
\v 11 Huyo mfalme wa Shamu alikasirishwa kuhusu haya maonyo, na akawaita watumishi wake na kuwaambia, “Je hamtaniambia ni nani miongoni mwetu aliye upande wa Israeli?”
\s5
\p
\v 12 Hivyo mmoja wa watumishi wake akasema, “Hapana, bwana wangu, mfalme, kwa ajili ya Elisha yule nabii katika Israeli humwambia yule mfalme wa Israeli maneno ambayo uyaongeayo kwenye kitanda chako cha kulala.”
\p
\v 13 Yule mfalme akajibu, “Nenda na uone Elisha alipo hivyo naweza kutuma watu na kumkamata.” Akaambiwa, “Tazama yuko Dothani.”
\s5
\v 14 Kwa hiyo yule mfalme akatuma farasi kwenda Donathi, magari ya farasi, na jeshi kubwa. Wakaja usiku na kuzunguka ule mji.
\p
\v 15 Wakati yule mtumishi wa mtu wa Mungu alipoamka mapema na kutoka nje, kumbe, jeshi kubwa pamoja na farasi na magari ya farasi yameuzunguka mji. Mtumishi wake akamwabia, “Kumbe, bwana wangu! Tutafanya nini?”
\p
\v 16 Elisha akajibu, “Usiogope, wale walio na sisi ni zaidi kuliko wale walio nao.”
\s5
\p
\v 17 Elisha akajibu na kusema, “BWANA, nakuomba kwamba utamfungua macho yake ili kwamba aweze kuona.” Ndipo BWANA alipofungua macho ya mtumishi, na akaona. Kumbe, ule mlima ulikuwa umejaa farasi na magari ya farasi ya moto yamemzunguka Elisha!
\p
\v 18 Wakati hao Washami walipomshukia chini, Elisha aliomba kwa BWANA na kusema, “Uwapige hawa watu kwa upofu, nakuomba.” Hivyo BWANA akawafanya vipofu, kama Elisha alivyoomba.
\p
\v 19 Kisha Elisha akawaambia Washami, “Hii njia sio, pia mji huu sio. Nifuateni mimi, na nitawaleta kwa yule mtu ambaye mnayemtafuta.” Ndipo akawaongoza kwenda Samaria.
\s5
\p
\v 20 Hata walipokwisha kufika Samaria, Elisha akasema, “BWANA, fungua macho ya hawa watu ili waweze kuona.” BWANA akawafungua macho yao na wakaona, na kumbe, walikuwa katikati ya mji wa Samaria.
\p
\v 21 Yule mfalme wa Israeli akamwambia Elisha, wakati alipowaona, “Baba yangu, niwaue? Niwaue?”
\s5
\p
\v 22 Elisha akajibu, “Usiwaue. Ungeweza kuwaua wale ambao uliokuwa umewachukua mateka kwa upanga na upinde wako? Weka mkate na maji mbele yao, ili kwamba waweze kula na kunywa, na kwenda kwa bwana wao.”
\v 23 Ndipo mfalme akaandaa chakula kingi kwa ajili yao, na wakati walipokula na kunywa, akawapeleka mbali, na walirudi kwa bwana wao. Lile kundi la jeshi la Washami halikurudi kwa muda mrefu katika nchi ya Israeli.
\s5
\p
\v 24 Baadaye baada ya huyu Ben Hadadi mfalme wa Shamu kukusanya majeshi yake yote na kuiteka Samaria na kuizingira.
\v 25 Hivyo kulikuwa na njaa kubwa katika Samaria. Kumbe, wakauzingira hadi kichwa cha punda kilipouzwa kwa vipande themanini vya fedha, na sehemu ya nne ya sehemu ya kibaba cha kinyesi cha njiwa kwa vipande vitano vya fedha.
\p
\v 26 Wakati mfalme wa Israeli alipokuwa akipita karibu na ukuta, mwanamke mmoja akamlilia akisema, “Nisaidie, bwana wangu, mfalme.”
\s5
\p
\v 27 Akasema, “Kama BWANA hawezi kukusaidia, je nitakusaidiaje? Je kuna kitu chochote kinakuja kutoka sehemu ya kupuria nafaka au shinikizoni?”
\v 28 Mfalme akaendelea, “Nini kinakusumbua?” Akajibu, “Huyu mwanamke ameniambia, Mtoe mtoto wako ili tuweze kumla leo, na tutamla wa kwangu kesho.’”
\p
\v 29 Hivyo tulimchemsha mtoto wangu na kumla, na siku ya pili yake nikamwambia, “Mtoe mtoto wako ili tuweze kumla, lakini alikuwa amemficha mtoto wake.”
\s5
\p
\v 30 Basi mfalme aliposikia yale maneno ya yule mwanamke, akayachana mavazi yake (sasa alikuwa akitembelea kwenye ukuta), na watu wakatazama na kuona kwamba alikuwa amevaa nguo ya gunia
\v 31 Kisha akasema, “Mungu afanye hivyo kwangu, na zaidi pia, kama kichwa cha Elisha mwana wa Shafati kitabaki juu yake leo.”
\s5
\p
\v 32 Basi Elisha alikuwa ameketi kwenye nyumba yake, na wazee walikuwa wamekaa pamoja naye. Yule mfalme akamtuma mtu wa mbele yake, lakini wakati mjumbe alipokuja kwa Elisha, akawaambia wazee, “Ona jinsi huyu mwana wa muuaji alivyotumwa kuchukua kichwa changu? Tazama, wakati yule mjumbe atakapokuja, funga mlango, na uushikilie huo mlango funga dhidi yake asiingie. Je sio sauti ya bwana wake nyuma mguuni pake?”
\v 33 Wakati alipokuwa bado akiongea pamoja nao, kumbe, yule mjumbe alishuka kwake. Mfalme akasema, “Kumbe, masumbuko haya yatoka kwa BWANA. Kwa nini nimsubiri BWANA tena?”
\s5
\c 7
\cl Sura 7
\p
\v 1 Elisha akasema, “Sikiliza neno la BWANA. Hivi ndivyo Yahwe asemavyo: Kesho muda kama huu kipimo cha unga mzuri kitauzwa kwa shekeli, na vipimo viwili vya shayiri kwa shekeli, kwenye lango la Samaria.’”
\p
\v 2 Basi yule mkuu ambaye alikuwa akitegemea mkono wake akamjibu mtu wa Mungu, na kusema, “Ona, hata kama BWANA ataweka madirisha mbinguni, je jambo hili linawezekana?” Elisha akajibu, “Ona, utaona ikitokea kwa macho yako mwenyewe, lakini hutakula chochote katika hilo.”
\s5
\p
\v 3 Basi, kulikuwa na watu wanne wenye ukoma upande wa nje wa lango la mji. Wakaambizana kila mmoja, “Kwa nini tukae hapa hadi hapo tutakapokufa?
\v 4 Kama tukisema kwamba tutaenda kwenye ule mji, maana mjini kuna njaa, na tutakufa hapo. Lakini kama tukiendelea kukaa hapa, bado tutakufa. Sawa, njooni, twendeni kwenye lile jeshi la Washami. Kama wakitupa uhai, tutakuwa hai, na kama wakituua, tutakufa tu.”
\s5
\v 5 Hivyo wakaamka asubuhi kabla giza halijaisha kwenda kwenye kambi ya Washami; Wakati walipofika sehemu ya mwanzo wa kambi, hapakuwa na mtu hapo.
\p
\v 6 Kwa kuwa Bwana alikuwa amelifanya jeshi la Washami kusikia sauti ya magari ya farasi, na sauti za farasi, sauti za jeshi jingine kubwa, ndipo wakaambizana kila mmoja wao, “Yule mfalme wa Israeli amekodisha wafalme wa Wahiti na Wamisri waje wapigane dhidi yetu.”
\s5
\v 7 Hivyo wale maaskari wakaondoka kungali giza; waliacha mahema yao, punda zao, na kambi kama ilivyokuwa, na kukimbia kwa ajili ya maisha yao.
\p
\v 8 Wakati wale watu wenye ukoma walipokuja sehemu ya mwisho wa kambi, wakaenda kwenye hema moja na kula na kunywa, na kubeba fedha na dhahabu na nguo, na kwenda na kuzificha. Wakarudi na kuingia kwenye hema nyingine na kubeba kutoka pale pia, na kwenda kuvificha.
\s5
\p
\v 9 Basi, wakaambizana kila mmoja, “Hatufanyi sahihi. Siku hii ni siku ya habari njema, lakini tunanyamaza kimya kuhusu hili. Kama tukisubiri mpaka kutakapopambazuka, adhabu itakuwa juu yetu. Basi, njooni, twendeni na kuwaambia nyumba ya mfalme.”
\p
\v 10 Kwa hiyo wakaenda na kuwaita mabawabu wa mji. Wakawaambia, wakisema, “Tumeenda kambi ya Washami, lakini hapakuwa na mtu pale, hakuna sauti ya mtu yeyote, lakini kulikuwa na farasi wamefungwa, na punda wamefungwa, na zile hema kama zilivyokuwa.”
\v 11 Ndipo mabawabu wakatoa habari, ndipo wakaambiwa ndani ya nyumba ya mfalme.
\s5
\p
\v 12 Basi yule mfalme akainuka usiku nakusema kwa watumishi wake, “Nitawaambia sasa kile ambacho Washami walichotufanyia. Wanajua kwamba tuna njaa, hivyo wameondoka kwenye kambi kwenda kujificha kwenye mashamba. Wanasema, Wakati watakapotoka mjini, tutawakamata wakiwa hai, na kuingia mjini.”
\p
\v 13 Mmoja wa wale watumishi wa mfalme akajibu na kusema, “Nakuomba, ngoja baadhi ya watu wachukue farasi watano wale waliosalia, ambao wamebaki kwenye mji. Wako kama mkutano wote wa Israeli waliobaki wengi wamekufa; ngoja tuwatume na tuone.”
\s5
\p
\v 14 Hivyo wakachukua magari mawili ya farasi pamoja na farasi, na mfalme akawatuma baada ya jeshi la Washami, akisema, “Enendeni mkaone.”
\v 15 Wakawafuata kwenda Yordani, na barabara zote zilikuwa zimejaa na vifaa ambavyo Washami walivitupa wapate kukimbia haraka. Kwa hiyo wale wajumbe wakarudi na kumwambia mfalme.
\s5
\v 16 Wale watu wakatoka nje na wakaziteka nyara zile kambi za Washami. Hivyo kipimo cha unga mzuri uliuzwa kwa shekeli moja, na vipimo viwili vya shayiri kwa shekeli moja, kama vile ambavyo neno la BWANA lilivyosema.
\p
\v 17 Naye mfalme alimwagiza yule akida ambaye alitegemea mkono wake kuwa mkuu wa lango, na watu wakamkanyaga chini langoni. Alikufa kama mtu wa Mungu alivyosema, ambaye ameongea wakati yule mfalme alipomshukia.
\s5
\v 18 Basi ikatokea kama yule mtu wa Mungu alivyosema kwa mfalme akisema, “Muda kama huu kwenye lango la Samaria, vipimo viwili vya shayiri vitapatikana kwa shekeli, na kipimo cha unga mzuri kwa shekeli.”
\p
\v 19 Yule akida alimjibu yule mtu wa Mungu na kusema, “Tazama, hata kama BWANA angefanya madirisha mbinguni, je hiki kitu kingeweza kutokea.” Elisha akasema, “Tazama, utaona kikitokea kwa macho yako mwenyewe, lakini hutakula chochote katika hicho.”
\v 20 Hivyo ndivyo haswa kilichompata, kwa kuwa watu wakamkanyaga kwenye lango, na kufa.
\s5
\c 8
\cl Sura 8
\p
\v 1 Basi, Elisha alikuwa amemwambia yule mwanamke ambaye alimfufulia mtoto wake. Akamwambia, “Inuka na uende pamoja na nyumba yako, na uishi popote uwezapo katika nchi nyingine, kwa sababu BWANA ameiita njaa ambayo itakuja katika hii nchi kwa miaka saba.”
\v 2 Basi yule mwanamke akainuka na akatii lile neno la mtumishi wa Mungu. Akaenda na nyumba yake na kuishi kwenye nchi ya Wafilisti miaka saba.
\s5
\p
\v 3 Ikafika kama mwishoni mwa miaka saba yule mwanamke akarudi kutoka kwenye ile nchi ya Wafilisti, na kwenda kwa mfalme kumuomba nyumba yake na kwa ajili ya nchi yake.
\v 4 Basi mfalme alikuwa anaongea na Gehazi yule mtumishi wa Mungu, akisema, “Tafadhali niambie yale mambo makubwa ambayo Elisha ameyafanya.”
\s5
\v 5 Basi alipokuwa akimwambia yule mfalme jinsi gani Elisha alivyomfufua yule mtoto aliyekufa, huyo mwanamke ambaye mtoto wake aliyekuwa amefufuliwa akaja kumuomba yule mfalme kwa ajili ya nyumba yake na nchi yake. Gehazi akasema, “Bwana wangu, mfalme, huyu ndiye yule mwanamke, na huyu ndiye mtoto wake, ambaye Elisha amemfufua.”
\p
\v 6 Wakati yule mfalme alipomuuliza yule mwanamke kuhusu mtoto wake, alimwelezea yule mfalme. Ndipo mfalme akamwagizia akida, akisema, “Mrudishie vyote vilivyokuwa vyake na mavuno yake yote ya mashamba tangu siku alipoondoka hadi sasa.”
\s5
\p
\v 7 Elisha akaja Dameski ambako Ben Hadadi yule mfalme wa Shamu alikuwa anaumwa. Yule mfalme aliambiwa, “Yule mtu wa Mungu amekuja hapa.”
\v 8 Mfalme akamwambia Hazaeli, “Chukua zawadi kwenye mkono wako na uende ukakutane na mtu wa Mungu, na ukazungumze na BWANA kupitia yeye, ukisema, “Je nitapona huu ugonjwa wangu?”
\p
\v 9 Basi Hazaeli akaenda kuonana naye na kuchukua zawadi zake za kila kitu kizuri cha Dameski, akabeba ngamia arobaini. Hivyo Hazaeli akaja na kusimama mbele ya Elisha na kusema, “Mtoto wako Ben Hadadi mfalme wa Shamu amenituma kwako, kusema, “Je nitapona huu ugonjwa?”
\s5
\p
\v 10 Elisha akamwambia, “Nenda, kwa Ben Hadadi, ukamwambie Utapona hakika, lakini BWANA amenionyesha kwamba atakufa hakika.”
\v 11 Basi Elisha akamkazia macho Hazaeli hadi alipojisikia aibu, na yule mtu wa Mungu akalia machozi.
\p
\v 12 Hazaeli akauliza, kwa nini unalia, bwana wangu?” Akajibu, “Kwa sababu najua uovu ambao utakaoufanya kwa watu wa Israeli. Utazichoma moto ngome zao kwa moto, na utawaua vijana wao kwa upanga, kuwaseta vipande vipande watoto wao wachanga, na kuwapasua mimba zao wanawake wenye mimba.”
\s5
\p
\v 13 Hazaeli akajibu, Ni nani mtumwa wako, ambaye atafanya jambo hili kubwa? Yeye ni mbwa tu.” Elisha akajibu, “BWANA amenionyesha kwamba utakuwa mfalme juu ya Shamu.”
\p
\v 14 Ndipo Hazaeli akamwacha Elisha na kuja kwa bwana wake, ambaye alimwambia, “Je Elisha alikwambiaje?” Akajibu, “Ameniambia kwamba utapona bila shaka.”
\v 15 Basi siku ya pili yake Hazaeli akachukua tandiko la kitandai na kulichovya kwenye maji, na kulitandaza kwenye uso wa Ben Hadadi hivyo akafa. Basi Hazaeli akawa mfalme katika sehemu yake.
\s5
\p
\v 16 Katika mwaka wa kumi na tano wa Yoramu mwana wa Ahabu, mfalme wa Israeli, Yehoramu akaanza kutawala. Alikuwa mwana wa Yehoshafati mfalme wa Yuda. Alianza wakati Yehoshafati alikuwa mfalme wa Yuda.
\v 17 Yoramu alikuwa na umri wa miaka thelathini na mbili alipoanza kutawala, na alitawala kwa muda wa miaka minane katika Yerusalemu.
\s5
\v 18 Yoramu akatembea kwenye njia ya huyo mfalme wa Israeli, kama walivyokuwa wakifanya kwenye nyumba ya Ahabu; kwa kuwa alikuwa na binti wa Ahabu kama mke wake, na alifanya uovu machoni pa BWANA.
\v 19 Walakini, kwa sababu ya mtumishi wake Daudi, BWANA hakutaka kuiharibu Yuda, tangu alipomwambia kwamba atampatia wazao.
\s5
\p
\v 20 Katika siku za Yoramu, Edomu akaasi kutoka chini ya mkono wa Yuda, na wakamfanya mfalme juu yao wenyewe.
\v 21 Basi Yoramu akaenda na makamanda wa jeshi na magari ya farasi yote. Ilitokea kwamba akaamka usiku na kushambulia na kuwazunguka Waedomu, waliokuwa wamemzunguka na wale makamanda wa jeshi la magari ya farasi. Ndipo wanajeshi wa Yehoramu wakakimbilia majumbani kwao.
\s5
\v 22 Hivyo Edomu aliasi dhidi ya utawala wa Yuda katika siku hizi. Libna pia aliasi katika kipindi hicho hicho.
\p
\v 23 Kwa mambo mengine yamhusuyo Yehoramu, yote aliyoyafanya, je hayakuandikwa kwenye kitabu cha matukio ya mfalme wa Yuda?
\v 24 Yehoramu akafa na kuzikwa pamoja na baba zake, na akalala pamoja na baba zake katika mji wa Daudi. Ndipo Ahazi mtoto wake akawa mfalme katika sehemu yake.
\s5
\p
\v 25 Katika mwaka wa kumi na mbili wa Yehoramu mwana wa Ahabu, mfalme wa Israeli, Ahazi mwana wa Yehoramu, mfalme wa Yuda, alianza kutawala.
\v 26 Ahazi alikuwa ana umri wa miaka ishirini na mbili wakati alipoanza kutawala; alitawala kwa muda wa mwaka mmoja katika Yerusalemu. Mama yake alikuwa anaitwa Athalia; alikuwa mtoto wa Omri, mfalme wa Israeli.
\v 27 Ahazia alitembelea katika nyumba ya Ahabu; alifanya yale yaliyo maovu katika uso wa BWANA, kama nyumba ya Ahabu ilivyokuwa ikifanya, kwa kuwa Ahazia alikuwa mkwe kwenye nyumba ya Ahabu.
\s5
\p
\v 28 Ahazia akaenda pamoja na Yoramu mwana wa Ahabu, kupigana dhidi ya Hazaeli, mfalme wa Shamu, katika Ramoth Geleadi. Washami wakamjeruhi Yoramu.
\v 29 Mfalme Yoramu akarudi ili auguzwe huko Yezreeli kwenye yale majeraha ambayo Washami walimpatia huko Rama. Wakati alipopigana dhidi ya Hazaeli mfalme wa Shamu. Hivyo Ahazi mwana wa Yehoramu, mfalme wa Yuda, akashuka kwa Yezreeli kumuona Yoramu mwana wa Ahabu, kwa sababu Yoramu alikuwa amejeruhiwa.
\s5
\c 9
\cl Sura 9
\p
\v 1 Nabii Elisha akamwita mmoja wa watoto wa manabii na kumwambia, “Vaa kwa safari, halafu chukua hii chupa ndogo ya mafuta kwenye mikono yako na uende Ramoth Geliadi.
\v 2 Wakati utakapofika, mtafute Yehu mwana wa Yehoshafati mwana wa Nimshi, na uende ukaingie na kumfanya ainuke kutoka miongoni mwa rafiki zake, na ukampeleke katika chumba cha ndani.
\v 3 Kisha chukua ile chupa ya mafuta na imiminie kwenye kichwa chake na kusema, BWANA anasema hivi: “Nimekumiminia mafuta uwe mfalme juu ya Israeli. “Halafu fungua mlango, na kukimbia; usichelewe.”
\s5
\p
\v 4 Basi yule kijana, yule nabii kijana, akaenda Ramoth Geliadi.
\v 5 Wakati alipofika, kumbe, wale majemedari wa lile jeshi walikuwa wamekaa. Hivyo yule nabii kijana akasema, “Nimekuja mara moja na neno kwako, jemedari.” Yehu akajibu, “kwa yupi katika sisi?” Yule nabii kijana akajibu, “Kwako ee Jemedari.”
\p
\v 6 Basi Yehu akainuka na kwenda kwenye nyumba, na yule nabii akammiminia mafuta kwenye kichwa chake na kumwambia Yehu, “BWANA, Mungu wa Israeli, anasema hivi: Nimekumiminia mafuta uwe mfalme juu ya watu wa BWANA, juu ya Israeli.
\s5
\v 7 Wewe lazima uiue familia ya Ahabu bwana wako, ili niweze kulipiza kisasi cha damu ya watumishi wangu manabii, na damu ya watumishi wote wa BWANA, ambao waliokuwa wameuawa kwa mkono wa Yezebeli.
\v 8 Kwa kuwa nyumba yote ya Ahabu itaangamia, na nitamkatilia mbali kila mtoto wa kiume wa Ahabu, yeyote awe mtumwa au mtu huru.
\s5
\v 9 Nitaifanya nyumba ya Ahabu kama nyumba ya Yerobohamu mwana wa Nebati na kama nyumba ya Baasha mwana wa Ahiya.
\v 10 Mbwa watamla Yezebeli katika Yezreeli, na hakutakuwa na mtu wa kumzika.” Kisha nabii akafungua mlango na kukimbia.
\s5
\v 11 Kisha Yehu akatoka kwenda kwa watumishi wa bwana wake, na mmoja akamwambia, “Je kila kitu kiko sawa? Kwa nini huyu mwenda wazimu amekuja kwako?” Yehu akawajibu, “Mnamjua huyo mtu na mambo asemayo.”
\p
\v 12 Wakasema, “Huo ni uongo. Tuambie.” Yehu akajibu, “Alisema hivi na vile juu yangu, na pia akasema, hivi ndivyo BWANA asemavyo: Nimekumiminia mafuta kama mfalme juu ya Israeli.’”
\p
\v 13 Kisha kila mmoja wao akachukua vazi haraka na kuweka chini ya Yehu juu ya madaraja. Wakapiga baragumu na kusema, “Yehu ni mfalme.”
\s5
\p
\v 14 Katika njia hii Yehu mwana wa Yehoshafati mwana wa Nimshi akafanya njama juu ya Yoramu. Basi Yoramu alikuwa akiilinda Ramothi Gileadi, yeye na Israeli yote, kwa sababu ya Hazaeli mfalme wa Shamu,
\v 15 lakini mfalme Yoramu alikuwa amesharudi kwa Yezreeli ili kuponywa yale majeraha aliyokuwa ameyapata na Washami, wakati akiwa anapigana dhidi ya Hazaeli mfalme wa Shamu. Yehu akawaambia watumishi wa Yoramu, “kama hili ndilo wazo lako, kisha usimwache mtu aondoke na kwenda nje ya mji, ili aende kupeleka habari hii Yezreeli.”
\v 16 Basi Yehu akaendesha gari la farasi mpaka Yezreeli; kwa kuwa Yoramu alikuwa amelala huko. Basi Ahazi mfalme wa Yuda alikuwa ameshuka chini kuonana na Yoramu.
\s5
\p
\v 17 Mlinzi alikuwa amesimama juu ya mnara katika Yezreeli, akaliona lile kundi la Yehu alipokuwa akija kwa mbali kidogo; akasema, “Naona kundi la watu wanakuja.” Yoramu akasema, “Chukua mwendesha farasi, na umtume akakutane nao; mwambie aseme, Je mnakuja kwa amani?’”
\p
\v 18 Hivyo mwendesha farasi akatoka kumlaki; akasema, “Mfalme asema hivi: Je mnakuja kwa amani?’” Basi Yehu akasema, “Wewe una nini na amani? Geuka na unifuate nyuma.” Kisha yule mlinzi akamwambia mfalme, Yule mjumbe ameshaonana nao, lakini anarudi.”
\s5
\p
\v 19 Kisha akapeleka mpanda farasi wa pili, ambaye alikuja kwao na kusema, “Mfalme asema hivi: Je mnakuja na amani?”’ Yehu akajibu, “Wewe una nini na amani? Geuka na kunifuata nyuma.
\p
\v 20 Tena yule mlinzi akatoa taarifa, “Amekwisha kuonana nao, lakini hatorudi. Kwa kuwa hilo gari la farasi limekuwa likiendeshwa ndivyo ambavyo Yehu mwana wa Nimshi aendeshavyo; anaendesha kwa kasi.”
\s5
\p
\v 21 Hivyo Yoramu akasema, “Andaa gari langu la farasi liwe tayari.” Wakaandaa gari lake la farasi, na Yoramu mfalme wa Israeli na Ahazi mfalme wa Yuda akaendesha, kila mmoja kwenye gari lake la farasi, kumlaki Yehu. Wakamkuta kwenye mali ya Nabothi Myezreeli.
\v 22 Wakati Yoramu alipomuona Yehu, alisema, “Je unakuja katika hali ya amani, Yehu?” Akajibu, “Amani gani hapo, wakati uzinzi wa ukahaba hufanywa na uchawi wa mama yako Yezebeli umejaa tele?”
\s5
\p
\v 23 Basi Yoramu akarudisha magari yake ya farasi na kukimbia na kumwambia Ahazia, “Kuna uhaini, Ahazia.
\p
\v 24 Ndipo Yehu akauvuta upinde wake kwa nguvu zake zote na kumpiga Yoramu kati ya mabega yake; mshale ukaenda kwenye moyo wake, akaanguka chini kwenye gari lake la farasi.
\s5
\v 25 Ndipo Yehu akamwambia Bidkari Jemedari wake, “Mchukue na mtupie kwenye shamba la Nabothi Myezreeni. Fikiria kuhusu vile ambavyo wewe na mimi tulivyoendesha pamoja baada ya Ahabu baba yake, BWANA aliuweka juu unabii dhidi yake:
\v 26 Jana niliona damu ya Nabothi na damu ya watoto wake asema BWANA na nitahakikisha unalipia hili shamba asema BWANA. Sasa basi, mchukue na mtupe kwenye hili shamba, sawa sawa na neno la BWANA.”
\s5
\p
\v 27 Wakati Ahazi yule mfalme wa Yuda alipoliona hili, akakimbia kwa njia ya Bethi Hagani. Lakini Yehu akamfuata, na kusema, “Muulie humo kwenye gari la farasi,” na wakampiga mahali pa kupandia Guri, karibu na Ebleamu. Ahazi akakimbilia Megido na kufia pale.
\v 28 Watumishi wake wakaubeba mwili wake kwa magari ya farasi kwenda Yerusalemu na kumzika kwenye kaburi lake pamoja na baba zake katika mji wa Daudi.
\s5
\v 29 Basi ilikuwa mwaka wa kumi na moja wa Yoramu mwana wa Ahabu huyo Ahazia akaanza kutawala juu ya Yuda.
\s5
\p
\v 30 Wakati Yehu alipokuja kwa Yezebeli, Yezebeli akasikia juu ya hilo, akapaka wanja kwenye macho yake, akatengeneza nywele zake vizuri, na kuchungulia kwenye dirisha.
\v 31 Kadiri Yehu alipokuwa akiingia kwenye lango, akamwambia, “Je unakuja kwa amani, wewe Zimri, muuaji wa bwana wako?”
\p
\v 32 Yehu akatazama juu ya dirisha na kusema, “Ni nani yuko upande wangu? Nani?” Matowashi wawili au watatu wakachungulia nje.
\s5
\v 33 Basi Yehu akasema, “Mtupeni chini.” Hivyo wakamtupa Yezebeli chini, na damu yake ikamwagika kwenye ukuta na farasi, na Yehu akamkanyaga kanyaga chini ya miguu.
\v 34 Basi Yehu akaingia hiyo sehemu, akala na kunywa. Kisha akasema, “Mtazameni sasa huyu mwanamke aliyelaaniwa na kumzika, kwa kuwa ni binti wa mfalme.”
\s5
\v 35 Wakaenda kumzika, lakini hawakumkuta ila fuvu, miguu, na viganja vya mikono yake.
\v 36 Basi wakarudi na kumwambia Yehu. Akasema, “Hili ndilo neno la BWANA ambalo ameliongea kupitia Eliya Mtishbi, likisema, Katika nchi Yezreeli mbwa ataula mwili wa Yezebeli,
\v 37 na mwili wa Yezebeli utakuwa kama kinyesi juu ya uso wa mashamba katika nchi ya Yezreeli, kwa hiyo basi hakuna atakayeweza kusema, Huyu ni Yezebeli.’”
\s5
\c 10
\cl Sura 10
\p
\v 1 Basi Ahabu alikuwa na watoto sabini katika Samaria. Yehu akaandika barua na kuzituma kwenda Samaria, kwa watawala wa Yezreeli, pamoja na wazee na walinzi wa wana wa Ahabu akisema,
\v 2 Hivyo basi, haraka iwezekanavyo barua hii ikufikiapo “Wana wa bwana wako pamoja nawe, kwa kuwa mna magari na farasi na mji wenye boma na silaha.
\v 3 Mchagueni aliye bora na anayestahili miongoni mwa mtoto wa bwana wenu na kumuweka kwenye kiti cha kifalme cha baba yake, na kupigania ufalme wa bwana wenu.”
\s5
\p
\v 4 Lakini waliogopa na kusema miongoni mwao, “Tazama, wafalme wawili hawatasimama mbele ya Yehu. Hivyo tutasimamaje?”
\p
\v 5 Kisha yule mtu ambaye alikuwa kiongozi kwenye nyumba ya mfalme, na wale waliowalea watoto, wakatuma ujumbe kwa Yehu, kusema, “Sisi ni watumishi wako. Tutafanya chochote utakacho tuamuru. Hatutamfanya mtu yeyote kuwa mfalme. Fanya lile lililo jema machoni pako.”
\s5
\p
\v 6 Kisha Yehu akaandika barua mara ya pili, akisema, “Kama mko upande wangu, na kama mtasikiliza sauti yangu, mtachukua vichwa vya watu wa wana wa mabwana wenu, na mje kwangu Yezreeli kesho muda kama huu.” Ndipo wana wa wafalme, sabini kwa hesabu, waliokuwa watu muhimu huko mjini, ambao walikuwa waliowalea.
\v 7 Hivyo barua ilipokuja kwao, waliwachukua wana wa wafalme na kisha kuwaua, watu sabini, wakaweka vichwa vyao kwenye vikapu, na kuvituma kwa Yehu katika Yezreeli.
\s5
\v 8 Mjumbe mmoja akaja kwa Yehu, akisema, “Wamevileta vile vichwa vya watoto wa wafalme.” Hivyo akasema, viwekeni kwenye mafungu mawili kwenye lango hadi asubuhi.”
\p
\v 9 Asubuhi Yehu akatoka nje na kusimama, na kusema kwa watu wote, “Ninyi hamna hatia. Tazameni, nimefanya fitina dhidi ya bwana wangu na kumuua, lakini ni nani aliyewaua hawa wote?
\s5
\v 10 Sasa hakika tafakarini kwamba hakuna sehemu ya neno la BWANA, lile alilonena BWANA kuhusu familia ya Ahabu, itaanguka kwenye udongo, kwa kuwa BWANA amefanya kile alichokisema kupitia mtumishi wake Eliya.”
\v 11 Basi Yehu akawaua wote waliokuwa wamebakia wa familia ya Ahabu katika Yezreeli, na watu wake muhimu wote, marafiki zake wa karibu, na makuhani wake, hakuna hata mmoja wao alisalia.
\s5
\p
\v 12 Kisha Yehu akainuka na kuondoka; akaenda Samaria. Kadri alivyokuwa akikaribia Bethi Ekedi ya wachungaji,
\v 13 akamlaki na ndugu wa Ahazia mfalme wa Yuda. Yehu akawaambia, “Ninyi ni akina nani?” Wakajibu, “Sisi ni ndugu zake na Ahazia, na tunashuka chini kuwasalimia watoto wa mfalme na watoto wa Malkia Yezebeli.”
\p
\v 14 Yehu akawaambia watu wake mwenyewe, “Wachukue wakiwa hai.” Hivyo wakawachukua wakiwa hai na kuwaua kwenye kisima cha Bethi Ekedi, watu wote arobaini na mbili. Hakumwacha hata mmoja wao akiwa hai.
\s5
\p
\v 15 Baada ya Yehu kuondoka huko, akakutana na Yehonadabu mwana wa Rekabu anakuja kukutana naye. Yehu akamsalimia na kisha akamwambia, “Je moyo wako uko na mimi, kama moyo wangu ulivyo pamoja na wako?” Yehonadabu akajibu, Ndio.” Yehu akasema, “kama ni ndio, nipatie mkono wako.” Kisha Yehonadabu akampatia mkono wake, na Yehu akampandisha Yehonadabu juu kwenye magari ya farasi pamoja naye.
\v 16 Yehu akasema, “Fuatana pamoja nami na uone wivu wangu kwa BWANA.” Hivyo alikuwa na Yehonadabu akiendesha gari la farasi.
\p
\v 17 Wakati alipokuja Samaria, Yehu akawaua wote waliobakia kutoka uzao wa Ahabu katika Samaria, hata akawaangamiza ukoo wa kifalme wa Ahabu, kama walivyokuwa wameambiwa kabla ya neno la Yahwe, ambalo aliloambiwa Eliya.
\s5
\p
\v 18 Kisha Yehu akawakusanya watu wote akawaambia, “Ahabu alimtumikia Baali kidogo, lakini Yehu atamtumikia sana.
\v 19 Basi niitieni manabii wote wa Baali, wote wamwabuduo, na makuhani wake wote. Asikosekane mtu hata mmoja, kwa kuwa nina dhabihu kubwa nataka kutoa kwa Baali. Yeyote atakayeshindwa kuja hataishi.” Lakini Yehu alifanya haya kwa udanganyifu, kwa dhamira ya kuwaua wanaomwabudu Baali.
\p
\v 20 Yehu akasema, “Tengeni muda tuwe na mkutano kwa ajili ya Baali.” Hivyo wakalitangaza.
\s5
\v 21 Kisha Yehu akatuma Israeli yote na wamwabuduo Baali waje, hivyo basi hakuna mtu hata mmoja ambaye aliacha kuja. Walikuja kwenye hekalu la Baali, na ilijaa kutoka mwanzo hadi mwisho.
\v 22 Yehu akamwambia yule mtu aliyekuwa anatunza kabati la nguo za makuhani, “Uwatolee mavazi wote wamwabuduo Baali.” Basi yule mtu akawatolea nguo.
\s5
\p
\v 23 Basi Yehu akaingia pamoja na Yohonadabu mwana wa Rekabu kwenye nyumba ya Baali, na kisha akawaambia wanaomwabudu Baali, “Tafuteni na muhahakishe kwamba hakuna mtu hapa pamoja na ninyi walio watumishi wa BWANA, lakini wamwabuduo Baali peke yao.”
\v 24 Kisha wakaenda kutoa dhabihu na sadaka ya kuteketeza. Basi Yehu alichagua watu themanini ambao walikuwa wamesimama nje, na aliwaambia, Kama mtu yeyote miongoni mwa hawa watu ambao nimewaleta kwenye mikono yenu atoroke, yeyote atakayemwacha huyo mtu atoroke, maisha yake yatachukuliwa kwa ajili ya yule aliyeokoka.”
\s5
\p
\v 25 Hivyo kisha baada ya muda mfupi Yehu alipomaliza kutoa sadaka ya kutekezwa, akamwambia mlinzi na majemedari, “Ingieni na muwaue. Msimwache mtu yeyote atoke.” Basi waliwaua kwa makali ya upanga, na mlinzi na majemedari wakawatupa nje na kwenda kwenye chumba cha ndani cha nyumba ya Baali.
\v 26 Wakazitoa nguzo za mawe ambazo zilikuwa kwenye nyumba ya Baali, na kisha kuzichoma.
\v 27 Kisha wakazivunja zile nguzo za Baali, na kuiharibu nyumba ya Baali na kuifanya choo, ambacho kipo hadi leo.
\p
\v 28 Hivi ndivyo ambavyo Yehu alivyomharibu muabudu Baali kutoka Israeli.
\s5
\v 29 Lakini Yehu hakuacha dhambi za Yeroboamu mwana wa Nebati, ambayo ilifanya Israeli kutenda dhambi ambayo ni kumwabudu ndama wa dhahabu katika Betheli na Dani.
\p
\v 30 Hivyo BWANA akamwambia Yehu, “Kwa kuwa umefanya vema kwa kufanya yaliyo sahihi kwenye macho yangu, na kuitendea nyumba ya Ahabu kulingana na yote yaliyokuwa kwenye moyo wangu, uzao wako utakaa kwenye kiti cha Israeli hadi kizazi cha nne.”
\v 31 Lakini Yehu hakujali kutembea kwenye sheria ya BWANA, Mungu wa Israeli, kwa moyo wake wote. Hakugeuka kutoka kwenye dhambi za Yeroboamu, ambayo iliwafanya Israeli kutende dhambi.
\s5
\p
\v 32 Siku zile BWANA akaanza kupunguza mikoa ya Israeli, na Hazaeli kuwashinda Waisraeli mipakani mwa Israeli,
\v 33 kutoka Yordani upande wa mashariki, nchi yote ya Gileadi, Wagadi, na Wareubeni, na Wamanase, kutoka Aroeri, alipo karibu na bonde la Arnoni, kupita Geleadi hadi Bashani.
\s5
\p
\v 34 Kama kwa mambo mengine yamhusuyo Yehu, na yote aliyoyafanya, na ushujaa wake, je hayakuandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli?
\p
\v 35 Yehu akalala na wazee wake, na walimzika katika Samaria. Kisha Yehoahazi mwanaye akawa mfalme katika sehemu yake.
\v 36 Muda ambao Yehu alitawala juu ya Israeli katika Samaria ulikuwa miaka ishirini na nane.
\s5
\c 11
\cl Sura 11
\p
\v 1 Basi Athalia, mama yake na Ahazia, alipoona kwamba mtoto wake amekufa, aliinuka na kuwaua watoto wote wa kifalme.
\v 2 Lakini Yehosheba, binti wa mfalme Yehoramu na dada wa Ahazia, akamchukua Yoashi mwana wa Ahazia, na kumficha mbali mwa miongoni mwa watoto wa mfalme waliokuwa wameuawa, wakati wote pamoja na mlezi wake; akawaweka kwenye chumba cha kulala. Wakamficha kutoka Athalia kwa hiyo hakuuawa.
\v 3 Alikuwa amoja na Yehosheba, wamejificha kwenye nyumba ya BWANA, kwa muda wa miaka sita, wakati Athalia alipotawala juu ya nchi.
\s5
\p
\v 4 Katika mwaka wa saba, Yehoyada alituma ujumbe na kuleta makamanda wamaamiri jeshi mamia wa Wakari na wa walinzi, na kuwaleta kwake mwenyewe, ndani ya nyumba ya BWANA. Akafanya agano pamoja nao, na kuwaapisha kiapo katika nyumba ya BWANA. Kisha akawaonyesha mtoto wa mfalme.
\v 5 Akawaamuru, akisema, “Hivi ndivyo mnavyotakiwa kufanya. Theluthi yenu mtakaokuja kwenye Sabato mtakuwa mkiiangalia nyumba ya mfalme,
\v 6 na theluthi mtakuwa langoni mwa Suri, na theluthi langoni nyuma ya walinzi.”
\s5
\v 7 Makundi mengine mawili ambayo hayatumikii Sabato, Mtayalinda juu ya nyumba ya BWANA kwa ajili ya mfalme.
\v 8 Ni lazima mumzunguke mfalme, kila mmoja na silaha zake kwenye mkono wake. Yeyote aingiaye ndani ya safu, auwawe. Lazima mkae pamoja na mfalme kila atokapo na kila aingiapo.
\s5
\p
\v 9 Hivyo mamia ya makamanda wamaamri jeshi wakatii kila kitu Yehoyada kuhani alichokiamuru. Kila mmoja akachukua watu wake, wale ambao walitakiwa kuja kutumika siku ya hiyo Sabato, na wale ambao wataacha kuitumika kwenye hiyo Sabato; ndipo wakaja kwa Yehoyada kuhani.
\v 10 Kisha Yehoyada yule kuhani akawapa mikuki na ngao mamia wa makamanda wamaamri jeshi ambayo ilikuwa mali ya mfalme Daudi ambayo ilikuwa kwenye nyumba ya BWANA.
\s5
\v 11 Basi walinzi wakasimama, kila mtu na silaha kwenye mkono wake, kutoka upande wa kuume wa hekalu, kwenda upande wa kushoto, karibu na madhabahu ya hekelu, wakimzunguka mfalme.
\p
\v 12 Kisha Yehoyada akamleta nje mtoto wa mfalme Yoashi, na kumvalisha taji la kifalme, na kumpa ushuhuda. Kisha wakamfanya mfalme na kummiminia mafuta. Wakapiga makofi wakisema, “Mfalme na aishi!”
\s5
\p
\v 13 Wakati Athalia aliposikia sauti za walinzi na za watu, alikuja kwa wale watu kwenye nyumba ya BWANA
\v 14 Akatazama, na, kisha, yule mfalme alikuwa amesimama kwenye nguzo, kama ilivyokuwa desturi, na wakuu na wapiga baragumu walikuwa karibu na mfalme. Watu wote wa nchi hiyo walikuwa wakifurahi na kupiga matarumbeta. Kisha Athalia akachana mavazi yake kwa hasira na kupiga kelele, “Uhaini! Uhaini!”
\s5
\v 15 Ndipo Yehoyada yule kuhani akawaagiza makamanda wa jeshi wa mamia ambao waliokuwa juu ya jeshi, akisema, “Mtoeni kwenye safu.” Atakayemfuata, muueni kwa upanga.” Kwa kuwa kuhani alisema, “Msimwache auawe kwenye nyumba ya BWANA.”
\v 16 Hivyo wakamtwaa kadiri walivyokuwa wakiikaribia hiyo sehemu iliyokuwa na farasi wakaingia chini, na akauawa huko.
\s5
\p
\v 17 Kisha Yehoyada akafanya agano kati ya BWANA na mfalme na watu, ambao wangekuwa watu wa BWANA, na pia kati ya mfalme na watu.
\v 18 Basi watu wote wa nchi wakaenda kwenye nyumba ya Baali na kuiangusha chini. Wakaangusha madhabahu ya Baali na sanamu zake wakazivunja vipande vipande, na kumuua Matani, mfalme wa Baali, mbele ya haya madhabahu. Kisha Yehoyada kuhani akawachagua walinzi juu ya hekalu la BWANA.
\s5
\v 19 Yehoyada akawachukua makamanda wa jeshi wa mamia, Wakari, walinzi, na watu wote wa nchi, na kwa pamoja wakamleta chini mfalme kutoka kwenye nyumba ya BWANA na wakaenda kwenye nyumba ya mfalme, wakaingia kwa njia ya lango la walinzi. Yoashi akachukua nafasi yake kwenye kiti cha enzi cha mfalme.
\v 20 Hivyo watu wote wa nchi wakamsifu, na nchi ilikuwa kimya baada ya Athalia kuuawa kwa upanga kwenye nyumba ya mfalme.
\s5
\p
\v 21 Yoashi alikuwa na umri wa miaka saba tangu alipoanza kutawala.
\s5
\c 12
\cl Sura 12
\p
\v 1 Katika mwaka wa saba wa Yehu, utawala wa Yoashi ulianza; alitawala kwa muda wa miaka arobaini huko Yerusalemu. Mama yake alikuwa anaitwa Sibia, wa Beersheba.
\v 2 Yoashi akafanya yaliyo mema machoni pa BWANA siku zote, kwa sababu Yehoyada kuhani alimfundisha.
\v 3 Lakini sehemu ya juu haikuchukuliwa. Watu wakaendelea kutoa sadaka na kuchoma ubani kwenye sehemu za juu.
\s5
\p
\v 4 Yoashi akamwambia kuhani, “Pesa zote zilizokuja kama sadaka takatifu kwenye nyumba ya BWANA, pesa za matumizi, pesa ya watu kadiri alivyoandikiwa kila mtu, na pesa yote aonayo moyoni mwake kuileta kwenye nyumba ya BWANA
\v 5 makuhani watapokea pesa kutoka miongoni mwa mmoja wa watunza pesa na kutengeneza kila sehemu itakayoonekana imeharibika kwenye hekalu.”
\s5
\p
\v 6 Lakini kama mwaka wa ishirini na tatu wa mfalme Yoashi, makuhani hawakuwa wameandaa kitu chochote kwenye hekalu.
\v 7 Mfalme Yoashi akamwita Yehoyada kuhani na kuhani mwingine; akawaambia, “Kwa nini hamjaandaa kitu chochote kwenye hekalu? Sasa msichukue tena pesa kutoka kwa walipa kodi wenu, lakini chukueni kile kilichokuwa kikikusanywa kwa ajili ya matengenezo ya hekalu na uwapatie wale wanaoweza kufanya matengenezo.
\v 8 Hivyo makuhani wakakubaliana wasichukue pesa tena kutoka kwa watu na wasitengeneze wenyewe.
\s5
\p
\v 9 Badala yake, Yehoyada yule kuhani akachukua kasha, akatoboa tundu kwenye kifuniko chake, na kuliweka karibu na madhabahu, upande wa kulia kama mtu anaingia kwenye madhabahu ya BWANA. Makuhani ambao walikuwa wakilinda mlango wa hekalu wakatumbukiza pesa zote ambazo zilizokuwa zimeletwa kwenye nyumba ya BWANA
\v 10 Ikawa walipoona kwamba kulikuwa na pesa za kutosha kwenye kasha, mwandishi wa mfalme na kuhani mkuu wakaja na kuweka pesa kwenye mifuko na kisha kuhesabu, pesa ikaonekana kwenye nyumba ya BWANA.
\s5
\v 11 Wakawapa pesa ambayo ilikuwa imepimwa kwenye mikono ya watu ambao waliokuwa wanatunza nyumba ya BWANA. Wakawalipa mafundi seremala na wajenzi ambao walikuwa wemefanya kazi kwenye nyumba ya BWANA,
\v 12 na waashi na wakata mawe, kwa ajili ya kununua mbao na kukata mawe kwa ajili ya kutengenezea nyumba ya BWANA, na yote iliyokuwa inahitajika kulipwa kwa ajili ya kuitengeneza.
\s5
\v 13 Lakini ile pesa iliyokuwa imeletwa kwenye nyumba ya BWANA haikulipwa kwa ajili ya vikombe vya fedha, mabeseni, au dhahabu au fedha yoyote ya vyombo.
\p
\v 14 Waliwapa hizi fedha wale ambao waliokuwa wamefanya kazi ya kutengeneza nyumba ya BWANA.
\s5
\v 15 Pia, hakukuhitajika zile pesa zilipwe kwa ajili ya matengenezo ili kuwajibika kwa kuwa watu walizipokea nakuzilipa kwa watenda kazi, kwa sababu hawa watu walikuwa waadilifu.
\v 16 Lakini pesa kwa ajili ya matoleo ya hatia na pesa kwa ajili ya matoleo ya dhambi hazikuwa zimeletwa kwenye hekalu la BWANA, kwa sababu zilikuwa mali ya makuhani.
\s5
\p
\v 17 Kisha Hazaeli mfalme wa Shamu akashambulia na kupigana dhidi ya Gathi, na kuichukua.
\v 18 Ndipo Hazaeli akageuka kuishambulia Yerusalemu. Yoashi mfalme wa Yuda akavichukua vitu vyote ambavyo Yehoshefati na Yehoramu na Ahazia, baba zake, wafalme wa Yuda, na kuviweka wakfu, na vile alivyokuwa ameviweka wakfu, na dhahabu zote zilizokuwa zimeonekana kwenye ghala la nyumba ya BWANA na la mfalme akawatuma kwenda kwa Ahazi mfalme wa Shamu. Kisha Hazaeli akaenda zake kutoka Yerusamu.
\s5
\p
\v 19 Kama mambo mengine yanayomuhusu Yoashi, yote aliyoyafanya, je hayakuandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Yuda?
\v 20 Watumishi wake wakainuka na kupanga pamoja; wakamteka Yoashi katika Bethi Milo, kwenye njia ya kushukia kwa Sila.
\v 21 Yozakari mwana wa Shimeathi, na Yehozabadi mwana wa Shomeri, watumishi wake, wakamshambulia na akafa. Wakamzika Yoashi pamoja na mababu zake katika mji wa Daudi, na Amazia, mtoto wake, akawa mfalme kwenye sehemu yake.
\s5
\c 13
\cl Sura 13
\p
\v 1 Katika mwaka wa ishirini na tatu wa Yoashi mwana wa Ahazia mfalme wa Yuda, Yehoazi mwana wa Yehu alianza kutawala juu ya Israeli katika Samaria; alitawala miaka kumi na saba.
\v 2 Alifanya yaliyo maovu usoni mwa Yahwe na kufuata dhambi za Yeroboamu mwana wa Nebati, ambaye alisababisha Israeli kuasi; na Yehoazi hakurudi kutoka kwao.
\s5
\v 3 Hasira ya Bwana ikawaka juu ya Israeli, na akaendelea kuwakabidhi kwenye mikono ya Hazaeli mfalme wa Shamu na kwenye mikono ya Ben Hadadi mwana wa Hazaeli.
\p
\v 4 Hivyo Yehoazi akamsihi Yahwe, na Yahwe akamsikiliza kwa sababu aliona mateso ya Israeli, vile mfalme wa Shamu alivyokuwa akiwatesa.
\v 5 Basi BWANA akawapa Israeli ulinzi, na wakakimbia kutoka kwenye mikono ya Washami, na watu wa Israeli wakaanza kuishi kwenye nyumba zao kama walivyokuwa kabla.
\s5
\v 6 Hata hivyo, hawakuziacha dhambi za nyumba ya Yeroboamu, ambaye alisababisha Israeli kuasi, na wakaendelea katika hayo; na huyo Ashera akabaki hivyo katika Samaria.
\p
\v 7 Washami wakamuacha Yehoazi pamoja na waendesha farasi hamsini tu, magari ya farasi kumi, na watembea kwa miguu 10,000, kwa ajili ya mfalme wa Shamu alikuwa ameiharibu na kuwafanya kama makapi yaliyopurwa.
\s5
\p
\v 8 Kama mambo mengine yanayomuhusu Yehoazi, na yote aliyoyafanya na nguvu zake, je hayakuandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli?
\v 9 Basi Yehoyazi akalala na mababu zake, na wakamzika katika samaria. Yohoashi mwanaye akawa mfalme katika sehemu yake.
\s5
\p
\v 10 Katika mwaka wa thelathini na saba wa Yoashi mfalme wa Yuda, utawala wa Yehoashi mwana wa Yehoazi ulianza juu ya Israeli katika Samaria; alitawala miaka kumi na sita.
\v 11 Akafanya yaliyo maovu kwenye uso wa Yahwe. Hakuacha nyuma dhambi zozote za Yeroboamu mwana wa Nebati, kwa kuwa aliwafanya Israeli kuasi, lakini alitembea pamoja nao.
\s5
\p
\v 12 Kama kwa mambo mengine yanayomuhusu Yehoashi, na yote aliyoyafanya, na shujaa wake ambaye aliyepigana dhidi ya Amazia mfalme wa Yuda, je hayakuandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli?
\v 13 Yehoashi akalala na mababu zake, na Yeroboamu akakalia kiti chake cha enzi cha kifalme. Yehoashi akazikwa katika Samaria pamoja na wafalme wa Israeli.
\s5
\p
\v 14 Basi Elisha akaugua ugonjwa ambao hatimaye ulimuua, hivyo Yehoashi yule mfalme wa Israeli akashuka chini kwake na kumlilia juu yake. Akasema, “Baba yangu, baba yangu, haya magari ya farasi ya Israeli na hawa waendesha farasi wanakuchukua!”
\p
\v 15 Elisha akamwambia, “Chukua upinde na mishale,” basi Yoashi akachukua upinde na mishale.
\v 16 Elisha akamwambia mfalme wa Israeli, “Weka mkono wako kwenye upinde,” basi akaweka mkono wake kwenye huo. Kisha Elisha akalaza mikono yake kwenye mikono ya mfalme.
\s5
\p
\v 17 Elisha akasema, “Fungua dirisha upande wa mashariki,” basi akalifungua. Kisha Elisha akasema, “Funga,” na akafunga. Elisha akasema, “Huu ndiyo mshale wa ushindi wa Yahwe, huu mshale wa ushindi juu ya Shamu, kwa kuwa utawapiga Washami katika Afeki hadi utakapowaangamiza.”
\p
\v 18 Kisha Elisha akasema, “Chukua mishale,” basi Yoashi akaichukua. Akamwambia mfalme wa Israeli, “Piga chini pamoja nao,” na akapiga chini mara tatu, kisha akaacha.
\v 19 Lakini mtu wa Mungu alikuwa na hasira naye na akasema, “Ungelipiga chini mara tano au mara sita. Ndipo ungeipiga Shamu hadi kuiangamiza, lakini sasa utaipiga Shamu mara tatu tu.”
\s5
\p
\v 20 Kisha Elisha akafa, na wakamzika. Sasa vikundi vya Wamoabi wakaingia kwenye nchi mwanzoni mwa mwaka.
\v 21 Ikawa walipokuwa wakimzika huyo mtu, wakaona kundi la Wamoabi, hivyo wakautupia ule mwili kwenye kaburi la Elisha. Mara yule mtu alipoigusa mifupa ya Elisha, alifufuka na kusimama kwa miguu yake.
\s5
\p
\v 22 Hazaeli mfalme wa Shamu akawatesa Israeli siku zote za Yehoazi.
\v 23 Lakini Yahwe aliwahurumia Israeli, na alikuwa na huruma juu yao na kushughulika kwa ajili yao, kwa sababu ya agano lake na Ibrahimu, Isaka, na Yakobo. Hivyo Yahwe hakuwaangamiza, na bado hakuwatupa kutoka kwenye uwepo wake.
\p
\v 24 Hazaeli mfalme wa Shamu akafa, na Ben Hadadi mtoto wake akawa mfalme katika sehemu yake.
\v 25 Yehoashi mwana wa Yehoazi akairudisha kutoka kwa Ben Hadadi mwana wa Hazaeli miji ambayo aliichukua kutoka Yehoazi baba yake kwa vita. Yehoashi akamshambulia mara tatu, na akaipata miji ya Israeli.
\s5
\c 14
\cl Sura 14
\p
\v 1 Katika mwaka wa pili wa Yehoashi mwana wa Yehoazi, mfalme wa Israeli, Amazia mwana wa Yoashi, mfalme wa Yuda, alianza kutawala.
\v 2 Alikuwa na umri wa miaka ishirini na tano wakati alipoanza kutawala; alitawala kwa muda wa miaka ishirini na tisa katika Yerusalemu.
\v 3 Mama yake alikuwa anaitwa Yehoyadani, wa Yerusalemu. Alifanya yale yaliyo mema usoni mwa macho ya BWANA, sio kama baba yake Daudi. Alifanya kila kitu ambacho Yoashi, baba yake, alichokuwa amekifanya.
\s5
\v 4 Lakini sehemu ya juu haikuondolewa. Watu wakaendelea kutoa dhabihu na kufukiza ubani katika sehemu mahala pa juu.
\p
\v 5 Ikawa mara utawala wake ulipokuwa imara, aliwaua watumishi ambao waliokuwa wamemuua baba yake, mfalme.
\s5
\v 6 Ila hakuwaweka watoto wa wale wauaji kwenye kifo; isipokuwa, alifanya kutokana na kile kilichokuwa kimeandikwa kwenye sheria, kwenye kitabu cha Musa, kama BWANA alivyokuwa ameamuru, akisema, “Wababa wasife kwa ajili ya watoto wao, wala watoto wasife kwa ajili ya makosa ya wazazi wao. Isipokuwa, kila mtu atakufa kwa ajili ya dhambi zake mwenyewe.”
\p
\v 7 Aliua maaskari 10,000 wa Edomi kwenye bonde la chumvi; pia alimchukua Sela kwenye vita na kuiita Yoktheeli, ndivyo paitwavyo hadi leo.
\s5
\p
\v 8 Kisha Amazia akatuma wajumbe kwa Yehoashi mwana wa Yehoahazi mwana wa Yehu mfalme wa Israeli, akisema, “Njoo, tuonane kila mmoja macho kwa macho kwenye mashinadano.”
\p
\v 9 Lakini Yehoashi mfalme wa Israeli akawatuma wajumbe kurudi kwa Amazia mfalme wa Yuda, akisema, “Mbaruti uliokuwa Lebanoni ulituma kwa mwerezi katika Lebanoni, kusema, Mpatie mwanangu binti yako amuoe; lakini hayawani aliyekuwako Lebanoni akaukanyaga chini ule mbaruti.
\v 10 Umempiga sana Edomu, na moyo wako umekuinua. Jisifu katika ushindi wako, lakini kaa nyumbani, kwa nini unataka kujisababishia matatizo na kuanguka, wote wewe na Yuda pamoja nawe?”
\s5
\p
\v 11 Lakini Amazia hakutaka kusikia. Hivyo Yehoashi mfalme wa Israeli akakwea yeye na Amazia mfalme wa Yuda wakakutana uso kwa uso huko Beth Shemeshi, ambayo ilikuwa ya Yuda.
\v 12 Yuda walishindwa mbele ya Israeli, na kila mtu akakimbia nyumbani.
\s5
\v 13 Yehoashi mfalme wa Israeli, akamchukua Amazia, mfalme wa Yuda mwana wa Yehoashi mwana wa Ahazia, huko Beth Shemeshi. Akaja Yerusalemu na kuuangusha chini ukuta wa Yerusalemu kutoka lango la Efraimu mpaka kwenye pembe ya lango, urefu wa mbali wa dhiraa mia nne.
\v 14 Akachukua dhahabu na fedha zote, na vitu vyote ambavyo vilipatikana katika nyumba ya BWANA, na vitu vya thamani kwenye nyumba ya mfalme, pamoja na mateka pia, na kurudi samaria.
\s5
\p
\v 15 Kama ilivyo kwa mambo mengine yamhusuyo Yehoashi, yote aliyoyafanya, ushujaa wake, na jinsi alivyopigana na Amazia mfalme wa Yuda, je hayakuandikwa kwenye kitabu cha matukio ya mfalme wa Israeli?
\v 16 Kisha Yehoashi akalala na wazee wake na ailizikwa katika Samaria pamoja na wafalme wa Israeli, na Yeroboamu, mwanaye, akawa mfalme katika eneo lake.
\s5
\p
\v 17 Amazia mwana wa Yoashi, mfalme wa Yuda, akaishi miaka kumi na tano baada ya Yehoashi mwana wa Yehoahazi, mfalme wa Israeli.
\v 18 Kama ilivyo kwa mambo mengine yanayomhusu Amazia, je hayakuandikwa kwenye kitabu cha matukio ya mfalme wa Yuda?
\p
\v 19 Wakafanya njama dhidi ya Amazia katika Yerusalimu, akakimbilia Lakishi. Akakimbia hadi Lakishi, lakini wakawatuma watu kumfuata hadi Lakishi na kumuua huko.
\s5
\v 20 Wakamrudisha kwa farasi, na alizikwa pamoja na wazee wake katika mji wa Saudi.
\p
\v 21 Watu wote wa Yuda wakamchukua Uzia, ambaye alikuwa na umri wa miaka kumi na minne, na walimfanya kuwa mfalme katika nyumba ya kifalme wa baba yake Uzaria.
\v 22 Alikuwa Uzia ambaye alijenga Elathi na kuirudisha kwa Yuda, baada ya mfalme Uzaria akalala pamoja na mababu zake.
\s5
\p
\v 23 Katika mwaka wa kumi na tano wa Amazia mwana wa Yoashi mfalme wa Yuda, Yeroboamu mwana wa Yoashi mfalme wa Israeli alianza kutawala katika Samaria; alitawala kwa muda wa miaka arobaini na moja.
\v 24 Akafanya yaliyo maovu usoni mwa BWANA. Hakuziacha dhambi zake za Yeroboamu mwana wa Nabeti, ambaye aliisababisha Israeli kuasi.
\v 25 Akairudisha mipaka ya Israeli kutoka Lebo Hamathi mpaka kwenye Bahari ya Araba, kufuata amri ya neno la BWANA, Mungu wa Israeli, ambalo aliongea kupitia mtumishi wake Yona mwana wa Amitai, yule nabii, ambaye alitokea Gathi Heferi.
\s5
\p
\v 26 Kwa kuwa BWANA aliyaona mateso ya Israeli, ambayo yalikuwa makali kwa kila mmoja, wote mtumwa na asiyemtumwa, na kwamba hapakuwa na ulinzi kwa ajili ya Israeli.
\v 27 Basi BWANA akasema kwamba hataweza kulifuta jina la Israeli chini ya mbingu; badala yake, aliwaokoa kwa mkono wa Yeroboamu mwana wa Yehoashi.
\s5
\p
\v 28 Kama ilivyo kwa mambo mengine yamhusuyo Yeroboamu, yote aliyoyafanya, ushujaa wake, jinsi alivyo pigana vita na kuipata tena Dameski na Hamathi, ambayo ilikuwa ya Yuda, kwa Israeli, je hayakuandikwa katika kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli?
\v 29 Yeroboamu akalala na mababu zake, pamoja na mfalme wa Israeli, na Zekaria mtoto wake akawa mfalme katika sehemu yake.
\s5
\c 15
\cl Sura 15
\p
\v 1 Katika mwaka wa ishirini na saba wa Yeroboamu mfalme wa Israeli, Azaria mwana wa Amazia mfalme wa Yuda akaanza kutawala.
\v 2 Azaria alikuwa na umri wa miaka kumi na sita alipoanza kutawala, na alitawala kwa muda wa miaka hamsini na mbili katika Yerusalemu. Mama yake alikuwa anaitwa Yekolia, na alikuwa anatokea Yerusalemu.
\v 3 Alifanya yaliyo mema machoni pa BWANA, kama baba yake Amazia alivyofanya.
\s5
\v 4 Lakini, mahali pa juu hapakuwa pameondolewa. Watu wakaendelea kutoa sadaka na kufukiza ubani katika mahala pa juu.
\p
\v 5 BWANA akampiga mfalme hivyo basi akawa na ukoma mpaka siku ya kifo chake na alikaa kwenye nyumba ya pekee. Yothamu, mtoto wa mfalme, alikuwa juu ya watu na kuwaongoza watu wa nchi.
\s5
\p
\v 6 Kama kwa mambo mengine yanayomhusu Azaria, yote aliyoyafanya, je hayajaandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Yuda?
\v 7 Hivyo Azaria alilala pamoja na babu zake katika mji wa Daudi. Yothamu, mtoto wake, akawa mfalme katika mahala pake.
\s5
\p
\v 8 Katika mwaka wa thelathini na nane mwaka wa Azaria mfalme wa Yuda, Zekaria mwana wa Yeroboamu akatawala juu ya Israeli katika Samaria kwa miezi sita.
\v 9 Alifanya yaliyo maovu usoni mwa BWANA, kama baba zake waliyoyafanya. Hakuziacha dhambi za Yeroboamu mwana wa Nabati, ambaye alisababisha Israeli kuasi
\s5
\p
\v 10 Shalumu mwana wa Yabeshi akafanya njama dhidi ya Zekaria, akamshambulia katika Ibleamu, na kumuua. Kisha akawa mfalme katika mahala pake.
\v 11 Kama kwa mambo mengine yanayomuhusu Zekaria, yameandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli.
\v 12 Hili ndilo lililokuwa neno la BWANA ambalo aliongea na Yehu, kusema, “Kizazi chako kitakaa katika kiti cha Israeli mpaka kizazi cha nne.” Hiyo ikatokea.
\s5
\p
\v 13 Shalumu mwana wa Yabeshi akaanza kutawala katika mwaka wa thelathini na tisa wa Azaria mfalme wa Yuda, na kutawala kwa mwezi mmoja tu katika Samaria.
\v 14 Menahemu mwana wa Gadi akapanda kutoka Tirza kwenda Samaria. Akamshambulia Shalumu mwana wa Yabeshi hapo, katika Samria. Akamuua na kuwa mfalme katika mahali pake.
\s5
\p
\v 15 Kama kwa mambo mengine yanayomuhusu Shalumu na njama aliyoifanya, yameandikwa kwenye kitabu cha matukio cha wafalme wa Israeli.
\p
\v 16 Ndipo Menahemu akamshambulia Tifsa na wote waliokuwa pale, na mipaka yote kuzunguka Tizra, kwa sababu hawakufungua kwenye mji. Hivyo akaushambulia, na akawapasua wanawake wajawazito wote katika hicho kijiji.
\s5
\p
\v 17 Katika mwaka wa thelathini na tisa wa Ahazia mfalme wa Yuda, Menahemu mwana wa Gadi akaanza kutawala; alitawala kwa miaka kumi katika Samaria.
\v 18 Alifanya yaliyo maovu usoni mwa BWANA. Katika maisha yake yote, hakuziacha dhambi za Yeroboamu mwana wa Nabeti, ambaye alifanya Israeli kufanya dhambi.
\s5
\p
\v 19 Kisha Pulu mfalme wa Ashuru akaja kinyume cha nchi, na Menahemu akampatia Pulu talanta 1,000 za fedha, hivyo msaada wa Pulu ungeweza kuwa na yeye kuimarisha utawala wa Israeli katika nchi yake.
\v 20 Menahemu akatoza hii pesa kutoka Israeli kwa kumtaka kila mtu tajiri alipe shekeli hamsini za fedha kwake kumpatia mfalme wa Ashuru. Hivyo mfalme wa Ashuru akarudi na hakukaa pale katika ile nchi.
\s5
\p
\v 21 Kama kwa mambo mengine yanayomuhusu Menahemu, na yote aliyoyafanya, je hayajaandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli?
\v 22 Hivyo Menahemu akalala pamoja na babu zake, na Pekahia mtoto wake akawa mfalme katika mahala pake.
\s5
\p
\v 23 Katika mwaka wa hamsini wa Azaria mfalme wa Yuda, Pekahia mwana wa Menahemu akaanza kutawala juu ya Israeli katika Samaria; alitawala kwa muda wa miaka miwili.
\v 24 Alifanya yaliyo maovu usoni pa BWANA. Hakuziacha dhambi za Yeroboamu mwana wa Nabati, ambazo kwa hizo alisababisha Israeli kufanya dhambi.
\s5
\v 25 Pekahia alikuwa na afisa aliyekuwa anaitwa Peka mwana wa Remalia, ambaye alifanya njama dhidi yake. Pamoja na watu hamsini wa Gileadi, Peka akamuua Pekahia pamoja na Argobu na Arie katika Samaria, katika ngome ya nyumba ya mfalme. Peka akamuua, alipomuua Pekahia akawa mfalme katika mahala pake.
\p
\v 26 Kama kwa mambo mengine yanayomuhusu Pekahia, yote aliyoyafanya, yameandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli.
\s5
\p
\v 27 Katika mwaka wa hamsini na mbili wa Azia mfalme wa Yuda, Peka mwana wa Remalia akaanza kutawala juu ya Israeli katika Samaria; alitawala miaka Ishirini.
\v 28 Alifanya yaliyo maovu usoni mwa Yahwe. Hakuziacha dhambi za Yeroboamu mwana wa Nabati, ambaye alisababisha Israeli kufanya dhambi.
\s5
\p
\v 29 Katika siku za Peka mfalme wa Israeli, Tiglath Pileseri mfalme wa Ashuru akaja na kuichukua Iyoni, Abel Beth Maaka, Yanoa, Kadeshi, Hazori, Gileadi, na nchi yote ya Naftali. Akawachukua hao watu hadi Ashuru.
\p
\v 30 Hivyo Hoshea mwana wa Ela akafanya njama dhidi ya Peka mwana wa Remalia. Akaishambulia na kisha kumuua. Kisha akawa mfalme katika mahali pake, katika mwaka wa ishirini wa Yothamu mwana wa Uzia.
\p
\v 31 Kama kwa mambo mengine yanayomuhusu Peka, yote aliyoyafanya, yameandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli.
\s5
\p
\v 32 Katika mwaka wa pili wa Peka mwana wa Remalia, mfalme wa Israeli, Yothamu mwana wa Azaria, mfalme wa Yuda akaanza kutawala.
\v 33 Alikuwa na umri wa miaka ishirini alipoanza kutawala; alitawala kwa muda wa miaka kumi na sita katika Yerusalimu. Mama yake alikuwa anaitwa Yerusha; alikuwa binti ya Sadoki.
\s5
\v 34 Yothamu alifanya yaliyo sahihi usoni pa Yahwe. Alifuata mfano wa yote baba yake Azaria aliyofanya.
\v 35 Ila, mahali pa juu hapakuchukuliwa. Watu walikuwa wakitoa sadaka na kufukiza ubani katika mahali pa juu. Yothamu akajenga lango la juu la nyumba ya Yahwe.
\p
\v 36 Kama kwa mambo mengine yanayomuhusu Yothamu, na yote aliyoyafanya, je yameandikwa katika kitabu cha matukio ya wafalme wa Yuda?
\v 37 Katika zamani hizo BWANA akaanza kumtuma dhidi ya Yuda Rezini mfalme wa Sahmu, na Peka mwana wa Remalia.
\v 38 Yothamu akalala pamoja na babu zake na akazikwa pamoja na babu zake katika mji wa Daudi, babu yake. Kisha Ahazi, mtoto wake, akawa mfalme katika mahali pake.
\s5
\c 16
\cl Sura 16
\p
\v 1 Katika mwaka wa kumi na saba wa Peka mwana wa Remalia, Ahazi mwana wa Yothamu mfalme wa Yuda, akaanza kutawala.
\v 2 Ahazi alikuwa na umri wa miaka ishirini alipoanza kutawala, na alitawala kwa muda wa miaka kumi na sita katika Yerusalemu. Alifanya yasiyo haki usoni mwa BWANA Mungu wake, kama Daudi baba yake.
\s5
\v 3 Badala yake, akatembea katika njia ya wafalme wa Israeli; hasa, akamuweka mwanaye kwenye moto kama sadaka ya kuteketeza, kufuatana na machukizo ya mataifa, ambayo BWANA aliwafukuza wana wa Israeli.
\v 4 Akatoa sadaka na kuchoma ubani mahali pa juu, juu ya milima, na chini ya kila mti mbichi.
\s5
\p
\v 5 Kisha Riseni, mfalme wa Shamu na Peka mwana wa Remalia, mfalme wa Israeli, wakaja mpaka Yerusalemu kuteka. Wakamzunguka Ahazi, lakini hawakuweza kumshinda.
\v 6 Katika kipindi hicho, Resini mfalme wa Shamu akawarudishia Elathi kwa Shamu na kuwapeleka watu wa Yuda nje ya Elathi. Kisha Washami wakaja kwa Elathi ambapo waliishi hadi leo.
\s5
\p
\v 7 Hivyo Ahazi akatuma wajumbe kwenda kwa Tiglath Pileseri mfalme wa Ashuru, akisema, “Mimi ni mtumishi wako na mwanao. Panda juu na uniokoe kutoka kwenye mikononi ya mfalme wa Shamu na kutoka kwenye mkono wa mfalme wa Israeli, ambao wameniteka.”
\v 8 Hivyo Ahazi akachukua fedha na dhahabu iliyokuwa imepatikana katika nyumba ya BWANA na mingoni mwa waweka hazina wa nyumba ya mfalme na kuituma kama zawadi kwa mfalme wa Ashuru.
\v 9 Kisha mfalme wa Ashuru akamsikiliza, na mfalme wa Ashuru akaenda juu dhidi ya Dameski, akaishinda na kuwabeba watu wake kama wafungwa hadi Kiri. Akamuua Resini pia yule mfalme wa Shamu.
\s5
\p
\v 10 Mfalme Ahazi akaenda Dameski kuonana na Tiglath Pileseri mfalme wa Ashuru. Akaiona madhabahu huko Dameski. Akampelekea Uria kuhani mfano wa ile madhabahu na mpangilio wake na mchoro kwa ustadi wote ulikuwa umehitajika.
\v 11 Hivyo Uria yule kuhani akajenga madhabahu kuwa kama mipango ambayo Mfalme Ahazi atakaporudi kutoka Dameski. Akaimaliza kabla mfalme Ahazi hajarudi kutoka Dameski.
\v 12 Kisha mfalme akaja kutoka Dameski akaiona ile madhabahu; mfalme akaikaribia ile madhabahu na kutoa sadaka juu yake.
\s5
\v 13 Akatengeneza sadaka yake ya kuteketezwa na sadaka yake ya nafaka, na kunyunyiza damu ya washirika wake sadaka juu ya madhabahu.
\v 14 Madhabahu ya shaba ambayo ilikuwa mbele ya Yahwe akaileta kutoka mbele ya hekalu, kutoka kati ya madhabahu yake na hekalu la Yahwe na kuiweka upande wa kaskazini wa madhabahu yake.
\s5
\p
\v 15 Kisha mfalme Ahazi akamwamuru Uria kuhani, akisema, “Juu ya madhabahu kubwa teketeza sadaka ya kutekezwa ya asubuhi na sadaka ya kuteketezwa ya nafaka ya jioni, pamoja na sadaka ya watu wote wa nchi, na matoleo ya sadaka ya mazao na sadaka zao za kinywaji. Nyunyiza juu ya hiyo damu yote ya sadaka ya kuteketeza, na damu yote ya kuteketeza. Lakini ile madhabahu ya shaba itakuwa kwa ajili yangu ili niulize ushauri.”
\v 16 Uria kuhani akafanya kile ambacho Ahazi aliamuru.
\s5
\p
\v 17 Kisha mfalme Ahazi akaondoa jopo na mabeseni vitako vinavyobebeka; pia akachukua bahari kutoka juu ya ng'ombe wa shaba ambayo ilikuwa chini ya hiyo na kuiweka juu ya sakafu ya mawe.
\v 18 Aliondoa njia iliyokuwa kwa ajili ya kuingia kwenye Sabato ambayo walikuwa wamejenga kwenye hekalu, wote pamoja na mahali pa kuingilia mfalme kwenye hekalu la BWANA, kwa sababu ya mfalme wa Ashuru.
\s5
\p
\v 19 Kama kwa mambo mengine yanayomuhusu Ahazi na yale aliyoyafanya, je yameandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Yuda?
\v 20 Ahazi alilala pamoja na baba zake na kuzikwa pamoja na baba zake katika mji wa Daudi. Hezekia mtoto wake akawa mfalme katika mahala pake.
\s5
\c 17
\cl Sura 17
\p
\v 1 Katika mwaka wa kumi na moja wa Ahazi mfalme Yuda, utawala wa Hoshea mwana wa Ela ulianza. Alitawala katika Samaria juu ya Israeli kwa muda wa miaka minane.
\v 2 Alifanya yaliyo maovu usoni pa BWANA, ila sio kama wafalme wa Israeli ambao ulikuwa kabla yake.
\p
\v 3 Shalmanesa mfalme wa Ashuru akamshambulia, na Hoshea akawa mtumishi na kumletea kodi.
\s5
\v 4 Kisha mfalme wa Ashuru akaona kwamba Hoshea alikuwa na njama dhidi yake, kwa kuwa Hoshea aliwatuma wajumbe kwa So mfalme wa Misri; pia, hakumpatia kodi mfalme wa Ashuru, kama alivyofanya mwaka hadi mwaka.
\v 5 Basi mfalme wa Ashuru akamfunga akamtia kifungoni. Kisha mfalme wa Ashuru akaishambulia nchi yote, akaishambulia Samaria na kuizunguka kwa miaka mitatu.
\v 6 Katika mwaka wa tisa wa Hoshea, mfalme wa Ashuru akaichukua Samaria na akawapeleka Israeli hadi Ashuru. Akawaweka kwenye Hala, kwenye Habori Mto wa Gozani, na katika mji wa Wamedi.
\s5
\p
\v 7 Utekwaji huu ulitokea kwa sababu wana wa Israeli walifanya dhambi dhidi ya BWANA Mungu wao, ambaye aliwaleta kutoka nchi ya Misri, kutoka chini ya mkono wa Farao mfalme wa Misri. Watu walikuwa wakiabudu miungu mingine
\v 8 na kutembea katika matendo ya wamataifa ambao BWANA aliwafukuza mbele ya watu wa Israeli, na katika matendo ya wafalme wa Israeli ambayo waliyokuwa wameyafanya.
\s5
\v 9 Wana wa Israeli wakafanya kwa siri mambo mabaya dhidi ya BWANA Mungu wao. Wakajijengea mahala pa juu katika miji yao yote, kutoka mnara wa walinzi hadi mji wenye boma.
\v 10 Pia wakasimamisha nguzo za mawe na Ashera juu ya kila mlima chini ya kila mti mbichi.
\s5
\v 11 Huko wakafukiza ubani katika mahali pa juu pote, kama mataifa walivyokuwa wamefanya, ambao Yahwe aliwafukuza mbele yao. Waisraeli wakafanya mambo maovu ili kuchochea hasira ya BWANA,
\v 12 wakaabudu sanamu, ambazo BWANA alizokuwa amewaambia, “Msifanye jambo hili.”
\s5
\v 13 Bado BWANA aliwashuhudia Israeli na Yuda kwa kila nabii na kila muonaji, kusema, “Geukeni kutoka njia zenu mbaya na kuzishika amri zangu na hukumu zangu, na kuwa makini kufuata ile sheria yote niliyowaamuru baba zenu, na ambayo niliwapelekea kwa watumishi wangu manabii.”
\s5
\p
\v 14 Lakini hawakuweza kusikia; badala yake walikuwa wakaidi kama baba zao ambao hawakumwamini BWANA Mungu wao.
\v 15 Walizikataa sheria zake na lile agano ambalo alilifanya pamoja na babu zao, na hilo agano wakakubaliana wapewe. Wakafuata mambo yao yasiyofaa na wakawa hawafai. Wakawafuata mataifa ya kipagani ambayo yaliwazunguka, ambao BWANA alikuwa amewaamuru wasiige.
\s5
\p
\v 16 Wakazipuuza amri zote za BWANA Mungu wao. Wakatengeneza sanamu za kusubu za ndama wawili kuziabudu. Wakatengeza nguzo ya Ashera, na wakaziabudu nyota zote za mbinguni na Baali.
\v 17 Wakawatupia watoto wao wakike kwa wakiume kwenye moto, wakapiga ramli na uchawi, wakajiuza wenyewe kufanya yale ambayo yalikuwa maovu usoni pa BWANA, na kuichochea hasira yake.
\p
\v 18 Kwa hiyo BWANA alikuwa na hasira na Israeli na kuwaondoa usoni mwake. Hakubakia mtu hata mmoja isipokuwa kabila la Yuda peke yake.
\s5
\v 19 Hata watu wa Yuda hawakushika amri za BWANA Mungu wao, lakini badala yake walifuata mambo hayo hayo ya kipagani ambayo Israeli walifuata.
\v 20 Hivyo BWANA akawakataa vizazi vyote vya Israeli; akawatesa na kuwatia kwenye mkono wa wale wenye kuwateka nyara, hadi atakapokuwa amewatupa usoni mwake.
\s5
\p
\v 21 Akawatoa Israeli kutoka kwenye mstari wa kifalme wa Daudi, na wakamfanya Yeroboamu mwana wa Nebati mfalme. Yeroboamu akawapeleka Israeli mbali kutoka kumfuata BWANA na kuwafanya wafanye dhambi kubwa.
\v 22 Wana wa Israeli wakafuata dhambi zote za Yeroboamu na hawakujiepusha nazo,
\v 23 basi BWANA akawaondoa Israeli kutoka usoni pake, kama alivyokuwa amesema kupitia watumishi wake wote manabii kwamba angeweza kufanya. Hivyo Israeli walichukuliwa kutoka nchi yao kwenda Ashuru, na iko hivyo hata leo.
\s5
\p
\v 24 Mfalme wa Ashuru akawaleta watu kutoka Babeli na kutoka Kutha, na kutoka Ava, na kutoka Hamathi na Sefarvaimu, na kuwaweka katika mji wa Samaria na kuishi katika huo mji wake.
\v 25 Ikatokea wakati walipoanza kuishi huko hawakumcha BWANA. Hivyo BWANA akatuma simba miongoni mwao ambao waliwaua baadhi yao.
\v 26 Basi wakaongea na mfalme wa Ashuru, wakisema, “Wale mataifa uliowahamisha na kuwaweka kwenye miji ya Samaria hawayajui mambo wanayotakiwa kuyafanya kutokana na mungu wa nchi. Hivyo alikuwa amewatuma simba kwenda kwao, na, tazama, wale simba walikuwa wakiwaua watu huko kwa sababu hawakufahamu yale mambo waliyokuwa wanatakiwa kuyafanya kwa mungu wa nchi.”
\s5
\p
\v 27 Kisha mfalme wa Ashuru akatoa amri, akisema, “Mchukueni mmoja wa makuhani hapo ambaye mmemleta kutoka huko, na mumwache aende na kuishi huko, na mumwache awafundishe mambo yanayotakiwa kwa mungu wa nchi.”
\v 28 Hivyo mmoja wa makuhani ambaye walimchukua kutoka Samaria akaja na kuishi katika Betheli; akawafundisha jinsi wanavyotakiwa kumcha MUNGU.
\s5
\p
\v 29 Watu wa kila kabila wakajifanyia miungu yao wenyewe, na kuiweka mahala pa juu ambapo Wasamaria walifanya kila kabila katika mji ambako walipoishi.
\v 30 Watu wa Babeli wakatengeneza Sakoth Benithi; watu wa Sakoth wakatengeneza Nergali; watu wa Hamathi wakatengeza Ashima;
\v 31 Waavi wakatengeneza Nibhazi na Tartaki. Nao Wasefarvi wakachoma watoto wao kwenye moto kwa Adrameleki na Anameleki, wale miungu wa Sefarvaimu.
\s5
\v 32 Pia wakamcha BWANA, na kuwateua kutoka miongoni mwao makuhani wa mahali pa juu, ambao waliteketeza kwa ajili yao kwenye hekaluni mahali pa juu.
\p
\v 33 Wakamcha BWANA na pia kuabudu miungu yao wenyewe, sawa sawa na tamaduni za mataifa kutoka miongoni mwao waliokuwa wamewachukua.
\s5
\v 34 Hadi siku hii ya leo wameshikilia tamaduni zao za zamani. Wala hawamwogopi BWANA, wala hawazifuati sheria zake, torati, au amri ambazo BWANA aliwapa watu wa Yakobo ambaye alimwita jina Israeli
\v 35 pamoja na ambao BWANA alifanya agano nao na kuwaamuru, “Msiiche miungu mingine, wala kuisujudia, wala kuiabudu, wala kuitolea sadaka.
\s5
\v 36 Lakini BWANA, ambaye aliwatoa kutoka nchi ya Misri kwa nguvu kubwa na mkono ulionyooshwa, yeye ndiye mnayetakiwa kumwabudu, yeye ndiye mnayetakiwa kumsujudia, na yeye ndiye mnayetakiwa kumtolea sadaka.
\v 37 Na sheria na hukumu, na torati na amri ambazo alizoziandika kwa ajili yenu, mtazishika milele. Hivyo msiiche miungu mingine,
\v 38 na agano ambalo nimelifanya pamoja nanyi, hamtalisahau; wala kuicha miungu mingine.
\s5
\v 39 Lakini BWANA Mungu wenu, ndiye ambaye mtakayemcha. Atawalinda mbali na nguvu ya maadui zenu,”
\p
\v 40 Hawakusikia, kwa sababu waliendelea kufanya yale waliyokuwa wameyafanya nyuma.
\v 41 Hivyo haya mataifa wakamcha wakamcha BWANA na pia wakaabudu sanamu zao za kuchonga, na watoto wao wakafanya hivyo na watoto wao, Wakaendelea kufanya yale ambayo baba zao waliyoyafanya, hata leo.
\s5
\c 18
\cl Sura 18
\p
\v 1 Ikawa katika mwaka wa tatu wa Hoshea mwana wa Ela, mfalme wa Israeli, Hezekia mwana wa Ahazi, mfalme wa Yuda akaanza kutawala.
\v 2 Alikuwa na umri wa miaka ishirini na tano alipoanza kutawala; alitawala miaka ishirini na tisa katika Yerusalemu. Jina la mama yake alikuwa anaitwa Abija; alikuwa binti wa Zekaria.
\v 3 Alifanya yaliyo mema usoni pa BWANA, kufuata mfano wa yote ambayo Daudi, babu yake, aliyoyafanya.
\s5
\v 4 Alipaondoa mahali pa juu, akaiharibu nguzo ya jiwe, akaikata hiyo nguzo ya Ashera. Akavunja vipande vipande ile nyoka ambayo Musa aliyokuwa ameifanya, kwa sababu siku zile wana wa Israeli walikuwa wakichoma ubani katika hiyo; ilikuwa inaitwa “Nehushtani.”
\p
\v 5 Hezekia alimwamini BWANA, Mungu wa Israeli, hivyo basi baada ya yeye hapakuwa kama yeye miongoni mwa wafalme wote wa Yuda, wala miongoni mwa wafalme ambao walikuwa kabla yake.
\s5
\v 6 Aliambatana na BWANA. Hakuacha kumfuata lakini alizifuata amri zake, ambazo BWANA alimwamuru Musa.
\v 7 Hivyo BWANA alikuwa na Hezekia, kila alipokwenda alifanikiwa. Akaasi dhidi ya mfalme wa Ashuru na hakumtumikia.
\v 8 Akawashambulia Wafilisti hadi Gaza na mipaka inayoizunguka, kutoka mnara wa walinzi hadi mji wenye ngome.
\s5
\p
\v 9 Katika mwaka wa nne wa Mfalme Hezekia, ambao ulikuwa mwaka wa saba wa Hoshea mwana wa Ela mfalme wa Israeli, Shalmanesa mfalme wa Ashuru akapanda hadi Samaria na kuizunguka.
\v 10 Mwishoni mwa miaka mitatu wakaichukua, katika mwaka wa sita wa Hezekia, ambao ulikuwa mwaka wa tisa wa Hoshea mfalme wa Israeli; hivi ndivyo Samaria ilivyotekwa.
\s5
\v 11 Basi mfalme wa Ashuru akawachukua Israeli kwenda Ashuru na kuwaweka kwenye Hala, na katika mto Habori katika Gozani, na katika mji wa Wamedi.
\v 12 Alifanya hivi kwa sababu hawakutii sauti ya BWANA Mungu wao, lakini walikiuka makubaliano ya agano lake, yote yale ambayo Musa yule mtumishi wa BWANA aliwaamuru. Walikataa kuyasikiliza au kuyafanya.
\s5
\p
\v 13 Kisha katika mwaka wa kumi na nne wa mfalme Hezekia, Senakerebu mfalme wa Ashuru akaishambulia miji yote yenye boma na kuwateka mateka.
\v 14 Basi Hezekia mfalme wa Yuda akatuma neno kwenda kwa mfalme wa Yuda akatuma neno kwa mfalme wa Ashuru, ambaye alikuwa Lakishi, akisema, “Nimekuudhi. Nichukue. Popote utakaponiweka nitavumulia.” Mfalme wa Ashuru akamtaka Hezekia mfalme wa Yuda kulipa talanta mia tatu za fedha na talanta thelathini za dhahabu.
\p
\v 15 Hivyo Hezekia akampatia fedha zote ambazo zilikuwa zimepatikana kwenye nyumba ya BWANA na kwenye hazina ya nyumba ya mfalme.
\s5
\p
\v 16 Kisha Hezekia akaikata ile dhahabu kutoka kwenye milango ya hekalu la BWANA na kutoka juu ya nguzo; akampatia dhahabu mfalme wa Ashuru.
\v 17 Lakini mfalme wa Ashuru akalihamasisha jeshi lake kubwa, akawatuma Tartani na Rabsarisi na amiri jeshi mkuu kutoka Lakishi kwenda kwa Hezekia huko Yerusalemu. Wakasafiri hadi kwenye mabarabara na kufika nje ya Yerusalemu. Wakakaribia karibu na mfereji wa birika la juu, kwenye barabara kuu ya shamba la dobi, na kusimama hapo.
\v 18 Wakati walipokuwa wamemwita Mfalme Hezekia, Eliakimu mwana wa Hilkia, ambaye alikuwa kiongozi wa nyumba ya mfalme na Shebna mwandishi, na Joa mwana wa Asafu, anayeandika kumbukumbu, wakatoka nje kwenda kuwalaki.
\s5
\p
\v 19 Basi yule amiri jeshi mkuu akawaambia wamwambie Hezekia kile alichosema mfalme mkuu, mfalme wa Ashuru, amesema: “Nini chanzo cha ujasiri wako?
\v 20 Unaongea maneno yasiyo na maana, kusema lipo neno na nguvu ya vita. Sasa unamtumainia nani? Nani anakupa ujasiri wa kuasi dhidi yangu?
\v 21 Tazama, unatumainia kutembelea fimbo ya mwanzi huu uliopondeka wa Misri, lakini kama mtu akiutegemea, utamchapa kwenye mkono wake na kuutoboa. Hivyo ndivyo alivyo Farao mfalme wa Misri kwa mtu yeyote ambaye anayemtumainia.”
\s5
\v 22 Lakini kama ukiniambia, “Tunamwamini BWANA Mungu wetu;” je si yeye ambaye mahali pa juu na madhabahu Hezekia amezichukua, na kumwambia Yuda na kwa Yerusalemu, Lazima uabudu mbele ya hii madhabahu katika Yerusalemu?
\p
\v 23 Basi kwa hiyo, nataka kukufanyia ahadi nzuri kutoka kwa bwana wangu mfalme wa Ashuru. Nitakupatia farasi 2,000, kama unaweza kuwatafuta wa kuwaendesha kwa ajili yao.
\s5
\v 24 Wawezaje kumpinga hata akida mmoja wa watumishi walio wadogo? Mmeweka tumaini lenu katika Misri kwa magari ya farasi na waendesha farasi!
\v 25 Je nimesafiri kwenda huko juu bila BWANA kupapigania hapa mahali na kupaharibu? BWANA ameniambia, Ishambulie hii nchi na uiharibu.”’
\s5
\p
\v 26 Kisha Elikana mwana wa Hilkia, na Shebna, na Joa wakamwambia amiri jeshi mkuu, “Tafadhali ongea na watumishi wako katika lugha ya Kiaramu, kwa kuwa tunaielewa. Usiongee nasi katika lugha ya Yuda katika masikio ya watu ambao wako ukutani.”
\p
\v 27 Lakini yule amiri jeshi mkuu akawaambia, “Je bwana wangu amenituma kwa bwana wako na kwako niyaseme maneno haya? Je hajanituma kwa hawa watu ambao wameketi kwenye ukuta, ambao watakula kinyesi chao na kunywa mkojo wao wenyewe?”
\s5
\p
\v 28 Kisha yule amiri jeshi mkuu akasimama na akapiga kelele kubwa kwa lugha ya Kiyahudi, akisema, “Sikilizeni neno la mfalme mkuu, mfalme wa Ashuru.
\v 29 Mfalme asema, Msimwache Hezekia akawadanganya, kwa kuwa hataweza kuwaokoa kwenye nguvu yangu.
\v 30 Msimwache Hezekia akawatumainisha katika BWANA, akisema, BWANA atatuokoa hakika, na huu mji hautawekwa kwenye mkono wa mfalme wa Ashuru.
\s5
\p
\v 31 Msimsikilize Hezekia, kwa kuwa hivi ndivyo mfalme wa Ashuru asemavyo: Fanyeni amani pamoja nami na njooni kwangu. Kisha kila mmoja wenu atakula kutoka kwenye mzabibu wake mwenyewe na kutoka kwenye mtini wake mwenyewe, na kunywa kutoka kwenye maji kwenye maji ya birika lake mwenyewe.
\v 32 Mtafanya hivyo hadi nitakapokuja na kuwachukua kwenda kwenye nchi kama nchi yenu, nchi ya nafaka na divai, nchi ya mkate na mashamba ya mizabibu, nchi ya miti ya mizaituni na asali, ili muweze kuishi na sio kufa. Msimsikilize Hezekia wakati atakapojaribu kuwashawishi, akisema, BWANA atatuokoa.
\s5
\v 33 Je miungu yeyote ya watu inaweza kuwaokoa kutoka kwenye mikono ya mfalme wa Ashuru?
\v 34 Iko wapi miungu ya Hamathi na Arpadi? Iko wapi miungu ya Sefarvaimu, Hena, na Iva? Je imeiokoa Samaria kutoka mkono wangu?
\v 35 Miongoni mwa miungu yote ya nchi, je kuna mungu ambaye ameiokoa nchi yake kutoka kwenye nguvu yangu? Inawezekanaje BWANA akaiokoa Yerusalemu kutoka kwenye uwezo wangu?”
\s5
\p
\v 36 Lakini watu wakabaki kimya na hawakujibu, kwa kuwa mfalme alikuwa ameamuru, “Msimjibu.”
\p
\v 37 Kisha Eliakimu mwana wa Hilkia, ambaye alikuwa juu ya nyumba ya mfalme; Shebna yule mwandishi; na Joa mwana wa Asafu, mtunza kumbukumbu, akaja kwa Hezekia pamoja na nguo zao zilizoraruliwa, na kumpatia taarifa ya maneno ya yule amiri mkuu.
\s5
\c 19
\cl Sura 19
\p
\v 1 Ikawa kuhusu kwamba wakati Mfalme Hezekia aliposikia taarifa zao, akararua mavazi yake, akavaa nguo za magunia, na kwenda kwenye nyumba ya BWANA.
\v 2 Akamtuma Elkana, ambaye alikua msimamizi wa nyumba ya mfalme, na Shebna yule mwandishi, na wazee wa makuhani, wote walikuwa wamefunikwa na nguo za magunia, kwenda kwa Isaya mwana wa Amozi, yule nabii.
\s5
\v 3 Wakamwambia, Hezekia wakisema, “Siku hii ni siku ya mateso, shutuma, na fedheha, kwa kuwa wakati umewadia watoto kuzaliwa, lakini hakuna nguvu ili wazaliwe.
\v 4 Inaweza kuwa BWANA Mungu wako atasikia maneno yote ya amiri jeshi mkuu, ambaye mfalme wa Ashuru bwana wake amemtuma kumdhihaki Mungu aliye hai, naye atayakemea yale maneno ambayo BWANA Mungu wako aliyasikia. Sasa inua maombi yako juu kwa ajili ya mabaki yaliyo bakia hapo.”’
\s5
\p
\v 5 Hivyo watumishi wa mfalme Hezekia wakaja kwa Isaya,
\v 6 na Isaya akawaambia, “Mwambieni bwana wenu: BWANA asema hivi, Usiyaogope maneno ambayo uliyoyasikia, pamoja na kwamba watumishi wa mfalme wa Ashuru wamenitukana.
\v 7 Tazama, nitaweka roho ndani yake, na yamkini atasikia taarifa na kurudi kwenye nchi yake mwenyewe. Nitamfanya aanguke kwa upanga katika nchi yake mwenyewe.’”
\s5
\p
\v 8 Kisha amiri jeshi mkuu akarudi na kumkuta mfalme wa Ashuru akipigana dhidi ya Libna, kwa kuwa alisikia kwamba mfalme alikuwa ameenda kutoka Lakishi.
\p
\v 9 Kisha Senakeribu akasikia kwamba Tirhaka mfalme wa Kushi na Misri alihamasisha kupigana dhidi yake, hivyo akatuma wajumbe tena kwa Hezekia pamoja na ujumbe:
\s5
\v 10 “Mwambieni Hezekia mfalme wa Yuda, Asikudanganye Mungu wako unayemwamini, kusema, Yerusalemu haitawekwa kwenye mikono ya mfalme wa Ashuru.
\v 11 Tazama, umesikia kwamba wafalme wa Ashuru wamemaliza nchi zote kwa kuziharibu kabisa. Kwa hiyo je utaokoka?
\s5
\v 12 Je wale miungu wa mataifa wamewaokoa, mataifa ambao baba zangu waliyaharibu: Gozani, Harani, Resefu, na watu wa Edeni katika Telasari?
\v 13 Je yuko wapi mfalme wa Hamathi, mfalme Arpadi, mfalme wa miji ya Sefarvaimu, wa Hena, na Iva?’”
\s5
\p
\v 14 Hezekia akapokea hii barua kutoka wale wajumbe na kuisoma. Kisha akapanda hata kwenye nyumba ya BWANA na kuukunjua mbele yake.
\v 15 Kisha Hezekia akaomba mbele ya BWANA na kusema, “BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, uketiye juu ya makerubi, wewe ni Mungu wa pekee juu ya tawala zote za dunia. Uliyeziumba mbingu na nchi.
\s5
\v 16 Tega sikio lako, BWANA, na usikie. Fungua macho yako, BWANA, na tazama, na sikia maneno ya Senakeribu, ambayo ameyatuma kumdhihaki Mungu aliye hai.
\p
\v 17 Ni kweli BWANA, wafalme wa Ashuru wameyaharibu mataifa na nchi zao.
\v 18 Wameiweka miungu yao kwenye moto, kwa kuwa hawakuwa miungu lakini ilikuwa kazi ya mikono ya watu, ilikuwa miti na mawe. Hivyo Waashuru wamewaharibu.
\s5
\v 19 Basi sasa, BWANA Mungu wetu, tuokoe, nakusihi, kutoka kwenye nguvu zake, ili kwamba mamlaka zote za dunia zipate kujua ya kwamba wewe, BWANA, ndiye Mungu wa pekee.”
\s5
\p
\v 20 Kisha Isaya mwana wa Amozi akatuma ujumbe kwa Hezekia, akisema, “BWANA, Mungu wa Israeli asema, Kwa sababu umeomba kwangu kuhusiana na Senakeribu mfalme wa Ashuru, nimekusikia.
\v 21 Hili ndilo neno ambalo BWANA ameliongea kuhusu yeye: Bikira binti Sayuni amekudharau na kukucheka kwa dharau. Binti wa Yerusalemu akatikisa kichwa juu yako.
\q
\v 22 Je ni nani uliyemchokoza na kumtukana? Dhidi ya nani umeinua sauti yako na kuinua macho yako katika majivuno? Juu ya Mtakatifu wa Israeli!
\s5
\q
\v 23 Kupitia wajumbe wako wamemdharau Bwana, na kusema, Pamoja na wingi wa magari yangu ya farasi nimeenda juu ya vilele ya milima, hata juu ya kilele cha Lebanoni. Nitaikata mierezi mirefu na kuchagua miti ya mivinje huko. Nitaingia sehemu za makazi yake yaliyo mbali, msitu wake uzaao sana.
\q
\v 24 Nimechimba visima na kunywa maji mageni. Nimekausha mito yote ya Misri chini ya nyayo za miguu yangu.
\s5
\q
\v 25 Je hukusikia jinsi nilivyoagiza tangu zamani, na kuyafanya tangu siku za zamani? Sasa ninalileta kupita. Uko hapa kupunguza miji isiyoingilika kwenye rundo la maangamizi.
\q
\v 26 Makazi yao, ya nguvu kidogo, imevunjwa vunjwa na aibu. Wamekuwa mimea katika shamba, majani ya kijani, majani juu kwenye dari au kwenye shamba, lililochomwa kabla halijakua.
\s5
\q
\v 27 Lakini najua kuketi kwako chini, na kutoka kwako, kuingia kwako dhidi yangu.
\q
\v 28 Kwa sababu kiburi chako kimeyafikia masikio yangu, nitaweka kulabu yangu kwenye pua yako, na hatamu yangu kwenye mdomo wako; nitakurudisha nyuma kwa njia ile ile uliyoijia.”
\s5
\q
\v 29 Hii ndiyo itakuwa ishara kwako: Mwaka huu mtakula vitu viotavyo porini, na katika mwaka wa pili vile vikuavyo katika huo. Lakini katika mwaka wa tatu ni lazima mpande na kuvuna, kupanda mashamba ya mizabibu na kula matunda yake.
\q
\v 30 Mabaki ya nyumba ya Yuda ambayo yataokoka yatachukua tena mizizi na kuzaa matunda.
\q
\v 31 Kwa kuwa mabaki yatatoka Yerusalemu, kutoka Mlima Sayuni wenye kuokoka utakuja. Wivu wa BWANA wa majeshi utafanya hivyo.
\s5
\q
\v 32 Kwa hiyo BWANA asema hivi kuhusu mfalme wa Ashuru: “Hatakuja kwenye huu mji wala kupiga mshale hapa. Wala hatakuja mbele yake na ngao au kujenga boma dhidi yake.
\q
\v 33 Njia ile ile aliyoijia ndiyo njia atakayoondokea; hatoingia mji huu hivi ndivyo asemavyo BWANA.”
\q
\v 34 Kwa maana nitaulinda huu mji na kuuokoa, kwa ajili yangu mwenyewe na kwa ajili ya Daudi mtumishi wangu.”’
\s5
\p
\v 35 Ikawa kuhusu usiku huo ambao malaika wa BWANA alitoka na kuvamia kambi ya Waashuru, akawaua maaskari mia themanini na tano elfu. Kisha watu wakaamka asubuhi na mapema, miili ya watu waliokuwa wamekufa ilikuwa imelala kila mahali.
\v 36 Hivyo Senakeribu mfalme wa Ashuru akaondoka Israeli na kwenda nyumbani na kuishi katika Ninawi.
\p
\v 37 Baadaye, alipokuwa akiabudu kwenye nyumba ya Nisroki mungu wake, watoto wake Adramaleki na Shareza wakamuua kwa upanga. Kisha wakakimbilia kwenye nchi ya Ararati. Kisha Esarhodani mwanaye akawa mfalme katika mahali pake.
\s5
\c 20
\cl Sura 20
\p
\v 1 Katika siku hizo Hezekia aliugua akawa kwenye hatari ya kufa. Hivyo Isaya mwana wa Amozi, akaja, na kumwambia, “BWANA asema, Weka nyumba yako kwenye mpangilio; kwa kuwa utakufa, na hutapona.’”
\p
\v 2 Kisha Ahazi akageuza uso wake kwenye ukuta na kumuomba BWANA, akisema,
\v 3 “Tafadhali, BWANA, ukumbuke jinsi nilivyo mwaminifu kutembea mbele yako kwa moyo wangu wote, na jinsi nilivyofanya yaliyo mazuri usoni kwako.” Kisha Hezekia akalia kwa sauti.
\s5
\p
\v 4 Kabla ya Isaya hajatoka nje kwenye mji wa kati, neno la BWANA likamjia, kusema,
\v 5 “Rudi, na umwambie Hezekia, kiongozi wa watu wangu, Hivi ndivyo BWANA, Mungu wa Daudi babu yako, asemavyo: Nimesikia maombi yako, na nimeyaona machozi yako. Nitakuponya katika siku ya tatu, na utapanda juu kwenye nyumba ya BWANA.
\s5
\v 6 Nitakuongeza miaka kumi na tano ya maisha yako, na nitakulinda na huu mji kwa ajili yangu na kwa ajili ya mtumishi wangu.’”
\p
\v 7 Hivyo Isaya akasema, “Chukueni mkate wa tini.” Walifanya hivyo na kuweka kwenye jipu lake, na akapona.
\s5
\p
\v 8 Hezekia akamwambia Isaya, “Je kutakuwa na alama gani ambayo BWANA ataniponya, na kwamba nitapanda juu hadi kwenye hekalu la BWANA katika siku ya tatu?”
\p
\v 9 Isaya akajibu, “Hii ndiyo itakuwa ishara kwako kutoka kwa BWANA kwamba BWANA atafanya kitu amacho alichokisema. Je kivuli kitaenda mbele hatua saba, au kurudi nyuma hatua saba?”
\s5
\p
\v 10 Hezekia akajibu, “Ni kitu chepesi kwa kivuli kwenda mbele hatua kumi. Hapana, hicho kivuli kirudi nyuma hatua kumi.”
\p
\v 11 Hivyo Isaya nabii akamlilia BWANA, na akaleta kivuli hatua kumi nyuma, kutoka pale ambapo zilikuwa zimevuka kwenye ngazi za Ahazi.
\s5
\p
\v 12 Katika kipindi hicho Merodak Baladani mfalme wa Babeli alituma barua na zawadi kwa Hezekia, kwa kuwa alisikia kwamba Hezekia alikuwa anaumwa.
\v 13 Hezekia akasikiliza hizo barua, na kisha kuwaonyesha wajumbe sehemu zote na sehemu zake za thamani, fedha, dhahabu, manukato na marhamu na nyumba yenye ghala la silaha zake, na yote yaliyokutwa kwenye ghala za nyumba zake. Hapakuwa na kitu kwenye nyumba, wala kwenye ufalme wake wote, ambao Hezekia hakuwaonyesha.
\s5
\p
\v 14 Kisha Isaya akaja kwa Hezekia na kumuuliza, “Hawa watu walikuwa wanakwambiaje? Wanatokea wapi?” Hezekia akasema, “Wamekuja kutoka nchi ya mbali ya Babeli.
\p
\v 15 Isaya akauliza, “Wameona nini kwenye nyumba yako?” Hezekia akajibu, “Wameona kila kitu kwenye nyumba yangu. Hakuna kitu miongoni mwa vitu vyangu vya thamani ambavyo sijawaonyesha.”
\s5
\p
\v 16 Basi Isaya akamwambia Hezekia, “Sikiliza neno la BWANA:
\v 17 Tazama siku zinakuja wakati kila kitu kwenye nyumba yako ya kifalme, vitu ambavyo baba zako walivitunza huko hadi leo, vitabebwa kwenda Babeli. Hakuna kitakachobakia, asema BWANA.
\v 18 Watoto waliozaliwa na wewe, ambao umewazaa wewe mwenyewe watawachukua mbali, na watakuwa matowashi kwenye nyumba ya kifalme ya mfalme wa Babeli.’”
\s5
\p
\v 19 Hezekia akamwambia Isaya, “Neno la BWANA uliloliongea ni jema.” Kwa kuwa alifikiri, Je sivyo ikiwapo amani na kweli katika siku zangu?”
\p
\v 20 Kama kwa mambo mengine yanamuhusu Hezekia, na ushujaa wake wote, na jinsi alivyotengeza bwawa la maji na mfereji, na kuleta maji kwenye mji-hayakuandikwa kwenye kitabu cha ya matukio ya wafalme wa Yuda?
\v 21 Hezekia akalala na baba zake, na Manase mwanae akawa mfalme katika sehemu yake.
\s5
\c 21
\cl Sura 21
\p
\v 1 Manase alikuwa na umri wa miaka kumi na mbili wakati alipoanza kutawala; alitawala miaka hamsini na tano katika Yerusalemu. Mama yake alikuwa anaitwa Hefziba.
\v 2 Alifanya maovu usoni kwa BWANA, kama machukizo ya mataifa ambayo BWANA aliyafukuza nje mbele ya wana wa Israeli.
\v 3 Kwa kupajenga tena mahala pa juu ambapo Hezekia baba yake alipaharibu, na akajenga madhabahu kwa ajili ya Baali, akafanya Ashera, kama Ahabu mfalme wa Israeli alivyofanya, akasujudu kwa nyota zote za mbinguni na kuwaabudu wao.
\s5
\v 4 Manase akajenga madhabahu za kipagani kwenye nyumba ya BWANA, ingawaje BWANA aliamuru, “Jina langu litakuwa Yerusalemu daima.”
\v 5 Akajenga madhabahu kwa ajili ya nyota zote za mbinguni katika behewa mbili za nyumba ya BWANA.
\v 6 Akamuweka mtoto wake wa kiume kwenye moto; akatazama bao, akafanya ushirikina na kujishuhulisha pamoja na wale ambao wenye pepo wa utambuzi na wale wachawi. Akafanya maovu mengi usoni mwa BWANA na kuchochea hasira kwa Mungu.
\s5
\p
\v 7 Sanamu ya kuchongwa ya Ashera ambayo aliitengeneza, akaiweka kwenye nyumba ya BWANA. Nyumba hii ndiyo ambayo BWANA alimwambia Daudi na Sulemani mwanawe; akisema: “Ni nyumba hii na katika Yerusalemu, ambayo nimeichagua kutoka makabila yote ya Israeli, ambako nitaliweka jina langu milele.
\v 8 Sitafanya miguu ya Israeli kushindwa tena nje ya nchi ambayo niliwapa babu zao, kama tu watakuwa makini kutii yale yote niliyowaamuru, na kufuata sheria zote ambazo mtumishi wangu Musa aliwaamuru.”
\v 9 Lakini watu hawakusikia, na Manase akawaongoza kufanya maovu zaidi kuliko yale ya mataifa ambayo BWANA aliyaharibu mbele ya watu wa Israeli.
\s5
\p
\v 10 Basi BWANA akaongea na watumishi wake manabii, akisema,
\v 11 “Kwa sababu Manase mfalme wa Yuda amefanya haya machukizo, na kutenda maovu zaidi kuliko yote waliyoyatenda Waamori ambao walikuwa mbele yake walikubali, na pia aliwafanya Yuda kuasi kwa sanamu zake,
\v 12 kwa hiyo BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi: Tazama, nakaribia kuleta uovu juu ya Yerusalemu na Yuda ambayo kila mtu asikiapo kuhusu hilo, masikio yake yote yatawasha.
\s5
\v 13 Nitanyoosha juu ya Yerusalemu kipimo kilichotumika dhidi ya Samaria, na kuangusha mstari utakaotumika dhidi ya nyumba ya Ahabu; Nitaifuta Yerusalemu safi, kama kufuta sahani, kuifuta na kuifunika juu chini.
\v 14 Nitawatupa masalia ya urithi wangu na kuwaweka mikononi mwa maadui zao. Watakuwa nyara na mateka kwa maadui zao wote,
\v 15 kwa sababu wamefanya yaliyo maovu usoni kwangu, na kunichochea hasira, tangu siku babu zao walipotoka Misri, hadi leo.’”
\s5
\p
\v 16 Aidha, Manase akazimwaga damu nyingi za wasio na hatia, hadi alipoijaza Yerusalemu kutoka upande huu kwenda mwingine kwa kifo. Hii ilikuwa ni kuongeza kwenye dhambi ambayo aliifanya Yuda kuasi, wakati walipofanya uovu mbele za BWANA.
\p
\v 17 Kama kwa mambo mengine yamhusuyo Manase, yote aliyoyafanya, na dhambi ambayo aliyoifanya, je haya hayajaandikwa kwenye kitabu cha matukio cha wafalme wa Yuda?
\v 18 Manase akalala pamoja na baba zake na alizikwa kwenye bustani ya nyumba yake, katika bustani ya Uza. Amoni mwanawe akawa mfalme katika sehemu yake.
\s5
\p
\v 19 Amoni alikuwa na miaka Ishirini na mbili alipoanza kutawala; alitawala miaka miwili katika Yerusalemu. Mama yake alikuwa anaitwa Meshlemethi; alikuwa binti wa Haruzi wa Yotba.
\v 20 Alifanya yaliyo maovu usoni mwa BWANA, kama manase baba yake alivyofanya.
\s5
\v 21 Amoni alifuata njia zote ambazo baba yake alizotembelea na kuabudu sanamu ambazo baba yake aliziabudu, na kuzisujudia.
\v 22 Akajitenga na BWANA Mungu wa baba zake, na hakutembea katika njia ya BWANA.
\v 23 Watumishi wa Amoni wakafanya njama dhidi yake na kumuua mfalme kwenye nyumba yake mwenyewe.
\s5
\p
\v 24 Lakini watu wa nchi wakawaua watu wote waliofanya njama dhidi ya mfalme Amoni, na wakamfanya Yosia mtoto wake kuwa mfalme katika sehemu yake.
\p
\v 25 Kama ilivyo kwa mambo mengine yamhusuyo Amoni yale aliyoyafanya, je hayajaandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Yuda?
\v 26 Watu wakamzika kwenye kaburi lake katika bustani ya Uza, na Yosia mwanawe akawa mfalme katika sehemu yake.
\s5
\c 22
\cl Sura 22
\p
\v 1 Yosia alikuwa na umri wa miaka minane wakati alipoanza kutawala; alitawala kwa mda wa miaka thelathini na moja katika Yerusalemu. Mama yake alikuwa anaitwa Yedida (Alikuwa binti wa Adaye wa Bozkathi).
\v 2 Alifanya yale yaliyo mema usoni mwa BWANA. Alitembea kwenye njia zote za Daudi baba yake, na hakugeuka wala upande wa kulia au kushoto.
\s5
\p
\v 3 Ikawa kwamba katika mwaka wa kumi na nane mfalme Yosia, akamtuma Shafani mwana wa Azalia mwana wa Meshulamu, mwandishi, kwenye nyumba ya BWANA, akisema,
\v 4 “Panda juu kwa Hilkia yule kuhani mkuu na mwambie ahesabu pesa ambazo zilizokuwa zimeletwa kwenye nyumba ya BWANA, ambazo walinzi wa hekalu wamezikusanya kutoka kwa watu.
\v 5 Zigawanywe kwenye mikono ya wafanyakazi ambao ni wasimamizi wa nyumba ya BWANA, na waache wawapatie wafanya kazi ambao wako kwenye nyumba ya BWANA, ili waweze kutengeneza pale palipoharibika.
\s5
\v 6 Wapewe pesa maseremala, wajenzi, na waashi, na pia kununua mbao na kukata jiwe kukarabati nyumba ya BWANA.”
\v 7 Lakini zile pesa hazikutakiwa kuhesabiwa wakati walipokuwa wanapewa, kwa sababu waliimudu ile kazi kwa uaminifu.
\s5
\p
\v 8 Hilkia kuhani mkuu akamwambia Shafani yule mwandishi, “Nimekipata kitabu cha sheria katika nyumba ya BWANA.” Basi Hilkia akampatia kile kitabu Shafani, na kukisoma.
\v 9 Shafani akaenda na kuchukua kile kitabu kwa mfalme, na pia kumjulisha, akisema, “Watumishi wako wamezitumia zile pesa ambazo zilizokuwa zimepatikana kwenye hekalu na zimegawiwa kwenye mikono ya wafanya kazi ambao husimamia kuangalia nyumba ya BWANA.”
\v 10 Kisha Shafani yule mwandishi akamwambia mfalme, “Hilkia yule kuhani amenipatia kitabu.” Kisha Shafani akakisoma mbele ya mfalme.
\s5
\p
\v 11 Ikawa kwamba wakati mfalme aliposikia maneno ya sheria, alichana nguo zake.
\v 12 Kisha mfalme akamwamuru Hilkia yule kuhani, Ahikamu mwana wa Shafani, Akbori mwana wa Mikaya, Shafani mwandishi, na Asaya, mtumishi wake mwenyewe, akisema,
\v 13 Nenda na ukaongee pamoja na BWANA kwa ajili yangu, na kwa ajili ya watu na kwa Yuda yote, kwa sababu ya maneno ya hiki kitabu ambacho kilichopatikana. Kwa hasira kubwa ya BWANA ambayo ametukasirikia dhidi yetu kwa sababu baba zetu hawakusikiliza maneno ya hiki kitabu hivyo kama kutii yote ambayo yalikuwa yameandikwa kuhusiana na sisi.
\s5
\p
\v 14 Basi Hilkia yule kuhani, Ahikamu, Akbori, Shafani, na Asaya wakaenda kwa Hulda nabii wa kike, mke wa Shalumu mwana wa Tikva mwana wa Harhasi, mtunza kabati la nguo (aliishi katika Yerusalemu katika mtaa wa pili), na wakaongea pamoja naye.
\p
\v 15 Akawaambia, “Hivi ndivyo BWANA, Mungu wa Israeli, asemavyo: Mwambie huyu mtu aliyekutuma kwangu,
\v 16 hivi ndivyo BWANA asemavyo: Tazama, nitaleta janga kwenye hii sehemu na juu ya wakaao hapa, kulingana na kila kitu kilichoandikwa kwenye kitabu ambacho mfalme wa Yuda alichokisoma.
\s5
\v 17 Kwa sababu wamenitelekeza na kufukiza ubani kwa miungu mingine, hivyo basi wanaweza kunichochea hasira pamoja na matendo yote waliyoyafanya, kwa hiyo hasira yangu ilikuwa inawaka dhidi ya hii sehemu, na haitazimika.”’
\v 18 Lakini kwa mfalme wa Yuda, aliye watuma kuuliza mapenzi ya BWANA, hivi ndivyo mtakavyo mwambia: “BWANA, Mungu wa Israeli asema hivi: Kuhusu yale maneno uliyoyasikia,
\v 19 kwa sababu moyo wako ulikuwa mlaini, na kwa sababu umejinyenyekesha mwenyewe mbele za BWANA, wakati uliposikia nilichokisema dhidi ya hii sehemu na wenyeji wake, kwamba wanaweza kuwa wakiwa na laana, na kwa sababu ulizozirarua nguo zako na kulia mbele yangu, Nami pia nimekusikia hivi ndivyo BWANA asemavyo.
\s5
\v 20 Tazama, nitakukusanya na baba zako, nawe utawekwa kaburini kwako kwa amani. Macho yako hayataona maafa yote ambayo nitayaleta kwenye hii sehemu.’” Hivyo watu wakachukua ujumbe huu kuurudisha kwa mfalme.
\s5
\c 23
\cl Sura 23
\p
\v 1 Hivyo mfalme akawatuma wajumbe waliokuwa wamemzunguka wazee wote wa Yuda na wa Yerusalemu.
\v 2 Kisha mfalme akapanda hadi kwenye nyumba ya BWANA, na watu wote wa Yuda na wenyeji wote wa Yerusalemu pamoja naye, na makuhani, manabii, na watu wote, kuanzia mdogo hadi mkubwa. Kisha akasoma masikioni kwao maneno yote ya kitabu cha agano ambalo lililokuwa limepatikana kwenye nyumba ya BWANA.
\s5
\v 3 Mfalme akasimama karibu na nguzo na kufanya agano mbele ya Yahwe, kutembea pamoja na Yahwe na kukumbuka maagizo yake, kanuni zake, na sheria zake, kwa moyo wake wote na kwa roho yake yote, kuthibitisha maneno ya hili agano ambalo lililokuwa limeandikwa kwenye hiki kitabu. Hivyo watu wote wakakubaliana kusimama kwenye agano
\s5
\p
\v 4 Mfalme akamwamuru Hilkia yule kuhani mkuu, makuhani chini yake, na walinzi wa lango watoe kwenye hekalu vyombo vilivyokuwa vimetengenezwa kwa ajili ya Baali na Ashera, na kwa ajili ya nyota zote za mbinguni. Akavichoma moto Yerusalimu kwenye mashamba ya bonde la Kidroni na kubeba majivu yake kwenda Betheli.
\v 5 Akawaondoa makuhani waliokuwa wanaabudu miungu ambao wafalme wa Yuda waliwachagua ili kwa ajili ya kufukiza ubani katika mahali pa juu kwenye miji ya Yuda na sehemu zinazoizunguka Yerusalemu wale waliokuwa wanachoma ubani kwa Baali, kwa jua na kwa mwezi, kwa sayari, na kwa nyota zote za mbinguni.
\s5
\v 6 Akaiondoa Ashera kutoka kwenye hekalu la BWANA, nje ya Yerusalemu hata bonde la Kidroni na kuichoma hapo. Akaipiga kwenye mavumbi na kuyatupa yale mavumbi kwenye makaburi ya watu wa kawaida.
\v 7 Akavisafisha vyumba vya makahaba ambao walikuwa kwenye hekalu la BWANA, ambako wanawake waliposhonea nguo kwa ajili ya Ashera.
\s5
\p
\v 8 Yosia akawaleta makuhani wote nje ya miji ya Yuda na kupanajisi mahali pa juu ambako makuhani walipokuwa wakichomea ubani, kutoka Geba hata Bersheba. Akapaharibu mahala pa juu kwenye malango ambayo yaliyokuwa ya kuingilia kwenda kwenye lango la Yoshua (liwali wa mji), upande wa kushoto wa lango la mji.
\v 9 Ingawa makuhani wa mahali pa juu hawakuruhusiwa kuhudumu kwenye madhabahu ya BWANA katika Yerusalemu, wakala mikate isiyotiwa chachu miongoni mwa ndugu zao.
\s5
\p
\v 10 Yosia akainajisi Tofethi, ambayo ipo kwenye bonde la Ben Hinomu, ili kwamba mtu yeyote asimuweke mtoto wake wa kiume au binti yake kwenye moto kama sadaka kwa Moleki.
\v 11 Akawachukua farasi ambao wafalme wa Yuda waliokuwa wametolewa kwa ajili ya jua. Walikuwa kwenye eneo la lango la kuingilia kwenye hekalu la BWANA, karibu na chumba cha Nathani Meleki, msimamizi mkuu wa nyumba ya mfalme. Yosia akayachoma yale magari ya farasi ya jua.
\s5
\p
\v 12 Yosia mfalme akayaharibu madhabahu yaliyokuwa kwenye dari ya juu ya chumba cha Ahazi, ambacho wafalme wa Yuda walikitengeneza, na madhabahu ambayo Manase aliyatengeneza kwenye behewa mbili za nyumba ya BWANA. Yosia akazivunga vipande vipande na kuvitupa kwenye bonde la Kidroni.
\v 13 Mfalme akapaangamiza mahali pa juu magharibi mwa Yerusalemu, kusini mwa mlima wa uharibifu ambapo Sulemani mfalme wa Israeli alipajenga kwa ajili ya Ashtorithi, chukizo la Wamoabu; sanamu za karaha za Wasidoni; kwa Kemoshi, sanamu za karaha wa Moabu; na kwa Moleki, sanamu wa karaha wa watu wa Amoni.
\v 14 Akazivunja nguzo za jiwe kuwa vipande vipande na kuziangusha chini nguzo za Ashera na kuzijaza zile sehemu kwa mifupa ya watu.
\s5
\p
\v 15 Yosia pia akaiteketeza kabisa madhabahu iliyokuwa Betheli na mahali pa juu ambako Yeroboamu mwana wa Nebati (ambaye aliwafanya Waisraeli kuasi) aliijenga. Pia aliichoma moto ile madhabahu na mahali pa juu na kupapiga hadi pakawa vumbi. Pia akaichoma moto nguzo ya Ashera.
\v 16 Yosia alipotazama kwenye lile eneo, akagundua kwamba yale makaburi yalikuwa juu ya mlima. Akawatuma watu kuichukua mifupa kutoka kwenye yale makaburi; kisha akaichoma kwenye madhabahu, akainajisi. Hii ilitokana na neno la BWANA ambalo mtu wa Mungu alilonena, yule mtu alikuwa amenena haya mambo kabla.
\s5
\p
\v 17 Kisha akasema, “Ni ukumbusho wa nani ule ninao uona?” Mtu wa ule mji akamwambia, “Lile ni kaburi la mtu wa Mungu ambaye alikuja kutoka Yuda na kutabiri kuhusu haya mambo ambayo umeyafanya dhidi ya madhabahu ya Betheli.”
\p
\v 18 Hivyo Yosia akasema, “Mwacheni. Mtu asihamishe mifupa yake.” Hivyo wakaacha mifupa yake, pamoja na mifupa ya nabii ambaye alikuja kutoka Samaria.
\s5
\p
\v 19 Kisha Yosia akahamisha nyumba zote za mahali pa juu ambazo zilikuwa katika mji wa Samaria, ambazo wafalme wa Israeli walizokuwa wamezitengeneza, na ambazo zilizokuwa zimemgadhabisha BWANA.
\v 20 Aliwafanyia kile ambacho kilikuwa kimefanyika katika Betheli. Aliwachinja makuhani wote wa mahali pa juu ya madhabahu na aliichoma mifupa ya watu juu yao. Kisha akarudi Yerusalemu.
\s5
\p
\v 21 Kisha mfalme akawaamuru watu wote, akisema, “Itunzeni Pasaka ya BWANA Mungu wenu, kama ilivyoandikwa kwenye hiki kitabu cha agano.”
\v 22 Hiyo Pasaka haijawahi kufanyika tangu siku za waamuzi ambao waliiongoza Israeli, wala katika siku zote za wafalme wa Israeli au Yuda.
\v 23 Lakini katika mwaka wa kumi na nane wa Mfalme Yosia Pasaka ya BWANA ilisheherekewa katika Yerusalemu.
\s5
\p
\v 24 Yosia pia akawafukuza wale ambao waliokuwa wameongea na wafu au na roho. Pia aliifukuza miungu ya sanamu, na vitu vyote ambavyo ni chukizo vilivyokuwa vinaonekana katika nchi ya Yuda na katika Yerusalemu, hivyo kwa kuthibitisha yale maneno ya sheria ambayo iliyokuwa imeandikwa kwenye kitabu cha Hilkia yule kuhani aliyekuwa amepatikana kwenye nyumba ya BWANA.
\v 25 Kabla ya Yosia, hapakuwa na mfalme kama yeye, aliyekuwa amemwelekea BWANA kwa moyo wake wote, roho yake yote, na nguvu zake zote, ambaye alifuata sheria zote za Musa. Hapakuwa na mfalme kama Yosia aliyeinuka baada ya yeye.
\s5
\p
\v 26 Walakini, BWANA hakugeuka kutoka kwenye ukali wa hasira yake, ambayo ilikuwa dhidi ya Yuda kwa waabudu wapagani wote pamoja ambao Manase aliokuwa amemgadhibisha.
\v 27 Hivyo BWANA akasema, “Pia nitaiondoa Yuda usoni kwangu, kama nilivyoiondoa Israeli, na nitautupilia mbali huu mji ambao nilio uchagua, Yerusalemu, na ile nyumba ambayo niliyokuwa nimesema, Jina langu litakuwa humo.”’
\s5
\p
\v 28 Kama kwa mambo mengine yanayo mhusu Yosia, kila kitu alichofanya, je vimeandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Yuda?
\p
\v 29 Katika siku zake, Farao Neko, mfalme wa Misri, alienda kupigana dhidi ya mfalme wa Ashuru huko mto Frati. Mfalme Yosia akaenda kuonana na Neco katika mapigano, na Neko akamuua huko Megido.
\v 30 Watumishi wa Yosia wakambeba kwenye gari la farasi akiwa amekufa kutoka Migido, kumleta Yerusalemu, na kumzika katika kaburi lake mwenyewe. Kisha watu wa nchi wakamchukua Yehoahazi mwana wa Yosia, wakamtia mafuta, na kumfanya kuwa mfalme katika mahali pake.
\s5
\p
\v 31 Yehoahazi alikuwa na umri wa miaka ishirini na tatu alipoanza kutawala, na alitawala miezi mitatu katika Yerusalemu. Mama yake alikuwa akiitwa Hamutali; alikuwa binti wa Yeremia wa Libana.
\v 32 Yehoahazi alifanya yaliyo maovu usoni kwa Yahwe, kama kila kitu ambacho babu zake walichokifanya.
\v 33 Farao Neko akamfunga gerezani huko Ribla katika nchi ya Hamathi, hivyo asiweze kutawala katika Yerusalemu. Kisha Neko akaitoza Yuda talanta mia moja za fedha na talanta moja ya dhahabu.
\s5
\v 34 Farao Neko akamfanya Eliakimu mwana wa Yosia mfalme katika mahali pa Yosia baba yake, na kubadilisha jina lake kuwa Yehoyakimu. Lakini akamchukua mfalme Yehoahazi kwenda Misri, na Yehoahazi akafia huko.
\p
\v 35 Yehoyakimu akalipa fedha na dhahabu kwa Farao. Ili akutane na amri ya Farao, Yehoyakimu akaitoza nchi na kulazimisha kila mtu miongoni mwa watu wa nchi wamlipe fedha na dhahabu kulingana na makadirio yao.
\s5
\p
\v 36 Yehoyakimu alikuwa na umri wa miaka ishirini na tano alipoanza kutawala, na alitawala miaka kumi na moja katika Yerusalemu. Mama yake alikuwa akiitwa Zebida; alikuwa binti wa Pedaia wa Ruma.
\v 37 Yehoyakimu akafanya yale yaliyo maovu usoni kwa BWANA, kama waliyoyafanya babu zake.
\s5
\c 24
\cl Sura 24
\p
\v 1 Katika siku za Yehoyakimu, Nebukadreza mfalme wa Babeli akaiteka Yuda; Yehoyakimu akawa mtumishi kwa muda wa miaka mitatu. Kisha Yehoyakimu akarudi na kuasi dhidi ya Nebukadreza.
\v 2 BWANA akatuma vikosi vya Wakaldayo dhidi ya Yehoyakimu, Washami, Wamoabu, na Waamoni; akawatuma dhidi ya Yuda kuiharibu. Hii ilikuwa ni kuthibitisha pamoja na neno la BWANA ambalo aliloliongea kupitia watumishi wake manabii.
\s5
\v 3 Ilikuwa baada ya muda mfupi kwenye kinywa cha BWANA kwamba hili likaja juu ya Yuda, kuwaondoa usoni mwa uso wake, kwa sababu ya dhambi za Manase, yote aliyoyafanya,
\v 4 na pia kwa sababu ya damu isiyokuwa na hatia aliyoimwaga, kwa kuijaza Yerusalemu kwa damu isiyokuwa na hatia. BWANA hakuwa tayari kusamehe hilo.
\s5
\p
\v 5 Kama kwa mambo mengine yanayomuhusu Yehoyakimu, na yote aliyoyafanya, je hayajaandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Yuda?
\v 6 Yehoyakimu akalala pamoja na wazee wake, na Yekonia mtoto wake akawa mfalme katika sehemu yake.
\s5
\p
\v 7 Mfalme wa Misri hakushambulia tena nje ya nchi yake, kwa sababu mfalme wa Babeli alikuwa amezishinda nchi zote ambazo zilikuwa zikitawaliwa na mfalme wa Misri, kutoka kwenye kijito cha Misri mpaka Mto wa Frati.
\s5
\p
\v 8 Yekonia alikuwa na umri wa miaka kumi na nane alipoanza kutawala; alitawala Yerusalemu miezi mitatu. Mama yake alikuwa anaitwa Nehushta; alikuwa binti wa Elnathani wa Yerusalemu.
\v 9 Alifanya yaliyo maovu usoni mwa BWANA; alifanya yale yote ambayo baba yake aliyafanya.
\s5
\p
\v 10 Katika kipindi hicho jeshi la Nebukadreza mfalme wa Babeli liliishambulia Yerusalemu na kuuzunguka mji.
\v 11 Nebukadreza mfalme wa Babeli akaja kwenye mji wakati maaskari wake walipokuwa wameuzunguka,
\v 12 na Yekonia mfalme wa Yuda akatoka nje kwenda kwa mfalme wa Babeli, yeye, mama yake, watumishi wake, watoto wake, na maafisa wake. Mfalme wa Babeli akamteka katika mwaka wa nane wa utawala wake.
\s5
\v 13 Nebukadreza akachukua kutoka pale vitu vyote vya thamani katika nyumba ya BWANA, na walio katika nyumba ya kifalme. Akavikata vipande vipande vitu vyote vya dhahabu ambavyo Sulemani mfalme wa Israeli alivitengeneza katika hekalu la BWANA, kama alivyokuwa amesema ingetokea.
\v 14 Akawachukua wote utumwani Yerusalemu, viongozi wote, na wapiganaji wote, mateka elfu kumi, na mafundi wote, na wafua vyuma. Hakuna aliyekuwa amesalia isipokuwa watu masikini katika nchi.
\s5
\p
\v 15 Nebukadreza akamchukua Yekonia utumwani Babeli, pia na mama yake na mfalme, wake, maafisa, na wakuu wa nchi. Akawachukua kwenda utumwani kutoka Yerusalemu mpaka Babeli.
\v 16 Wapiganaji wote, 7,000 kwa hesabu, na mafundi 1,000 na wafua vyuma, wote wanaostahili kumpiga mfalme wa Babeli aliwaleta hawa watu kwenye utumwa Babeli.
\v 17 Mfalme wa Babeli akamfanya Matania, kaka yake na baba yake na Yehokimu, mfalme katika sehemu yake, na kubadilisha jina lake kuwa Sedekia.
\s5
\p
\v 18 Sedekia alikuwa na umri wa miaka ishirini na moja wakati alipoanza kutawala; alitawala miaka kumi na moja katika Yerusalemu. Mama yake alikuwa anaitwa Hamutali; alikuwa binti wa Yeremia kutoka Libna.
\v 19 Alifanya yaliyo maovu machoni mwa BWANA; aliyafanya yale yote ambayo Yehokimu aliyoyafanya.
\v 20 Kupitia hasira ya BWANA, haya matukio yote yalitokea Yerusalemu na Yuda, hadi alipowaondoa kwenye uso wake. Kisha Sedekia akaasi dhidi ya mfalme wa Babeli.
\s5
\c 25
\cl Sura 25
\p
\v 1 Ilitokea kwamba katika mwaka wa tisa wa utawala wa mfalme Sedekia, katika mwezi wa kumi, na siku ya kumi ya huo mwezi, Nebukadreza mfalme wa Babeli alikuja pamoja na jeshi lake lote kwa ajili ya kupigana dhidi ya Yerusalemu. Akaweka kambi kuelekeana nayo, na wakajenga ukuta kuizunguka.
\v 2 Hivyo mji huo ulizungukwa mpaka miaka kumi na moja ya utawala wa Sedekia.
\v 3 Katika siku ya tisa ya mwezi wa nne wa huo mwaka, njaa ilikuwa kali sana kwenye huo mji kwamba hapakuwa na chakula kwa ajili ya watu wa nchi.
\s5
\v 4 Wakati huo ule mji ulikuwa umebomoka ndani, na wapiganaji wote wakakimbia usiku kwa njia ya lango kati ya kuta mbili, karibu na bustani ya mfalme, ingawa Wakaldayo walikuwa wote wameuzunguka mji. Mfalme akaenda kuelekea upande wa Araba.
\v 5 Lakini jeshi la Wakaldayo likamfuata mfalme Sedekia na kumchukua katika tambarare ya bonde la Mto Yoradani karibu na Yeriko. Jeshi lake lote lilitawanyika wakamwacha.
\s5
\v 6 Wakamkamata mfalme na kumleta mpaka kwa mfalme wa Babeli huko Ribla, ambapo walipitisha hukumu juu yake.
\v 7 Wakawachinja watoto wake mbele ya macho yake. Kisha wakamtoa macho Sedekia, wakamfunga pingu, na kumpeleka hadi Babeli.
\s5
\p
\v 8 Basi katika mwezi wa tano, katika siku ya saba ya mwezi, ambapo ulikuwa mwaka wa kumi na tisa wa utawala wa Nebukadreza mfalme wa Babeli, Nebuzaradani, mtumishi wa mfalme wa Babeli na amri jeshi wa walinzi wake, wakaja hadi Yerusalemu.
\v 9 Akaichoma moto nyumba ya BWANA, nyumba ya mfalme, na nyumba zote za Yerusalemu; pia kila jengo la muhimu katika mji akayachoma,
\v 10 kuta zote zilizoizunguka Yerusalemu, jeshi lote la Wababeli ambao walikuwa chini ya amri jeshi wa walinzi wakaziharibu.
\s5
\v 11 Basi watu waliokuwa wamebaki ambao walikuwa wameondoka katika mji, wale waliokuwa wameasi kwa mfalme wa Babeli, na mabaki ya watu Nebuzadani, amiri jeshi wa mlinzi, wakachukuliwa kwenda utumwani.
\v 12 Lakini amiri jeshi wa mlinzi aliwaacha baadhi ya maskini wa nchi ili wafanye kazi kwenye shamba la mizabibu na kulima.
\s5
\p
\v 13 Na zile nguzo za shaba ambazo zilikuwa kwenye nyumba ya Yahwe, na misimamio na bahari ya chuma ambayo ilikuwa kwenye nyumba ya Yahwe, Wakaldayo wakazivunja vipande vipande na kubeba shaba kuirudisha Babeli.
\v 14 Masufuria, mabeleshi, makasi, vijiko, na vyombo vyote vya shaba ambavyo kuhani alivyokuwa amevitunza kwenye hekalu- Wakaldayo wakavichukua vyote.
\v 15 Masufuria ya kuhamisha majivu na mabakuli ambayo yalikuwa yametengenezwa kwa dhahabu, na yale yaliyotengenezwa kwa fedha, yule nahodha wa mlinzi wa mfalme akavichukua pia.
\s5
\p
\v 16 Zile nguzo mbili, ile bahari, na vile vitako ambavyo Sulemani alivitengeneza kwa ajili ya nyumba ya Yahwe shaba ya vyombo hivyo vyote haikuwa na uzani.
\v 17 Urefu wa ile nguzo ya kwanza ulikuwa ridhaa kumi na nane, na kichwa cha shaba kilikuwa juu yake. Na urefu wa kichwa ulikuwa ridhaa tatu, pamoja na mapambo ya wavu na makomamanga yote yakizunguka kwenye hicho kichwa, vyote vilikuwa vimetengenezwa kwa shaba. Na ile nguzo nyingine ilikuwa vivyo hivyo kama ile ya kwanza pamoja na wavu wake.
\s5
\p
\v 18 Yule amiri jeshi wa mlinzi akamchukua Seraya kuhani mkuu, pamoja za Sefania, yule kuhani wa pili, na walinzi watatu wa kwenye lango.
\v 19 Kutoka mjini akamchukua mlinzi, afisa mmoja ambaye aliyekuwa msimamizi wa maaskari, na watu watano ambao walikuwa wakimshauri mfalme, ambao walikuwa bado katika mji. Pia alimchukua mfungwa wa afisa jeshi la mfalme, kwa ajili ya kuandika watu kwenye jeshi, pamoja na watu sitini muhimu kutoka hiyo nchi ambao walikuwa katika mji.
\s5
\v 20 Kisha Nebuzaradani, amiri wa mlinzi, akawachukua na kuwapeleka kwa mfalme Babeli huko Ribla.
\v 21 Mfalme wa Babeli akawaua huko Ribla katika nchi ya Hamathi. Kwa njia hii, Yuda akaiacha nchi yake kwenda utumwani.
\s5
\p
\v 22 Na wale watu waliokuwa wamebakia katika nchi ya Yuda, wale ambao Nebukadreza mfalme wa Babeli aliwaacha, akamuweka Gedalia mwana wa Ahikamu, mwana wa Shafani, msimamizi wao.
\v 23 Kisha wakati maamiri wote wa majeshi, wao na watu wao, waliposikia kwamba mfalme wa Babeli amemfanya Gedalia kuwa liwali, wakaenda kwa Gedalia huko Mispa. Hawa watu walikuwa Ishmaeli mwana wa Nethania, Yohanani mwana wa Karea, Seraya mwana wa Tanhumethi Mnetofa, na Yezania mwana wa Mmaaka wao na watu wao.
\p
\v 24 Gedalia akafanya kiapo kwa watu wake na kuwaambia, “Msiwaogope Wakaldayo. Muishi katika nchi na kumtumikia mfalme wa Babeli, na itakuwa vema kwenu.”
\s5
\p
\v 25 Lakini ilitokea kwamba katika mwezi wa saba Ishmaeli mwana wa Nethania mwana wa Elishama, kutoka familia ya kifalme, wakaja na watu kumi na kumshambulia Gedalia. Gedalia akafa, pamoja na watu wa Yuda na Wababeli ambao walikuwa pamoja nae huko Mizpa.
\v 26 Kisha wale watu wote, kutoka chini kwenda juu, na maamiri wa jeshi, wakainuka na kwenda Misri, kwa sababu walikuwa wanawaogopa Wababeli.
\s5
\p
\v 27 Ilitokea baadaye katika mwaka wa thelathini na saba wa utumwa wa Yekonia mfalme wa Yuda, katika mwezi wa kumi na mbili, siku ya ishirini na saba ya mwezi, Evil-merodaki mfalme wa Babeli akamtoa Yekonia mfalme wa Yuda kutoka gerezani. Hii ilitokea katika mwaka ambao Evil-Merodaki alipoanza kutawala.
\s5
\v 28 Akaongea naye kwa ukarimu na kumpatia kiti kizuri zaidi kuliko kile cha wafalme wengine ambao walikuwa pamoja naye Babeli.
\v 29 Evil-Merodaki akamvua Yekonia nguo za gerezani,
\v 30 na Yekinia akala siku zote kwenye meza ya mfalme katika maisha yake yote yaliyokuwa yamebakia.