\v 1 Paulo, aliyeitwa na Kristo kuwa mtume kwa mapenzi ya Mungu, na Sosthene ndugu yetu,
\v 2 kwa kanisa la Mungu lililoko Korintho, kwa wale ambao wamewekwa wakfu katika Yesu Kristo, ambao wameitwa kuwa watu watakatifu. Tunawaandikia pia wale wote wanaolitii jina la Bwana wetu Yesu Kristo katika mahali pote, Bwana wao na wetu.
\p
\v 3 Neema na amani iwe kwenu kutoka kwa Mungu Baba yetu na Bwana wetu Yesu Kristo.
\s5
\p
\v 4 Siku zote namshukru Mungu wangu kwa ajili yenu, kwa sababu ya neema ya Mungu ambayo Kristo Yesu aliwapa.
\v 5 Amewafanya kuwa matajiri katika kila njia, katika usemi na pamoja na maarifa yote.
\v 10 Sasa nawasihi kaka na dada zangu, kupitia jina la Bwana wetu Yesu Kristo, kwamba wote mkubali, na kwamba pasiwe na migawanyiko miongoni mwenu. Nawasihi kuwa muungane pamoja katika nia moja na katika kusudi moja.
\v 11 Kwani watu wa nyumba ya Kloe wamenitaarifu kuwa kuna mgawanyiko unaoendelea miongoni mwenu
\v 17 Kwa maana, Kristo hakunituma kubatiza bali kuhubiri injili. Hakunituma kuhubiri kwa maneno ya hekima ya kibinadamu, ili kwa nguvu ya msalaba wa Kristo isiondolewe.
\v 20 Yuko wapi mtu mwenye busara? Yuko wapi mwenye elimu? Yuko wapi msemaji mshawishi wa dunia hii? Je, Mungu hakuigeuza hekima ya dunia hii kuwa ujinga?
\v 26 Angalia wito wa Mungu juu yenu, kaka na dada zangu. Si wengi wenu mlikuwa na hekima katika viwango vya kibinadamu. Si wengi wenu mlikuwa na nguvu. Si wengi wenu mlizaliwa katika ukuu.
\v 27 Lakini Mungu alichagua vitu vijinga vya dunia ili kuviaibisha vyenye hekima. Mungu alichagua kilicho dhaifu katika dunia kukiaibisha chenye nguvu.
\v 28 Mungu alichagua kile kilicho cha hali ya chini na kilichodharauliwa katika dunia. Alichagua hata vitu ambavyo havikuhesabiwa kuwa kitu, kwa kuvifanya si kitu vitu vilivyo na thamani.
\v 30 Kwa sababu ya kile Mungu alichofanya, sasa mko ndani ya Kristo Yesu, ambaye amefanyika hekima kwa ajili yetu kutoka kwa Mungu. Alikuwa haki yetu, utakatifu na ukombozi.
\v 31 Kama matokeo, kama andiko lisemavyo, “Anayejisifu, ajisifu katika Bwana.”
\v 3 Na nilikuwa nanyi katika udhaifu, na katika hofu, na katika kutetemeka sana.
\v 4 Na ujumbe wangu na kuhubiri kwangu hakukuwa katika maneno ya ushawishi na hekima. Badala yake, yalikuwa katika kudhihirisha dalili za Roho na za nguvu,
\v 7 Badala yake, tunaizungumza hekima ya Mungu katika ukweli uliofichika, hekima iliyofichika ambayo Mungu aliichagua kabla ya nyakati za utukufu wetu.
\v 8 Hakuna yeyote wa watawala wa nyakati hizi aliyeijua hekima hii, Kama wangeifahamu katika nyakati zile, wasingelimsulubisha Bwana wa utukufu.
\v 9 Lakini kama ilivyoandikwa, “Mambo mbayo hakuna jicho limeyaona, hakuna sikio lililoyasikia, mawazo hayakufikiri, mambo ambayo Mungu ameyaandaa kwa ajili ya wale wampendao yeye.”
\v 11 Kwa kuwa nani afahamuye mawazo ya mtu, isipokuwa roho ya mtu ndani yake? Hivyo pia, hakuna ajuaye mambo ya ndani ya Mungu, isipokuwa Roho wa Mungu.
\v 13 Tunasema mambo haya kwa maneno, ambayo hekima ya mtu haiwezi kufundisha, lakini ambayo Roho hutufundisha. Roho hutafasiri maneno ya kiroho kwa hekima ya kiroho.
\v 3 Kwa kuwa ninyi bado ni wa mwilini. Kwa kuwa wivu na majivuno yanaonekana miongoni mwenu. Je, hamuishi kulingana na mwili, na je, hamtembei kama kawaida ya kibinadamu?
\v 4 Kwa kuwa mmoja husema, “Namfuata Paulo.” Mwingine husema “Namfuata Apolo,” hamuishi kama wanadamu?
\p
\v 5 Apolo ni nani? Na Paulo ni nani? Watumishi wa yule mliyemwamini, kwa kila ambaye Bwana alimpa jukumu.
\v 10 Kutokana na neema ya Mungu niliyopewa kama mjenzi mkuu, niliuweka msingi, na mwingine anajenga juu yake. Lakini mtu awe makini jinsi ajengavyo juu yake.
\v 13 kazi yake itafunuliwa, kwa mwanga wa mchana utaidhihirisha. Kwa kuwa itadhihirishwa na moto. Moto utajaribu ubora wa kazi wa kila mmoja alichofanya.
\v 4 Sijihukumu mimi mwenyewe, hii haina maana kuwa mimi ni mwenye haki. Ni Bwana anihukumuye.
\s5
\v 5 Kwa hiyo, msitamke hukumu juu ya lolote kabla ya wakati, kabla ya kuja kwa Bwana. Atayaleta nuruni mambo yaliyofichika gizani na kufunua makusudi ya mioyo. Ndipo kila mmoja atapokea sifa yake kutoka kwa Mungu.
\v 6 Sasa, kaka na dada zangu, mimi mwenyewe na Apolo tumetumia kanuni hizi kwa ajili yenu. Ili kwamba kutoka kwetu mnaweza kujifunza maana ya usemi, “Usiende zaidi ya kilivyoandikwa.” Hii ni kwamba hakuna mmoja wenu ajivunaye juu ya mwingine.
\v 7 Kwani ni nani aonaye tofauti kati yenu na mwingine? Ni kipi ulicho nacho hukukipokea bure? Kama umekwisha kupokea bure, kwa nini mnajivuna kama hamkufanya hivyo?
\v 8 Tayari mmeshapata vyote ambavyo mngetaka! Tayari mmekuwa na utajiri! Mmeanza kutawala; na kwamba mnamiliki zaidi yetu sisi! Kweli, nawatakia umililki mwema ili kwamba tumiliki pamoja nanyi.
\v 9 Kwa hiyo ninadhani Mungu ametuweka sisi mitume kama kutuonyesha wa mwisho katika mustari wa maandamano na kama watu waliohukumiwa kuuawa. Tumekuwa kama tamasha kwa ulimwengu, kwa malaika na kwa wanadamu.
\v 10 Sisi ni wajinga kwa ajili ya Kristo, lakini ninyi ni wenye hekima katika Kristo. Tu wanyonge, lakini ninyi mna nguvu. Mnaheshimiwa, lakini sisi tunadharauliwa.
\v 11 Hata saa hii tuna njaa na kiu, hatuna nguo, tuna mapigo, na tena hatuna mahali pa kuishi.
\v 17 Hiyo ndiyo sababu nilimtuma kwenu Timotheo, mpendwa wangu na mtoto mwaminifu katika Bwana. Atawakumbusheni njia zangu katika Kristo, kama ninavyofundisha kila mahali na kila kanisa.
\v 1 Tumesikia taarifa kuwa kuna zinaa miongoni mwenu, aina ya zinaa ambayo haipo hata katikati ya watu wa Mataifa. Tuna taarifa kwamba mmoja wenu analala na mke wa baba yake.
\v 6 Majivuno yenu si kitu kizuri. Hamjui chachu kidogo huharibu donge zima?
\v 7 Jisafisheni ninyi wenyewe chachu ya kale, ili kwamba muwe donge jipya, ili kwamba mwe mkate usiochachuliwa. Kwa kuwa, Kristo, Mwana Kondoo wetu wa pasaka amekwisha kuchinjwa.
\v 8 Kwa hiyo tusherekee karamu si kwa chachu ya kale, chachu ya tabia mbaya na uovu. Badala yake, tusherekee na mkate usiotiwa chachu wa unyenyekevu na kweli.
\v 9 Niliandika katika barua yangu kuwa msichangamane na wazinzi.
\v 10 Sikua na maananisha wazinzi wa dunia hii, au na wenye tamaa au wanyang'anyi au waabudu sanamu, kwa kukaa mbali nao, basi ingewapasa mtoke duniani.
\v 11 Lakini sasa nawaandikia kutojichanganya na yeyote anayeitwa kaka au dada katika Kristo, lakini anaishi katika uzinzi au ambaye ni mwenye kutamani, au mnyang'anyi, au mwabudu sanamu, au mtukanaji au mlevi. Wala msile naye mtu wa namna ile.
\v 12 Kwa hiyo nitajihusishaje kuwahukumu walio nje ya Kanisa? Badala yake, ninyi hamkuwahukumu walio ndani ya kanisa?
\v 13 Lakini Mungu anawahukumu walio nje. “Mwondoeni mtu mwovu miongoni mwenu.
\v 7 Ukweli ni kwamba kuna matatizo katikati ya Wakristo yaliyoleta tayari usumbufu kwenu. Kwanini msiteseke kwa mabaya? Kwanini mnakubali kudanganywa?
\v 11 Na hao walikuwa baadhi yao ni ninyi. Lakini mmekwisha kutakaswa, lakini mmekwisha kuoshwa, lakini mmekwisha kutengwa kwa Mungu, lakini mmefanywa haki mbele za Mungu katika jina la Bwana Yesu Kristo na kwa Roho wa Mungu wetu.
\v 12 “Vitu vyote ni halali kwangu,” lakini si kila kitu kina faida. “Vitu vyote ni halali kwangu,” lakini sitatawaliwa na kimoja cha hivyo.
\v 13 “Chakula ni kwa ajili ya tumbo, na tumbo ni kwa ajili ya chakula,” lakini Mungu atavitowesha vyote. Mwili haujaumbwa kwa ajili ya ukahaba, badala yake, mwili ni kwa ajili ya Bwana, na Bwana atauhudumia mwili.
\v 5 Msinyimane mnapolala pamoja, isipokuwa mmekubaliana kwa muda maalum. Fanyeni hivyo ili kupata muda wa maombi. Kisha mnaweza kurudiana tena pamoja, Ili kwamba Shetani asije akawajaribu kwa kukosa kiasi.
\p
\v 6 Lakini nasema haya mambo kwa hiari na si kama amri.
\v 12 Lakini kwa waliobaki, nasema- mimi, si Bwana- kwamba kama ndugu yeyote ana mke asiyeamini na anaridhika kuishi naye, hapaswi kumwacha.
\v 13 Kama mwanamke ana mume asiyeamini, na kama anaridhika kuishi naye, asimwache.
\v 14 Kwa mume asiyeamini anatakaswa kwa sababu ya imani ya mkewe. Na mwanamke asiyeamini anatakaswa kwa sababu ya mumewe aaminiye. Kama isingekua hivyo, watoto wenu wangekuwa si safi, lakini kwa kweli wametakaswa.
\v 27 Umefungwa kwa mwanamke na kiapo cha ndoa? Usitake uhuru kutoka kwa hiyo. Una uhuru kutoka kwa mke au hujaolewa? Usitafute mke.
\v 28 Lakini kama ukioa, hujafanya dhambi. Na kama mwanamke hajaolewa akiolewa, hajafanya dhambi. Bado wale wanaoana wanapata masumbufu ya aina mbalimbali. Nami nataka niwaepushe hayo.
\v 29 Lakini nasema hivi, kaka na dada zangu, muda ni mfupi. Tangu sasa na kuendelea, wale walio na wake waishi kama hawana.
\v 30 Wote walio na huzuni wajifanye kama walikuwa hawana huzuni, na wote wanaofurahi, kama walikuwa hawafurahi, na wote wanaonunua kitu chochote, kama hawakumiliki chochote.
\v 34 amegawanyika. Mwanawake asiyeolewa au bikira hujihusisha na vitu kuhusu Bwana, namna ya kujitenga katika mwili na katika roho. Lakini mwanamke aliyeolewa hujihusisha kuhusu vitu dunia, namna ya kumfurahisha mme wake.
\s5
\v 35 Nasema hivi kwa faida yenu wenyewe, na siweki mtego kwenu. Nasema hivi kwa vile ni haki, ili kwamba mnaweza kujiweka wakfu kwa Bwana bila kikwazo chochote.
\v 36 Lakini kama mtu anafikiri hawezi kumtendea kwa heshima mwanawali wake, kwa sababu ya hisia zake zina nguvu sana, acha aoane naye kama apendavyo. Siyo dhambi.
\v 37 Lakini kama amefanya maamuzi kutokuoa, na hakuna haja ya lazima, na kama anaweza kutawala hamu yake, atafanya vyema kama hatamwoa.
\v 4 Basi kuhusu kula vyakula vilivyotolewa sadaka kwa sanamu: twajua kuwa sanamu si kitu katika dunia hii, na ya kuwa hakuna Mungu ila mmoja tu.
\v 5 Kwa maana kuna wengi waitwao miungu ikiwa ni mbinguni au duniani, kama vile walivyo miungu na mabwana wengi.
\v 6 Ijapokuwa kwetu kuna Mungu mmoja tu ambaye ni Baba, vitu vyote vimetoka kwake, nasi tunaishi kwake, na Bwana mmoja Yesu Kristo, ambaye kwake vitu vyote vimekuwapo, na kwa yeye sisi tupo.
\v 7 Hata hivyo, ujuzi huu haupo ndani ya kila mmoja. Badala yake, wengine walishiriki ibada za sanamu hapo zamani, na hata sasa wanakula vyakula hivi kana kwamba ni kitu kilichotolewa sadaka kwa sanamu. Dhamiri zao zimepotoshwa kwa kuwa ni dhaifu.
\v 10 Hebu fikiri kwamba mtu amekuona, wewe uliye na ujuzi, unakula chakula katika hekalu la sanamu. Dhamiri yake mtu huyo haitathibitika hata yeye naye ale vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu?
\v 11 Kwa hiyo kwa sababu ya ufahamu wako wa ukweli juu ya asili ya sanamu, kaka au dada yako aliye dhaifu, ambaye pia Kristo alikufa kwa ajili yake, anaangamizwa.
\v 12 Hivyo, unapofanya dhambi dhidi ya kaka na dada zako na kuzijeruhi dhamiri zao zilizo dhaifu, mnatenda dhambi dhidi ya Kristo.
\v 7 Ni nani afanyaye kazi kama askari kwa gharama zake mwenyewe? Ni nani apandaye mzabibu na asile matunda yake? Au ni nani achungaye kundi asiyekunywa maziwa yake?
\p
\v 8 Je, ninasema haya kwa mamlaka ya kibinadamu? Sheria nayo haisemi haya?
\v 9 Kwa kuwa imeandikwa katika sheria ya Musa, “usimfunge ng'ombe kinywa apulapo nafaka.” Ni kweli kwamba hapa Mungu anajali ng'ombe?
\v 10 Au je, hasemi hayo kwa ajili yetu? Imeandikwa kwa ajili yetu, kwa sababu yeye alimaye nafaka inampasa kulima kwa matumaini, naye avunaye inampasa avune kwa matarajio ya kushiriki katika mavuno.
\v 12 Ikiwa wengine walipata haki hii kutoka kwenu, Je! Sisi si zaidi? Hata hivyo, hatukuidai haki hii. Badala yake, tulivumilia mambo yote badala ya kuwa kikwazo cha injili ya Kristo.
\v 13 Hamjui ya kuwa wote wafanyao kazi hekaluni hupata chakula chao kutoka hekaluni? Hamjui ya kuwa wote watendao kazi madhabahuni hupata sehemu ya kile kilichotolewa madhabahuni?
\v 15 Lakini sijawadai haki zote hizi. Na siandiki haya ili jambo lolote lifanyike kwa ajili yangu. Ni heri mimi nife kuliko mtu yeyote kubatilisha huku kujisifu kwangu.
\v 18 Basi thawabu yangu ni nini? Ya kuwa nihubiripo, nitaitoa injili pasipo gharama na bila kutumia kwa utimilifu wa haki yangu niliyonayo katika Injili.
\v 20 Kwa Wayahudi nilikuwa kama Myahudi, ili niwapate Wayahudi. Kwa wale walio chini ya sheria, nilikuwa kama mmoja wao aliye chini ya sheria ili niwapate wale walio chini ya sheria. Nilifanya hivyo ingawa mimi binafsi sikuwa chini ya sheria.
\v 21 Kwa wale walio nje ya sheria, nilikuwa kama mmoja wao nje ya sheria, ingawa mimi binafsi sikuwa nje ya sheria ya Mungu, bali chini ya sheria ya Kristo. Nilifanya hivyo ili niwapate wale walio nje ya sheria.
\v 22 Kwa walio wanyonge nilikuwa mnyonge, ili niwapate walio wanyonge. Nimekuwa hali zote kwa watu wote, ili kwa njia zote nipate kuwaokoa baadhi.
\v 24 Hamjui ya kuwa katika mbio wote washindanao hupiga mbio, lakini apokeaye tuzo ni mmoja? Hivyo pigeni mbio ili mpate tuzo.
\v 25 Mwana michezo hujizuia katika yote awapo katika mafunzo. Hao hufanya hivyo ili wapokee taji iharibikayo, lakini sisi tunakimbia ili tupate taji isiyoharibika.
\v 26 Kwa hiyo mimi sikimbii bila sababu au napigana ngumi kama kupiga hewa.
\v 7 Msiwe waabudu sanamu, kama wengi wao walivyokuwa. Hii ni kama ilivyoandikwa, “Watu walikaa chini wakila na kunywa, na waliinuka kucheza kwa tamaa za mapenzi.”
\v 13 Hakuna jaribu lililowapata ninyi lisilo kawaida ya wanadamu. Ila Mungu ni mwaminifu. Hatawaacha mjaribiwe kupita uwezo wenu. Pamoja na jaribu yeye atawapa mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili.
\v 20 Lakini nasema juu ya vitu vile wavitoavyo sadaka watu wapagani wa Mataifa, ya kuwa wanatoa vitu hivi kwa mapepo na sio kwa Mungu. Nami sitaki ninyi kushirikiana na mapepo!
\v 21 Hamwezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mapepo. Hamwezi kuwa na ushirika katika meza ya Bwana na katika meza ya mapepo.
\v 33 Jaribuni kama mimi ninavyojaribu kuwapendeza watu wote kwa mambo yote. Sitafuti faida yangu mwenyewe, bali ya wengi. Nami nafanya hivi ili wapate kuokolewa.
\v 6 Ikiwa kama mwanamke hatafunika kichwa chake, na akatwe nywele zake ziwe fupi. Maana ikiwa ni aibu mwanamke kukata nywele zake au kunyolewa, basi afunike kichwa chake.
\v 22 Je hamna nyumba za kulia na kunywea? Je mnalidharau kanisa la Mungu na kuwafedhehesha wasio na Kitu? Niseme nini kwenu? Niwasifu? Sitawasifu katika hili!
\v 25 Na vivi hivi akachukua kikombe baada ya kula, na kusema, “Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu. Fanyeni hivi mara nyingi kila mywapo, kwa kunikumbuka mimi.”
\v 34 Mtu akiwa na njaa, na ale nyumbani kwake, ili kwamba mkutanikapo pamoja isiwe kwa hukumu. Na kuhusu mambo mengine mliyoandika, nitawaelekeza nitakapokuja.
\v 1 Kuhusu karama za rohoni, kaka na dada zangu sitaki mkose kufahamu.
\v 2 Mwajua ya kuwa mlipokuwa wapagani mliongozwa kufuata sanamu zisizoongea, kwa njia zozote mliongozwa nazo.
\v 3 Kwa hiyo, nataka mfahamu kwamba hakuna yeyote anenaye kwa Roho wa Mungu akisema, “Yesu amelaaniwa.” Hakuna yeyote atakayesema, “Yesu ni Bwana,” isipokuwa katika Roho Mtakatifu.
\s5
\p
\v 4 Basi kuna karama tofauti tofauti, bali Roho ni yeye yule.
\v 5 Na kuna huduma tofauti tofauti, bali Bwana ni yeye yule.
\v 9 Kwa mwingine humpa imani kwa Roho yeye yule, na kwa mwingine karama ya uponyaji kwa Roho mmoja.
\v 10 Kwa mwingine matendo ya nguvu, na mwingine unabii. Na kwa mwingine uwezo wa kupambanua roho, mwingine aina mbalimbali za lugha, na kwa mwingnine tafsiri za lugha.
\v 13 Kwa maana katika Roho mmoja sisi sote tulibatizwa kuwa mwili mmoja, kwamba tu Wayahudi au Wayunani, kwamba tu watumwa au huru, na wote tulinyweshwa Roho mmoja.
\v 24 Na sasa viungo vyetu vilivyo na mvuto havina haja ya kupewa heshima, kwa kuwa tayari vina heshima. Lakini Mungu ameviunganisha viungo vyote pamoja, na amevipa heshima zaidi vile visivyo heshimiwa.
\v 28 Na Mungu ameweka katika kanisa kwanza mitume, pili manabii, tatu waalimu, kisha wale wote watendao matendo makuu, kisha karama za uponyaji, wale wasaidiao, wale wafanyao kazi ya kuongoza, na wote walio na aina mbalimbali za lugha.
\v 1 Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, lakini kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo au upatu uvumao.
\v 2 Tena nijapokuwa nina karama ya unabii na ufahamu wa kweli zilizofichika na maarifa, na kwamba ninayo imani ya kuhamisha milima, lakini ikiwa sina upendo, mimi si kitu.
\v 3 Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha masikini, tena nikiutoa mwili wangu nichomwe moto, lakini kama sina upendo, hainifaidii kitu.
\s5
\p
\v 4 Upendo huvumilia na hufadhili. Upendo haujisifu au kujivuna. Hauna kiburi
\v 5 au ukorofi. Hautafuti mambo yake, hauoni uchungu haraka, wala hauhesabu mabaya.
\v 6 Haufurahii udhalimu. Badala yake, hufurahi katika kweli.
\v 11 Nilipokuwa mtoto, nilisema kama mtoto, nilifikiri kama mtoto, niliamua kama mtoto. Nilipokuwa mtu mzima, niliweka mbali nami mambo ya kitoto.
\v 12 Kwa kuwa sasa tunaona kama kwa kioo, kama sura gizani, lakini wakati ule tutaona uso kwa uso. Sasa ninajua kwa sehemu, lakini wakati ule nitajua sana kama na mimi ninavyojulikana sana.
\v 5 Sasa natamani kwamba ninyi nyote mnene kwa lugha. Lakini zaidi ya hayo, natamani ya kwamba mtoe unabii. Yeye atoaye unabii ni mkuu kuliko yeye anenaye kwa lugha (labda awepo wa kutafasiri), ili kwamba kanisa lipate kujengwa.
\v 6 Lakini sasa, kaka na dada zangu, nikija kwenu na kunena kwa lugha, nitawafaidia nini ninyi? Siwezi, isipokuwa nasema nanyi kwa njia ya ufunuo, au kwa njia ya maarifa, au unabii, au kwa njia ya fundisho.
\v 20 Kaka na dada zangu, msiwe watoto katika kufikiri kwenu. Badala yake, kuhusiana na uovu, iweni kama watoto wachanga. Lakini katika kufikiri kwenu mkawe watu wazima.
\v 21 Imeandikwa katika sheria, “Kwa watu wa lugha nyingine na kwa midomo ya wageni nitasema na watu hawa. Wala hata hivyo hawatanisikia,” asema Bwana.
\v 26 Nini kifuatacho basi, kaka na dada zangu? Mnapokutana pamoja, kila mmoja ana Zaburi, mafundisho, mafunuo, lugha au tafsiri. Fanyeni kila kitu ili kwamba mlijenge kanisa.
\v 27 Kama yeyote ananena kwa lugha, wawepo wawili au watatu, na kila mmoja katika zamu. Na mtu lazima atafasiri kilichosemwa.
\v 34 imewapasa wanawake wakae kimya katika kanisa. Kwa kuwa hawaruhusiwi kuzungumza. Badala yake, wanapaswa kuwa katika unyenyekevu, kama pia sheria inavyosema.
\v 35 Kama kuna chochote wanatamani kujifunza, basi wawaulize waume zao nyumbani. Kwa kuwa ni aibu kwa mwanamke kuongea katika kanisa.
\v 10 Lakini kwa neema ya Mungu nipo kama nilivyo, na neema yake kwangu haikuwa bure. Badala yake, nilifanya bidii kuliko wote. Lakini haikuwa mimi, bali neema ya Mungu iliyo ndani yangu.
\v 27 Kwa kuwa “ameweka kila kitu chini ya nyayo zake.” Lakini inaposema “ameweka kila kitu,” ni wazi kwamba hii haihusishi wale walioweka kila kitu chini yake mwenyewe.
\v 28 Wakati vitu vyote vimewekwa chini yake, kisha Mwana mwenyewe atawekwa chini kwake Yeye ambaye aliviweka vitu vyote chini yake. Hii itatokea ili kwamba Mungu Baba awe yote katika vyote.
\v 31 Kaka na dada zangu, kupitia kujisifu kwangu katika ninyi, ambayo ninayo katika Kristo Yesu Bwana wetu, natangaza hivi: nakufa kila siku.
\v 32 Inanifaidia nini, katika mtazamo wa wanadamu, kama nilipigana na wanyama wakali huko Efeso, kama wafu hawafufuliwi? “Acha basi tule na kunywa, kwa kuwa kesho tunakufa.”
\v 39 Miili yote haifanani. Isipokuwa, kuna mwili mmoja wa wanadamu, na mwili mwingine wa wanyama, na wili mwingine wa ndege, na mwingine kwa ajili ya samaki.
\v 41 Kuna utukufu mmoja wa jua, na utukufu mwingine wa mwezi, na utukufu mwingine wa nyota. Kwa kuwa nyota moja inatofautiana na nyota nyingine katika utukufu.
\v 47 Mtu wa kwanza ni wa dunia, alitengenezwa kwa mavumbi. Mtu wa pili alitoka mbinguni.
\v 48 Kama vile yule aliyetengenezwa kwa mavumbi, hivyo pia wale waliotengenezwa kwa mavumbi. Kama vile mtu wa mbinguni alivyo, hivyo pia wale wa mbinguni.
\v 52 Tutabadilishwa katika wakati, katika kufumba na kufumbua kwa jicho, katika tarumbeta ya mwisho. Kwa kuwa tarumbeta italia, na wafu watafufuliwa na hali ya kutoharibika, na tutabadilishwa.
\v 54 Lakini wakati huu wa kuharibika ukivikwa wa kutokuharibika, na huu wa kufa ukivaa wa kutokufa, ndipo utakuja msemo ambao umeandikwa, “Kifo kimemezwa katika ushindi.”
\q1
\v 55 “Kifo, ushindi wako uko wapi? Kifo, uko wapi uchungu wako?”
\v 58 Kwa hiyo, wapendwa kaka na dada zangu, iweni imara na msitikisike. Daima itendeni kazi ya Bwana, kwa sababu mnajua kuwa kazi yenu katika Bwana siyo bure.
\v 2 Katika siku ya kwanza ya wiki, kila mmoja wenu aweke kitu fulani kando na kukihifadhi, kama muwezavyo. Fanyeni hivyo ili kwamba kusiwe na michango wakati nikija.
\v 12 Sasa kuhusiana na ndugu yetu Apolo. Nilimtia moyo sana kuwatembelea ninyi pamoja na ndugu. Lakini aliamua kutokuja kwa sasa. Hata hivyo, atakuja wakati ana nafasi.
\v 15 Mnaijua kaya ya Stefana. Mnajua kwamba walikuwa waamini wa kwanza huko Akaya, na kwamba walijiweka wenyewe kwenye huduma ya waumini. Na sasa nawasihi, kaka na dada zangu,