# Kwa ajili yako "Kwa niaba yako" # Nimebeba lawama Lawama za adui wa mwandishi zinazungumziwa kana kwamba ni mzigo mzito ambapo alitakiwa kubeba. "Nimevumilia matusi ya adui zangu" # aibu imefunika uso wangu Mwandishi anazungumzia aibu anayoihisi kana kwamba ni kitu kibaya usoni pake ambacho kila mtu anakiona vizuri. "Nimeaibika sana" # Nimekuwa mgeni kwa ndugu zangu Mwandishi anajizungumzia mwenyewe kana kwamba hakuwa sehemu ya familia yake mwenyewe. "Ndugu zangu hawanijui tena au kunikubali kabisa" # mgeni kwa ndugu zangu ... mgeni kwa watoto wa mama yangu Misemo hii miwili inamaana moja. Inarudiwa kusisitiza mtengano na familia yake mwenyewe. # mgeni kwa watoto wa mama yangu Mwandishi anajizungumzia mwenyewe kana kwamba hakuwa sehemu ya familia yake mwenyewe. "ndugu zangu hawanijui tena au kuniamini kabisa" # ari ya nyumba yako imenila Mwandishi anazungumzia ari kwa ajili ya hekalu la Mungu kana kwamba ni mnyama pori unaommeza mwandishi. "ari niliyonayo kwa ajili ya nyumba yako inanimeza" # imenila Lahaja hii inamaanisha ari ya mwandishi kwa ajili ya hekalu inateka mawazo na matendo yake yote. "inatawala kabisa kila kitu nachowaza na kufanya" # lawama ... zimeniangukia Mwandishi anazungumzia lawama za adui wa Mungu kana kwamaba ni mawe yaliyopondwa kwa mwandishi. "wale wanaokulaumu piwa wanatuma lawama zao kwangu"