# wewe ni duni sana, wakuhuzunikiwa, maskini, kipofu na uchi Yesu anazungumzia hali yao ya kiroho kama vile anazungumzia hali yao ya kimwili. "Nyie ni kama watu duni sana, wakusikitisha, maskini, vipofu, na uchi." # Nunua kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto Dhahabu iliyo safishwa katika moto ni safi na ya dhamani sana. Hapa wokovu ambao Yesu anawapa binadamu unazungumziwa kama dhahabu. "Pokeeni kutoka kwangu kilicho cha dhamani zaidi kama vile ni dhahabu iliyotakaswa katika moto." # upate kuwa tajiri Hii humaanisha utajiri wa kiroho, kuishi maisha yenye dhamani sana mbele za Mungu. "wawe matajiri kiroho" au "aishi maisha ya dhamani zaidi" # nguo nyeupe za kumetameta Nguo nyeupe zinaonesha utakatifu. "utakatifu kama nguo nyeupe" # upate kuona Kuona inamaanisha kuelewa ukweli.